Na Oscar Assenga, Tanga.
MICHUANO ya Copa Coca
Cola ngazi ya wilaya ya Tanga inatarajiwa kuanza kutimua vumbi April 25 hadi
Mei 31 mwaka huu katika viwanja ambavyo vitapendekezwa na itashirikisha timu
zenye wachezaji chini ya umri wa miaka 15.
Akizungumza blogi hii,Katibu
Msaidizi wa Chama cha Soka wilaya ya Tanga,Salim Carlos alisema mashindano hayo
yatakuwa tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma ambayo ilikuwa ikishirikisha
vijana wenye umri chini ya umri wa miaka 17 toka kwenye klabu zilizokuwa na
usajili wa kudumu na kituo.
Carlos alisema kutokana na utaratibu mpya wa mashindano hayo yataitwa FIFA Copa Coca Cola under 15 na yatashirikisha timu za shule za sekondari na vituo vya kukuzia vipaji vilivyo sajiliwa kwa mujibu wa sheria zilizopo za soka.
Aliongeza kuwa timu
itakayokuwa mshindi katika michuano hiyo ndio itakuwa bingwa wa wilaya ya
mashindano hayo ambapo jumla ya shule za sekondari 10 zinatarajiwa kushiriki
katika mashindano hayo.
Katibu huyo alizitaja
timu ambazo mpaka sasa zimethibitisha kushiriki kwa kujitokeza kuchukua fomu ni
mbili tu ambazo ni Mikanjuni sekondari na Hotel sekondari ambapo fomu za
ushiriki zilianza kutoka tangia April 15 mwaka huu.
Aidha aliongeza kuwa
wachezaji ambao wataruhusiwa kushiriki mashindano hayo ni wenye umri chini ya
miaka 15 pamoja na kuwa na fomu za usajili ambapo watatakiwa kuambatanisha na
vyeti halisi vya kuzaliwa.
Alieleza kuwa fomu
ambazo zitaweza kupokelewa ni zile ambazo zimekamilika zikiwa na TSM.9 au
nakala iliyochukuliwa na mamlaka husika na usajili wake ulianza Machi 19 mwaka
huu na utamalizika April 22 mwaka huu.
Mwisho.
“Majuto Units kuachia “Kitu Bomba”
Na Oscar Assenga, Tanga.
KUNDI la Filamu la
Majuto Units lenye makazi yake jijini Tanga linatarajiwa kutoa filamu yao ya
inayokwenda kwa jina la Kitu Bomba ambayo ilikuwa ni filamu ya mwisho kati ya
Msanii Sharomillionea na Mzee Majuto.
Akizungumza na blog hii, Hamza Majuto ambaye ni msemaji wa familia hiyo alisema filamu
hiyo ilianza kuachiwa mwezi uliopita iliweza kuvunja rekodi ya mauzo yake baada
ya kuuza nakala zaidi ya 10,000 sokoni kutokana na kupokewa vema na mshabiki
wao.
Hamza alisema filamu
hiyo ilikuwa imebeba mandhari ya ukimwi jinsi unavyohatarisha maisha ya watu
kutokana na maambukizo wanayokuwa wakiyapata.
Akizungumzia soko la
filamu lilivyo hapa nchini tofauti na miaka ya nyuma, Hamza alisema zamani
wasanii wa filamu wakiwa wakicheza kazi zao kutokana na hobi lakini hivi sasa
imejeuka kuwa ajira ambayo inaweza kuwainua watu kutoka katika maisha duni na
kuelekea kwenye maisha mazuri na yenye kipato kizuri.
Akizungumzia mtu ambaye
alikuwa akimvutia katika tasnia hiyo ya filamu kabla ya kuanza kuingia rasmi
alisema miongoni mwa wasanii ambao walikuwa wakimvutia sana ni marehemu Steven
Kanumba tokea akiwa chuo kikuu jijini Dar es Salaam UDSM.
Aidha alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dokta Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwasaidia wasanii hapa nchini ambapo alisema juhudi za kiongozi huyo zinapaswa kuigwa na viongozi waliopo chini yake ili wasanii waweze kuona matunda yao nao na sio kumtakisha tama.
Mwisho.
Na Oscar Assenga, Tanga.
CHAMA cha Mpira wa Wavu
Tanzania (TAVA) kinatarajiwa kufanya mkutano mkuu wa uchaguzi Mei 18 mwaka huu
katika ukumbi wa Hotel ya Mkonge jijini Tanga ambapo nafasi mbalimbali
zinatarajiwa kugombewa katika uchaguzi huo.
Akizungumza
na Blogii hii,Mwenyekiti wa Chama hicho,Augustino Agapa alisema maandalizi ya uchaguzi
huo yanaendelea vizuri na kila kitu kimekamilika kwa asilimia kubwa ambapo
wajumbe watakuwa ni makatibu wa vyama vya mikoa vilivyojishirikisha na TAVA na
kamati ya utendaji wanaomaliza muda wao.
Agapa alizitaja nafasi
ambazo zinatarajiwa kugombewa katika nafasi hiyo kuwa Mwenyekiti wa chama
hichoi,Makamu wa kwanza mwenyekiti wa mipango na maendeleo,makamu wa pili wa
mwenyekiti wa fedha na utawala,Katibu Mkuu,Naibu Katibu Mkuu
Aidha alizitaja nafasi nyengine zinazogombewa kuwa
ni Mwenyekiti wa kamati ya ufundi,Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya shule na
vyuo,Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya mikoa,mwenyekiti wa kamati ya
maendeleo ya waamuzi na Mwenyekiti wa Kamati ya maendeleo ya makocha.
Nafasi
nyengine zitakazogombewa kuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya mpira wa
ufukweni, Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya wanawake,Mwenyekiti wa kamati ya
maendeleo ya watoto
Mwenyekiti huyo alisema uchaguzi wa TAVA utasimamiwa
na Baraza la michezo la Taifa kwa mujibu wa katiba ya TAVA na Utaratibu wa fomu
za wagombea utatolewa muda mfupi ujao.
Mwisho.
EmoticonEmoticon