MKUU wa wilaya ya
Mkinga, Mboni Mgazi amewaagiza viongozi wa vijiji na kata kuendelea kuwahimiza
wananchi kupanda miti kwenye maeneo yao na kuhakikisha wanaitunza ili iweze
kukua na kutumika kw
malengo yanayotarajiwa.
Agizo la Mkuu wa wilaya alilitoa
leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya kupanda miti kiwilaya iliyofanyika kwenye
kata ya Duga Maforoni wilayani humo katika hotuba yake ambayo ilisomwa na Afisa
Tarafa ya Mkinga, Qegen Mkinga ambapo
amesema wiki hiyo ya kupanda miti ililengwa makusudi ya kuwahimiza wananchi
kushiriki katika mchakato huo wa upandaji na kutunza mazingira katika maeneo
yao.
Mgaza amesema mabadiliko
mbalimbali ya tabia ya nchini ambayo yanachangiwa na shughuli za kibinadamu
ikiwemo ukataji miti usiozingatiwa urushiaji huleta madhara mbalimbali ikiwemo
kupata mvua zisizo za uhakika, ongezeko la joto duniani na upungufu wa
rasilimali zinazotokana na miti pamoja na kukauka kwa vyanzo vya maji.
Amesema licha ya kuleta
madhara hayo huchangia pia ongezeko la magonjwa ya mlipuko pamoja na kuongezeka
kina cha bahari hivyo kuwataka wananchi kutoruhusu ukataji wa miti ovyo kwenye
maeneo yao kwani athari watakazo kumbana nazo ni kubwa kuliko wanavyodhani.
Aidha amesema kutokana
na upungufu wa miti ya asili jamii imehamishia matumizi kwenye miti ya matunda
kama vile mikorosho, miembe, minazi na mifenesi ambayo sasa inapasuliwa mabo
kwa matumizi mbalimbali ambapo aliwataka wananchi wafuate ushauri wa kitaalamu
na sio kujichukulia sheria mikononi za kuikata.
Mkuu huyo wa wilaya
amesema wilaya hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wilayani humo
wanajukumu la kutoa elimu ya upandaji wa miti kwa wananchi wa kuanzia ngazi za
vijiji na kata pamoja na kukemea uharibifu wa mazingira.
Pamoja na hayo alisema wilaya hiyo imepanga
kupanda miti 810,000 hasa katika maeneo yote yenye vyanzo vya maji ikiwemo
kuwahimiza wananchi kuisimamia na kuilanda ili iweza kukua na kutunza mazingira
yao siku zijazo.
Alisema hata hiyo wanajukumu la kuongeza kasi ya upandaji miti ili kukabiliana na upungufu wa miti uliopo na mabadiliko ya tabia ya nchi vile vile kufikia lengo lililowekwa na Taifa la kila wilaya kupanda miti 1,000,000 kila mwaka.
Katika uzinduzi huo
jumla ya miti 100 ilipandwa katika maeneo yaliyopo pembezoni mwa vyanzo vya
maji ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuendelea wiki nzima.
Mwisho.
EmoticonEmoticon