KAMPUNI ya ORYX Energies Tanzania kwa kushirikiana na Serikali na wadau wa soko, wamezindua mfumo wa kwanza wa usambazaji wa gesi ya LPG kwa wingi katika Soko la Samaki la Kimataita Ferry jijini Dar es Salaam ambapo unakwenda kuimarisha upatikanaji wa nishati safi kwa wauzaji wa samaki na wajasiriamali wadogo katika soko hilo.
AGIZO LA MINADA YOTE NCHINI KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA LAANZA KUTEKELEZWA
habari📌 *Wachoma nyama na Mama Lishe katika mnada wa Msalato Dodoma waanza kuonja matunda ya Nishati Safi ya Kupikia;*
📌 *Dkt. Biteko asema ni matunda ya Rais, Dkt. Samia ambaye anafahamu machungu ya kutumia Nishati isiyo safi ya Kupikia*
📌 *Atoa maagizo kwa Mkurugenzi Jiji la Dodoma kuweka miundombinu itakayohakikisha majiko ya Nishati Safi ya Kupikia ya Wachoma nyama yanakuwa salama*
📌 *Apongeza REA, Wizara ya Nishati kutekeleza agizo alilolitoa: STAMICO yatakiwa kuweka kituo cha kudumu cha mkaa mbadala Mnada wa Msalato*
📌 *Kituo kikubwa cha kusambaza umeme na kusimamia gridi ya Taifa kujengwa Dodoma*
Agizo la Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha kuwa minada yote nchini inakuwa na miundombinu itakayowawezesha Wachoma nyama, Mama Lishe na Baba Lishe kutumia nishati Safi ya Kupikia limeanza kutekelezwa ikiwa ni utekelezaji wa ajenda ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wote wanatumia Nishati iliyosafi ya kupikia.
Safari ya kuhakikisha minada yote nchini inatumia nishati safi ya kupikia, imeanzia katika Mnada wa Msalato jijini Dodoma ambapo leo tarehe 21 Agosti 2025, Dkt. Biteko amegawa majiko banifu kwa Mamalishe takriban 27 wanaohudumu katika mnada huo pamoja na majiko ya kuchomea nyama.
“Kama mnavyofahamu, Mhe. Rais alitoa maelekezo kuwa watanzania asilimia 80 ifikapo 2034 watumie nishati safi ya kupikia, maelekezo yake yanaendelea kutekelezwa, tulianza na taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 kuondoa matumizi ya kuni na mkaa ikiwemo magereza yote nchini, shule za Sekondari , vyuo na taasisi nyinginezo lakini moja ya maeneo yaliyobaki ni pamoja na minada ambayo inahudumia watu wengi.” Amesema Dkt.Biteko
Dkt. Biteko ameeleza kuwa kazi ya kufunga mifumo ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye minada ilianza na utafiti ili kupata hali halisi ya matumizi ya nishati hiyo ambapo katika utafiti huo, asilimia 89.5 ya wachoma nyama wote walisema hawana uelewa kuhusu nishati safi ya kupikia, pia utafiti huo umeonesha asilimia 26.3 ya wachoma nyama wamewahi kutumia nishati safi ya kupikia na asilimia iliyobaki haijawahi kutumia. Hii ikionesha kuwa bado kuna kazi ya kufanya kuelekea kwenye matumizi ya Nishati Safi ya kupikia.
Amesisitiza kuwa, hatua hizo zinazochukuliwa na Serikali katika Nishati Safi ya Kupikia, ni matunda ya Mhe. Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye amejipambanua kama kiongozi mwanamke anayejua machungu ya matumizi ya nishati isiyo safi na wakati wote anaelekeza kuwa yeye anachotaka kuona ni watu wengi hawatumii nishati isiyo safi ya kupikia.
Ameongeza kuwa, Tanzania ndiyo nchi nchi pekee barani Afrika ambayo imezindua Mkakati wa Taifa wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambao umekuwa ni mfano barani Afrika na nchi nyingine zinakuja kujifunza hivyo lazima iwe mfano na kinara kwa kuishi yale inayoyasema.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuweka miundombinu ambayo itafanya majiko ya nishati safi ya kupikia katika minada mkoani Dodoma kuwa katika sehemu ya kudumu na zoezi hilo lianze mara moja.
Aidha, ameliagiza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuweka kituo cha kudumu cha kuuza mkaa mbadala katika mnada wa Msalato ili wananchi wasikwame pale wanapohitaji nishati hiyo.
Vilevile ameitaka REA, kuhakikisha majiko makubwa ya kuchomea nyama ambayo yanatumia Nishati Safi ya Kupikia yanapatikana ili wananchi wanaochoma nyama na wanaofuata huduma wasipoate madhara ya afya kuanzia sasa kwenda mbele.
Dkt. Biteko ameipongeza REA na Watendaji wa Wizara ya Nishati kwa kupoeka agizo lake kwa haraka na kulifanyia kazi, pia amewaasa kuendelea na ubunifu utakaowawezesha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia na wasisahau kufanya tathmini ya matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika minada hiyo.
Pia, amewaasa Mama lishe na Baba lishe kuiunga mkono ajenda ya nishati safi ya kupikia na kuwa mabalozi wa nishati hiyo kwani watu wakiona faida zinazotokana na kutumia nishati safi ya kupikia kutoka kwao nao watavutika kuitumia.
Dkt. Biteko amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kubwa ya mfano katika sekta ya Nishati ambapo amesema Mkoa wa Dodoma muda si mrefu utakuwa ni kitovu cha usambazaji umeme katika mikoa mbalimbali ikiwemo Singida, Shinyanga, Tabora, Kigoma na Arusha na pia kitajengwa kituo kikubwa cha kusambaza umeme na kusimamia gridi ya Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema walaji katika mnada wa Msalato kwa wiki ni kati ya 2000 na 3000 hivyo kwa kutumia Nishati Safi ya Kupikia itawezesha kuokoa mazingira kwa kuondokana na kuni na mkaa ambao ulikuwa ukitumika kuhudumia idadi hiyo ya watu.
Aidha ameomba a kampeni hiyo ya Nishati Safi ya Kupikia ifike kwenye masoko mbalimbali ambayo ina mama lishe na baba lishe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amemshukuru Dkt. Biteko kwa maono yake ambayo yamewezesha Mnada wa Msalato kufikiwa na Nishati Safi ya Kupikia ikiwa ni mwanzo wa kusogeza huduma kwenye minada mingine.
Ameeleza kuwa kiwango cha matumizi ya nishati safi ya kupikia kimepanda kutoka asilimia 6.9 ya mwaka 2022 na hadi kufikia asilimia 20.3 na kusema kuwa kwa jinsi matumizi ya nishatil safi ya kupikia yanavyoongezeka Serikali itatimiza lengo lake ya kufikisha Nishati Safi ya Kupikia kwa watanzania wapatao asilimia 80 kama alivyoagiza Mhe.Rais.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amesema mnada wa Msalato una wachoma nyama kati ya 45 na 50 ambao watapatiwa majiko makubwa ya kuchomea nyama, pia kuna mama lishe 27 ambao tayari wote wamepatiwa majiko banifu.
Mwenyekiti wa Wachoma nyama katika Mnada wa Msalato, Mathias Raphael amesema baada ya kupata elimu ya nishati safi ya kupikia katika mnada huo ameanza kutumia jiko linalotumia mkaa mbadala ambao amesema kuwa unatumika kidogo huku ukichoma nyama nyingi, unakaa muda mrefu na hauna moshi.
Mwisho
AGIZO LA DKT.BITEKO LA MINADA YOTE NCHINI KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA LAANZA KUTEKELEZWA
Nishati📌 Wachoma nyama na Mama Lishe katika mnada wa Msalato Dodoma waanza kuonja matunda ya Nishati Safi ya Kupikia
📌 Dkt. Biteko asema ni matunda ya Rais, Dkt. Samia ambaye anayefahamu machungu ya kutumia Nishati isiyo safi ya Kupikia
📌 Atoa maagizo kwa Mkurugenzi Jiji la Dodoma kuweka miundombinu itakayohakikisha majiko ya Nishati Safi ya Kupikia ya Wachoma nyama yanakuwa salama
📌 Apongeza REA, Wizara ya Nishati kutekeleza agizo alilolitoa: STAMICO yatakiwa kuweka kituo cha kudumu cha mkaa mbadala Mnada wa Msalato
📌 Kituo kikubwa cha kusambaza umeme na kusimamia gridi ya Taifa kujengwa Dodoma
Agizo la Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko alilolitoa kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha kuwa minada yote nchini inakuwa na miundombinu itakayowawezesha Wachoma nyama, Mama Lishe na Baba Lishe kutumia nishati Safi ya Kupikia limeanza kufanyiwa kazi ikiwa ni utekelezaji wa ajenda ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wote wanatumia Nishati iliyosafi ya kupikia.
Safari hiyo ya kuhakikisha minada yote nchini inatumia nishati safi ya kupikia, imeanzia katika Mnada wa Msalato jijini Dodoma ambapo tarehe 21 Agosti 2025, Dkt. Biteko amegawa majiko banifu kwa Mamalishe takriban 27 wanaohudumu katika mnada huo pamoja na majiko ya kuchomea nyama.
“Kama mnavyofahamu, Mhe. Rais alitoa maelekezo kuwa watanzania asilimia 80 ifikapo 2034 watumie nishati safi ya kupikia, maelekezo yake yanaendelea kutekelezwa, tulianza na taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 kuondoa matumizi ya kuni na mkaa ikiwemo magereza yote nchini, shule za Sekondari , vyuo na taasisi nyinginezo lakini moja ya maeneo yaliyobaki ni pamoja na minada ambayo inahudumia watu wengi.” Amesema Dkt.Biteko
Dkt. Biteko ameeleza kuwa kazi ya kufunga mifumo ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye minada ilianza na utafiti ili kupata hali halisi ya matumizi ya nishati hiyo ambapo katika utafiti huo, asilimia 89.5 ya wachoma nyama wote walisema hawana uelewa wowote kuhusu nishati safi ya kupikia, pia utafiti huo umeonesha asilimia 26.3 ya wachoma nyama wamewahi kutumia nishati safi ya kupikia na asilimia iliyobaki haijawahi kutumia. Hii ikionesha kuwa bado kuna kazi ya kufanya kuelekea kwenye matumizi ya Nishati Safi ya kupikia.
Amesisitiza kuwa, hatua hizo zinazochukuliwa na Serikali katika Nishati Safi ya Kupikia, ni matunda ya Mhe. Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye amejipambanua kama kama kiongozi mwanamke anayejua machungu ya matumizi ya nishati isiyo safi na wakati wote anaelekeza kuwa yeye anachotaka kuona ni watu wengi hawatumii nishati isiyo safi ya kupikia.
Ameongeza kuwa, Tanzania ndiyo nchi pekee barani Afrika ambayo imezindua Mkakati wa Taifa wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambao umekuwa ni mfano barani Afrika na nchi nyingine zinakuja kujifunza hivyo lazima iwe mfano na kinara kwa kuishi yale inayoyasema.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuweka miundombinu ambayo itafanya majiko ya nishati safi ya kupikia katika minada mkoani Dodoma kuwa katika sehemu ya kudumu na zoezi hilo lianze mara moja.
Aidha, ameliagiza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuweka kituo cha kudumu cha kuuza mkaa mbadala katika mnada wa Msalato ili wananchi wasikwame pale wanapohitaji nishati hiyo.
Vilevile ameitaka REA, kuhakikisha majiko makubwa ya kuchomea nyama ambayo yanatumia Nishati Safi ya Kupikia yanapatikana ili wananchi wanaochoma nyama na wanaofuata huduma wasipoate madhara ya afya kuanzia sasa kwenda mbele.
Dkt. Biteko ameipongeza REA na Watendaji wa Wizara ya Nishati kwa kupoeka agizo lake kwa haraka na kulifanyia kazi, pia amewaasa kuendelea na ubunifu utakaowawezesha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia na wasisahau kufanya tathmini ya matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika minada hiyo.
Pia, amewaasa Mama lishe na Baba lishe kuiunga mkono ajenda ta nishati safi ya kupikia na kuwa mabalozi wa nishati hiyo kwani watu wakiona faida zinazotokana na kutumia nishati safi ya kupikia kutoka kwao nao watavutika kuitumia.
katika hafla hiyo, Dkt. Biteko amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kubwa ya mfano katika sekta ya Nishati ambapo amesema Mkoa wa Dodoma muda si mrefu utakuwa ni kitovu cha usambazaji umeme katika mikoa mbalimbali ikiwemo Singida, Shinyanga, Tabora, Kigoma na Arusha na pia kitajengwa kituo kikubwa cha kusambaza umeme na kusimamia gridi ya Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule kwa upande wake amesema walaji katika mnada wa Msalato kwa wiki ni kati ya 2000 na 3000 hivyo kwa kutumia Nishati Safi ya Kupikia itawezesha kuokoa mazingira kwa kuondokana na kuni na mkaa ambao ulikuwa ukitumika kuhudumia idadi hiyo ya watu.
Aidha ameomba a kampeni hiyo ya Nishati Safi ya Kupikia ifike kwenye masoko mbalimbali ambayo ina mama lishe na baba lishe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba yeye amemshukuru Dkt. Biteko kwa maono yake ambayo yamewezesha Mnada wa Msalato kufikiwa na Nishati Safi ya Kupikia ikiwa ni mwanzo wa kusogeza huduma kwenye minada mingine.
Ameeleza kuwa kiwango cha matumizi ya nishati safi ya kupikia kimepanda kutoka asilimia 6.9 ya mwaka 2022 na hadi kufikia asilimia 20.3 na kusema kuwa kwa jinsi matumizi ya nishatil safi ya kupikia yanavyoongezeka Serikali itatimiza lengo lake ya kufikisha Nishati Safi ya Kupikia kwa watanzania wapatao asilimia 80 kama alivyoagiza Mhe.Rais.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amesema amesema katika mnada wa Msalato kuna wachoma nyama kati ya 45 na 50 ambao watapatiwa majiko makubwa ya kuchomea nyama, pia kuna mama lishe 27 ambao tayari wote wamepatiwa majiko banifu.
Mwenyekiti wa Wachoma nyama katika Mnada wa Msalato, Mathias Raphael amesema baada ya kupata elimu ya nishati safi ya kupikia katika mnada huo ameanza kutumia jiko linalotumia mkaa mbadala ambao amesema kuwa unatumika kidogo huku ukichoma nyama nyingi, unakaa muda mrefu na hauna moshi.
Mwisho
JAPAN KUWAJENGEA UWEZO VIJANA WA TANZANIA KATIKA SEKTA YA UJENZI
habariTPA IMECHUKUA HATUA MBALIMBALI IKIWEMO UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU
habariMamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) imechukua hatua mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa Miundombinu, kusimika mifumo bora ya TEHAMA na kushirikisha Wadau wa Sekta Binafsi wakiwemo waendeshaji wa Bandari, ili kuongeza ufanisi katika kuhudumia Shehena za ndani na nje ya nchi kupitia katika bandari za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mbossa wakati akifungua kikao cha Wadau wa Usafirishaji wa Shehena kupitia Ushoroba wa kati, Agosti 21, 2025 Kilichofanyika Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, Naibu Mkurugenzi Mkuu Mha. Dkt. Baraka Mdima amesema, hatua hizi madhubuti zilichukuliwa na zinaendelea kuchukuliwa na TPA kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuboresha tija Bandarini, ziende sambamba na kujenga utamaduni wa Uadilifu na Uwajibikaji kwa Wafanyakazi wake, wateja na wadau ili kurahisisha ufanyaji biashara kupitia ushoroba wa kati.
Mha. Dkt. Mdima amesisitiza kuwa ni vyema, Wadau wanaoshiriki kikao hicho, wakajadiliana changamoto zinazokabili Sekta ya usafirishaji na kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza ufanisi, kupunguza gharama na kurahisisha biashara kupitia ushoroba wa kati.
Aidha, amewahakikishia Wadau wa Usafirishaji kuwa TPA inaendelea kuwa na dhamira ya dhati ya kuendelea kushirikiana na Wadau wake ili kuhakikisha kuwa Ushoroba wa Kati unakuwa wa kisasa, wenye ufanisi, na wenye mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania na nchi zote zinazohudumiwa na ushoroba huo.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Bw. Martin Masunga, amesema maoni yote yaliyotolewa na Wadau hao, yamepokelewa na yatafanyiwa kazi na Serikali ili kurahisisha ufanyaji wa Biashara na kuondoa ucheleweshaji kupitia Ushoroba wa kati.
Kikao hiki cha Wadau wa Usafirishaji kimeandaliwa na TPA chini ya Usimamizi wa Wizara ya Uchukuzi na kimehudhuriwa na Wadau mbalimbali wakiwemo Chama cha Mawakala wa Meli ( TASAA), Chama cha Mawakala wa Forodha ( TACAS) Baraza la Wasafirishaji ( TSC) Wamiliki wa Bandari Kavu ( CIDAT) Chama cha Wasafirishaji Tanzania ( TAT) na Chama cha Wamiliki wa Malori madogo na ya kati ( TAMSTOA).