SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA UONGOZI NA USIMAMIZI WA ELIMU KUPITIA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA SHULE

July 09, 2025 Add Comment
NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeendelea kuimarisha uongozi na usimamizi wa elimu nchini kwa kutoa mafunzo ya uongozi, usimamizi na utawala bora kwa walimu wakuu wa shule za awali na msingi pamoja na maafisa elimu kata kutoka Tanzania Bara.

SEKTA YA HABARI NI NYENZO MUHIMU KULINDA NA KUDUMISHA AMANI KIPINDI CHA UCHAGUZI - DKT.BITEKO

July 09, 2025 Add Comment




📌 *Avitaka vyombo vya habari kuheshimu tofauti za maoni*


📌 *Aviasa vyombo vya habari kuwa kioo, vijiepushe na uzushi,upendeleo kuelekea Uchaguzi Mkuu*


📌 *Sekta ya habari yaahidi kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa weledi*


📌 *Serikali ya Dkt. Samia inatoa kipaumbele kwa sekta ya habari*


📌 *TAI – Habari yasajili waandishi wa habari zaidi ya 2900*


*Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati*

 

Tasnia ya habari nchini inatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi kabla na baada ya uhuru ambapo uwepo wa baadhi ya vyombo vya habari vya awali kama vile gazeti la Sauti ya TANU na redio Sauti ya Dar es Salaam vilisaidia kutoa mchango mkubwa katika kujenga umoja, utaifa na kuhamasisha ushiriki wa harakati za kudai uhuru.


Akifungua Mkutano wa Wadau Kujadili Mchango wa Sekta ya Habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2025, jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewaasa waandishi wa habari nchini kuwa walinzi wa ukweli, wajenzi wa amani na wachochezi wa uwajibikaji wa kisiasa. 

Amevitaka vyombo vya habari kuwa kioo cha jamii na kujiepusha na uzushi, chuki au upendeleo na badala yake kuhimiza maelewano, uvumilivu wa kisiasa, na utamaduni wa kuheshimu tofauti za maoni.


 “ Ni wajibu wa Serikali kuhakikisha waandishi wa habari katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi wanabaki salama pamoja na vitendea kazi vyao. Aidha, Serikali, tutaendelea kulisimamia hili kwa nguvu zetu zote. Tutahakikisha kuwa, mnakuwa na mazingira salama, huru na rafiki wakati wote wa majukumu yenu, amesema Dkt. Biteko.

Ameendelea kusema katika kuelekea Uchaguzi Mkuu 20205 katika jamii kutakuwa na watu wenye mitazamo todauti kulingana na vipaumbele vyao hata hivyo vyombo vya habari vina fursa ya kutoa uelekeo kwa taifa.


“Uchaguzi ni kipindi cha muda mfupi, tumuombe Mungu hata  baada ya Uchaguzi tubaki kuwa Taifa moja lenye ustahimilivu na kila mmoja akitoka kwake aende kutafuta mkate arudi nyumbani kwa familia yake kukiwa na amani, sisi kupitia mkutano huu tuungane kuhakikisha Taifa letu linabaki salama. Sekta ya habari ni nyenzo muhimu katika kulinda na kudumisha amani katika kipindi chote cha uchaguzi,” amesisitiza Dkt. Biteko.

Ameongeza kuwa kutokana na mazingira wezeshi kwa sekta hiyo ya habari Tanzania kwa sasa ina idadi kubwa ya vyombo vya habari ikilinganishwa na miaka iliyopita, ambapo kuna jumla ya magazeti 375, vituo vya redio 247, vyombo vya habari vya mtandaoni 355, blogs 72 na vituo vya televisheni 68, hivyo amevitaka vyombo hivyo kukumbushana wajibu wao na kuzingatia miiko na maadili ya taaluma yao na kuilinda tasnia yao kwa wivu mkubwa.


Kutokana na utafiti wa Taasisi ya REPOA (Research on Poverty Alleviation) mwaka 2022 unaonesha kuwa vyombo vya habari ndiyo chanzo kikuu cha taarifa za kisiasa kwa wananchi ambapo zaidi ya asilimia 76 ya wananchi hupata taarifa za kisiasa kupitia vipindi vya redio na televisheni, Dkt. Biteko ameviasa vyombo vya habari kutoa majukwaa ya mijadala ya kisera na kisiasa ambayo huwasaidia wapiga kura kufanya maamuzi sahihi kwa kusikiliza sera na ajenda za wagombea ikiwa ni pamoja na  kuhamasisha ushiriki wa makundi yote katika jamii, yakiwemo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Aidha, amesema kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili  kuhakikisha Sekta ya Habari na Utangazaji nchini inakua na kutoa huduma bora kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ambapo Aprili 6, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo ya kuvifungulia vyombo vya habari vilivyokuwa vimefungiwa. Na pia kuvirejeshea leseni vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vimemaliza adhabu zake ili viendelee na majukumu ya kuhabarisha jamii. 

Amesema ni hatua ambayo  inadhihirisha kuwa Serikali ya Dkt. Samia inaendeleza dhana ya kuheshimu na kuipa kipaumbele sekta ya habari nchini ili Watanzania wapate habari sahihi. Serikali itaendelea kuthamini na kuenzi mchango wa sekta ya habari, aidha, katika kutekeleza kwa vitendo falsafa ya "4Rs" yaani Maridhiano (Reconciliation), Ustahimilivu (Resilience), Mageuzi (Reforms), na Ujenzi Mpya wa Taifa(Rebuilding) bado sekta ya habari inahitajika  na mchango wake ni wa muhimu.

Hatahivyo, Dkt. Biteko amesema kutokana na matumizi makubwa ya teknolojia na mitandao ya kijamii sekta ya habari ina jukumu kubwa la kupambana na taarifa potofu na kuhakikisha kuwa jamii inapata taarifa sahihi kwa njia ya kidigitali kwa kutumia lugha ya staha, kuepuka uchochezi na kuripoti kwa usawa, vyombo vya habari huchangia katika kudumisha utulivu wa kitaifa.


Fauka ya hayo, ameipongeza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kazi wanayoifanya kuandaa uchaguzi wa mwaka 2025 na kusema kuwa ni Rais Samia angependa kuona uchaguzi unafanyika kwa haki na amani.


“ Ni matarajio yetu kuwa Tume itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari kwa karibu, kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu taratibu zote za uchaguzi. Ushirikiano huu ni nguzo muhimu ya kuimarisha imani ya wananchi kwa mchakato wa uchaguzi.” amemalizia Dkt. Biteko.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa kupitia mkutano huo  wa wadau wa sekta ya habari wanalenga kuweka msingi madhubuti wa ushirikiano kati ya Serikali, vyombo vya habari, asasi za kiraia, taasisi za usalama na taasisi huru kama Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, ili kulinda amani, kuhimiza usawa wa fursa kwa vyama vyote vya siasa, na kuruhusu wananchi kupata taarifa za msingi zitakazowawezesha kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kuchagua viongozi wao.


“Tunafahamu kuwa uchaguzi ni tukio nyeti. Ni kipindi ambacho jamii inakuwa na matarajio makubwa ya kupata taarifa zilizo sahihi, kwa wakati na zisizo na upendeleo. Ndiyo maana mkutano huu pia umehusisha vyombo vya ulinzi na usalama, ili kwa pamoja tuhakikishe kuwa waandishi wa habari wanafanya kazi katika mazingira salama, bila vitisho wala bugudha. Ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi na vyombo vya habari ni jambo la msingi na tunalipa kipaumbele katika mjadala wetu wa leo,” amesema Prof. Kabudi.



Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Albert Msando akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Albert Chalamila amesema wataendelea kushirikiana na vyombo vya habari ili kuhakikisha wanapata taarifa sahihi kutoka ndani ya Mkoa huo na Wilaya zake ili kuhabarisha wananchi.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wameona umuhimu wa kuungana katika mkutano huo kwa lengo la kujadiliana ili kuhakikisha sekta ya habari  inashiriki Uchaguzi Mkuu kwa mwaka 2025 kwa weledi.


“Mwaka huu tunashiriki Uchaguzi Mkuu tukiwa tumesimamia weledi, tumeanza kuendesha taaluma yetu kitaalamu na sasa tuna mfumo wa kidigiti wa kusajili na kutoa ithibati kwa waandishi wa habari,” amesema Msigwa.


Pamoja na ufunguzi wa mkutano huo, Dkt. Biteko amezindua rasmi Mfumo wa Kidigiti wa TAI – Habari wa kusajili na kutoa ithibati kwa waandishi wa habari ambao unasimamiwa na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari ambapo hadi  sasa Bodi hiyo imesajili waandishi wa habari zaidi ya 2900 kupitia mfumo huo  ambao unachakata taarifa zote muhimu za mwandishi wa habari na kisha kumpatia mwandishi wa habari kitambulisho cha kidigiti  yaani Digital Press Card.


MWISHO.

RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA

July 09, 2025 Add Comment


*📌Apatiwa elimu juu ya utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa  Nishati safi ya kupikia


*📌 Wizara ya Nishati kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa tasisi zake kutekeleza majukumu yake kikamilifu


Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi leo 7 Julai, 2025 ametembelea banda la Wizara ya Nishati  kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba jijini Dar es salaam


Akiwa kwenye banda la Wizara ya Nishati Mhe Mwinyi alipokelewa na Mkuu wa kitengo cha  Mawasiliano Serikalini Bi Neema Chalila Mbuja, ambapo alimweleza juu ya hatua za utekelezaji zilizofikiwa kwenye utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa nishati safi ya kupikia na kuongeza kuwa ajenda hiyo ni utekelezaji wa azimio la Mhe Rais Samia kama kinara wa nishati safi ya kupikia.



Amesema Wizara ya Nishati kupitia taasisi zilizopo chini ya Wizara zimekuwa zikitekeleza kwa vitendo ajenda hiyo kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambae ni kinara wa nishati safi ya kupikia kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.

Wizara ya nishati tayari imezindua mikakati miwili ya nishati safi ya kupikia na ule wa mawasiliano ili kuwezesha utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo

RAIS SAMIA ATOA BILIONI 16.696 KWA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU MKOANI TANGA KUPITIA MRADI WA SEQUIP.

July 09, 2025 Add Comment
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025, imetoa jumla ya shilingi bilioni 16.696 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) mkoani Tanga.

Tanzania na Marekani Zaahidi Kuimarisha Ushirikiano wa Kisekta

July 09, 2025 Add Comment
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Samwel Shelukindo, alikutana na kufanya mazungumzo na Bw. Andrew Lentz, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini.