MRADI WA BOMBA LA GESI NTORYA–MADIMBA KUGHARIMU SHILINGI BILIONI 120

July 03, 2025 Add Comment
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya China ya CPP na CPTDC kwaajili ya ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Ntorya hadi Madimba mkoani Mtwara kwa kipindi cha miezi 12.

TBS YAWASILISHA UTEKELEZAJI WA SERA YA KURUDISHA KWA JAMII

July 03, 2025 Add Comment
EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limepokea tuzo kutoka Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope, kutokana na desturi waliyojiwekea kutoa mchango wao kwa watu mbalimbali hususani jamii ya watu wenye ulemavu.

SADC YAITAJA TANZANIA KINARA UTEKEKEZAJI AJENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

July 03, 2025 Add Comment


📌 *Rais Samia aendelea kupongezwa kwa kuwa kinara wa Nishati safi ya Kupikia Afrika*


📌 *Mhe. Kapinga ataka mikakati, ubunifu utekelezaji nishati safi ya Kupikia Jumuiya ya  SADC*


📌 *Asisitiza uelimishaji matumizi ya nishati safi ya kupikia kupewa nguvu*


📌 *SADC yapongeza Tanzania mkutano wa Misheni 300*


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametajwa kuwa kinara namba moja wa uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia Afrika na Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya  Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 

Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 3, 2025 na Viongozi mbalimbali na Wataalam kutoka Nchi nane za (SADC) ambao wamekutana jijini Harare nchini Zimbabwe katika Mkutano  unaolenga kuimarisha na kujadili masuala mbalimbali yatakayowezesha mtangamano wa Kikanda katika sekta za nishati na maji.

Akizungumza Katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema kuwa Serikali imeendelea kuwezesha, kuhamasisha na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia (2024 – 2034).


Kuhusu utekelezaji wa nishati safi ya kupikia kwa jumuiya hiyo, Mhe. Kapinga ameitaka SADC kuweka dhamira na mikakati ya utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia ili kuwafikia watu wengi zaidi SADC. 

Vilevile, amesisitiza SADC kuwa wabunifu katika matumizi ya nyenzo mbalimbali zitakazowezesha na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia huku akitolea mfano matumizi ya mkaa mbadala kama vile wa rafiki briquettes katika matumizi ya kupikia kama njia ya kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo kwa wananchi. 


Pia, Mhe. Kapinga ameitaka SADC kuweka nguvu zaidi katika uelimishaji na uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuwataka wanachama wa SADC kuweka mkakati utakaowezesha unarahisisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kuwa muhimu kwa uchumi endelevu katika maeneo yao.



Katika hatua nyingine, Mhe. Kapinga amepokea pongezi zilizotolewa na Wanachama wa SADC kwa Tanzania kwa  kuandaa, kuwa mwenyeji na kufanikisha mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Nishati wa Afrika (Misheni 300 - M300) kwa ufanisi mkubwa uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Naye, Waziri wa Nishati wa Malawi, Mhe. Ibrahim Matola amempongeza Rais Samia kwa uthubutu wake wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Watanzania. Mhe. Matola ameitaka SADC kuitumia Tanzania kama balozi wa matumizi ya nishati safi ya kupikia katika jumuiya hiyo.


Mkutano huo umehudhuliwa na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Suzan Kaganda, Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati akiwemo Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme, Mha. Styden Rwebangila, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy, Mkurugenzi wa  Mipango na Uwekezaji (TPDC), Derick Moshi, Mkurugenzi wa Mifumo ya Udhibiti Umeme (TANESCO) , Mha. Deogratius Mariwa, Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi (EWURA), Msafiri Mtepa na  Wataalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

NAIBU WAZIRI UMMY AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUGHARAMIA MAZISHI WALIOFARIKI SAME

July 03, 2025 Add Comment


Na Mwandishi Wetu - KILIMANJARO


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa upendo  kwa kugharamia mazishi ya  miili  42 ya watu waliofariki dunia kufuatia  ajali iliyotokea  Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Mhe. Nderiananga ametoa shukrani hizo  tarehe 03 Julai, 2025 wakati aliposhiriki tukio la kuaga miili 35 katika viwanja vya Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) akisema miili Saba ilichukuliwa na ndugu zao na miili miwili bado vipimo vya DNA vinafanyiwa kazi ili kutambulika.

Tukio hilo lilioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Nurdin Babu ambapo Mhe. Nderiananga alimpongeza kwa kujitoa kwa kiasi kikubwa tangu ilipotokea ajali hiyo akishirikiana na watendaji wake wote.

Amesema Serikali  kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa iliyopo Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kilimanjaro kwa juhudi kubwa zilizofanyika kuokoa manusura wa ajali hiyo pamoja na miili ya walioungua kwa moto mara baada ya ajali kutokea.

Vilevile ameipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuchukua  sampuli za miili hiyo (DNA)  kuhakikisha ndugu wanatambua miili ya wapendwa wao.

Hata hivyo  Mhe. Nderiananga ameendelea kutoa pole kwa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huo mzito kwa Taifa  huku akiwaomba kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu hadi watakapokamilisha kuwahifadhi wapendwa wao. 



Aidha, ajali hiyo iliyotokea Juni 28 2025 katika Kitongoji Mahuu, Kata ya Same, takribani kilomita nne kutoka Same mjini, ililihusisha basi kubwa la abiria, Mali ya Kampuni ya Chanel One, lenye namba za usajili T 179 CWL na basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster, lenye namba T 199 EFX linalomilikiwa na Kampuni ya Mwami Trans.




Coaster hiyo, ilikuwa ikitokea Same kuelekea Manispaa ya Moshi, wakati basi la Chanel One lilikuwa likitokea Arusha kuelekea Tanga.

MIRADI YA NISHATI SAFI IACHE ALAMA KWA WANANCHI,ASEMA KAMISHNA LUOGA

July 03, 2025 Add Comment

 



*📌Afungua Mkutano wa Sita wa Kamati ya Uwekezaji miradi ya nishati safi ya kupikia*


*📌 Aishukuru EU na UNCDF kutekeleza ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo*


*📌 Asema ushirikishwaji wa srkta binafsi ni chachu ya kuleta maendeleo miradi ya nishati safi*


*📌UNCDF kuangalia uwezekano wa kituo cha elimu kwa vitendo kuhusu nishati safi ya kupikia*


Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Innocent Luoga amesema utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia inapaswa kuweka alama kwa wananchi  ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa


Kamishna luoga ameyasema hayo leo julai 3 ,2025 wakati akifungua mkutano wa sita wa wa kamati ya uwekezaji miradi ya nishati safi ya kupikia unaotekelezwa kwa pamoja kati ya Serikali, Umoja wa Ulaya na Shirika la umoja wa mataifa la maendeleo na mitaji ili kusaidia utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia

‘’Serikali kupitia Wizara ya Nishati na wadau wa nishati safi ya kupikia imefanya kazi kubwa kuhakikisha malengo yanatimia ikiwemo utekelezaji na ushirikishwaji wa sekta binafsi kwenye miradi ya nishati safi ya kupikia ili kubadili fikra na kutimiza azma ya Serikali ya kufikia asilimia 80 ya watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034’’ Amesema Mha. Luoga.

Amesema chini ya uwepo wa kamati hii ya uwekezaji kumekuwa na mafanikio mbalimbali ikiwemo uwekezaji kwenye teknolojia mbalimbali za miradi ya nishati safi ya kupikia ili kuwezesha wanachi kutumia teknolojia mbalimbali ikiwemo gesi,umeme, na mabaki ya kinyesi cha wanyama na kuachana na matumizi ya nishati isiyo safi

 


Kwa upande wake, Mratibu wa mradi kutoka UNCDF Bw. Emmanuel Muro amesema  UNCDF kupitia Cook fund chini ya ufadhili wa Umoja wa ulaya inaandaa mpango wa kuanzisha kituo maalum cha matokeo kwa vitendo ili kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa nishati mbalimbali zinazotumika kwa ajili ya matumizi ya kupikia ili wananchi wawe na uwelewa mpana juu ya nishati mbalimbali za kupikia

Mkutano huo wa sita wa wadau umepitisha wafanyabiashara wadogo 17 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya teknolojia ya nishati  safi ya kupikia kwa ajili ya ufadhili ili isaidie urahisishaji kwa watumiaji wa teknolojia ya nishati safi ya kupikia.