KIKAO KAZI CHA KUPITIA NA KUTHIBITISHA RASIMU YA MPANGO MKAKATI WA TAIFA WA KUZUIA KUZAMA MAJI CHAFANYIKA DODOMA

June 11, 2025 Add Comment


Na Mwandishi wetu Dodoma.

Kikao kazi cha kupitia na kuthibitisha Rasimu ya Mpango Mkakati wa Taifa wa Kuzuia Kuzama Maji chafanyika tarehe 11 Juni, 2025 katika ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na uokoa Jijini Dodoma.

Kikao hicho kimewashirikisha Wawakilishi kutoka Wizara, Taasisi na Idara za Serikali, Mashirika ya Kimataifa, Asasi zisizo za Kiserikali, Mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza na Mara.


Akifungua kikao hicho, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Kanali Selestine Masalamado amesema Nchi yetu imeendelea kukumbwa na matukio mbalimbali ya majanga ya asili na yanayosababishwa na shughuli za kibinadamu, ambayo yamekuwa na madhara makubwa kwa maisha ya wananchi hasa waishio pembezoni mwa fukwe wakiwemo Wazee, Vijana na Watoto, hivyo kuathiri maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Hata hivyo Kanali Masalamado amesema, Kutokana na majanga hayo, Serikali ilianza Mchakato wa kuandaa mkakati wa Taifa wa Kuzuia Kuzama Maji mwaka 2024, kwa lengo la kuanzisha mfumo madhubuti na jumuishi wa kupunguza matukio ya vifo vinavyotokana na kuzama maji. 


Ameongeza kwa kusema, Mkakati huu umeandaliwa kwa njia shirikishi, ukihusisha wadau kutoka sekta mbalimbali, ili kuhakikisha hatua zinazopendekezwa zinajengwa juu ya ushahidi wa kisayansi, uzoefu wa jamii, na muktadha halisi wa Tanzania.

Ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa washiriki wote kuchangia mawazo yao kwa weledi na uzalendo katika kupitia na kuboresha Rasimu ya Mkakati, ili ifikie viwango vinavyostahili kabla ya kuidhinishwa rasmi na kuanza kutekelezwa.

Mwisho 


WAONGOZA WATALII WATOA KONGOLE KWA NCAA MABORESHO YA BARABARA KUTEKEKEA MSIMU WA UTALII

June 11, 2025 Add Comment



Na Mwandishi wa NCAA, Ngorongoro


Waongoza utalii kutoka kampuni mbalimbali zinazojihusisha na shughuli za utalii nchini wameipongeza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa juhudi wanazofanya  kuboresha miundombinu ya barabara katika Eneo la  Hifadhi ya Ngorongoro. 


Wadau hao wameelezeq hatua hiyo kuwa ni suluhisho la muda mrefu kwa changamoto zilizokuwa zikiwakabili, hasa wakati wa msimu wa kilele cha utalii (high season)


Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika geti la kuingia hifadhi ya Ngorongoro Juni 11, 2025, baadhi waongoza utalii hao wameeleza kuwa maboresho hayo yameleta mabadiliko makubwa katika usafiri, kupunguza muda wa safari, kuongeza usalama wa wageni, na kuboresha hali ya utalii katika hifadhi hiyo maarufu duniani.

“Tunatoa pongezi kwa NCAA kwa kazi kubwa waliyoifanya kuboresha barabara,  kwa sasa imekuwa rahisi zaidi kuwafikisha wageni kwa haraka na salama kwenye maeneo ya vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro 

” alisema Mohammed Tenga kutoka kumpuni ya Zara Tours. 

Kwa upande wake Walter Temba kutoka 

kampuni ya utalii ya Serengeti Smiles alieleza kuwa maboresho ya miundombinu ya barabara yanayoendelea yamekuja kwa wakati muafaka, ikizingatiwa kuwa sekta ya utalii nchini inaendelea kukua kwa kasi huku idadi ya wageni kutoka ndani na nje ya nchi ikiendelea kuongezeka kila mwaka.

“Kwa muda mrefu tumekuwa tukikumbana na changamoto kubwa hasa wakati wa mvua magari yanakwama na wageni kuharibika hata kabla ya kufika kwenye vivutio. Lakini sasa hali ni tofauti kabisa, barabara zimekarabatiwa kwa kiwango kizuri na zinaweza kupitika hata kipindi cha mvua ombi letu ni kuwa jitihada hizi ziwe endelevu,” alisema Temba.


Kwa Mujibu wa NCAA, maboresho ya barabara ni sehemu ya maandalizi ya taasisi hiyo kukabiliana na ongezeko kubwa la watalii ambalo limeanza mwezi juni ambalo linatarajiwa kuongezeka   hadi mwezi Oktoba kila mwaka.

 Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro hupokea maelfu ya wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani wanaokuja kutembelea vivutio vya utalii ambapo takwimu zinaonesha kuwa kati ya Mwezi Julai 2024 hadi Mei, 2025 jumla ya watalii 972,896 wametembelea hifadhi kwa shughuli za utalii.

WAKUU WA VITENGO REA,TARURA,RUWASA WAKUTANA KUJENGEANA UWEZO

June 11, 2025 Add Comment

 Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Bi. Martha Chassama amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasilino wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Bi. Catherine Sungura na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Masoko wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Bw. Athumani Shariff katika kikao kifupi kilichofanyika jijini Dodoma.   Kikao hicho kifupi kililenga kujengeana uwezo wa taasisi hizo hususan katika maeneo ya vijijini ili kuongeza chachu katika maeneo hayo.







VIJANA ZAIDI YA 350 KATIKA JIJI LA TANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA INCLU-CITIES PROJECT

June 11, 2025 Add Comment





Na Oscar Assenga, TANGA

ZAIDI ya Vijana 350 Jijini Tanga wanatarajiwa kunufaika na mradi wa Inclu-Cities Project uliopo chini ya Programu ya SASA kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ubelgiji (ENABEL) kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya .

Hayo yalisemwa leo wakati wa uzinduzi wa utambulisho wa mradi huo uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian uliofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho.
Akizungumza katika uzinduzi huo wakati akitoa taarifa yake wakati wa utambulisho wa mradi huo ,Mkuu wa Chuo cha Veta Tanga Gidioni Lairumbe alisema wakiwemo wanawake asilimia 50 katika Jiji la Tanga bila kusahau uchumi wa bluu ambapo program hiyo ni kuwaandaa na kuwajengea uwezo wa kujiajiri au kuajiwa vijana 150 asilimia 50 wasio na ujuzi kabisa katika fani mbalimbali.

Alizitaja fani hizo ni usindikaji na uandaaji wa chakula,Umeme wa Sola,Uchomeleaji na uungaji wa vyumba pamoja na utengenezaji wa mkaa mbadala ikiwemo mpango wa kuwapa ujuzi vijana walio sokoni ambao utawagusa vijana 150 ikilenga asilimia 50 ya wanawake katika fani.

Mkuu huyo wa chuo cha Veta alizitaja fani hizo ni Usindikaji na uandaaji wa chakula,uvuvi,Umeme wa sokla na uchomeleaji na uungaji wa vyuma sambamba na program ya utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo usio rasmi ambao utawagusa vijana 150 ukilenga wanawake kwa asilimia 50 katika fani za usindikaji na uandaaji wa chakula,uchomeleaji na uungaji wa vyuma,matengenezo ya pikipiki za umeme na matengenezo ya siku za mkononi.

Alisema kupitia mradi wa utekelezaji wa mradi huo wa Inclu –Cities uliopo chini ya Programu ya SASA kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ubelgiji (ENABEL) kwa ufadhili wa umoja wa ulaya pia kitaanzishwa kitengo cha utoaji wa ushauri wa masuala mbalimbali yahusuyo ujuzi na huduma mbalimbali kwa wanafunzi ,Ukarabati wa jengo la mgahawa pamoja na jiko kama eneo la kujifunzia wanafunzi wa mapishi na kupata vifaa mbalimbali vya kujifunzia

“Lengo kuu la mradi huu ni kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi kwa lengo la kuzalisha wahitimu wanaohitajika katika soko la ajira na kuifanya VETA Tanga kuwa kituo cha Umahiri wa Utoaji wa Mafunzo ya Ufundi Stadi katika Sekta husika waweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kukamilika mafunzo hayo “Alisema Mkuu huyo wa chuo cha VETA Tanga.

Alisema kwamba wanaimani kwamba elimu ya vitendo na ushirikiano kati ya waajiri na wadau mbalimbali wa maendeleo itasaidia kuelekea kupunguza ukosefu wa ajira na kuongeza kipato kwa wahitimu na kuwategemea baada ya mafunzo haya zaidi ya asilimia 75 ya wahitimu watakaopata ujuzi watakuwa katika nafasi nzuri ya kuingia kwenye soko kwa kujiamini.

Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian alisema kwamba wanaendelea kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa mambo makubwa anayoyafanya yanayopelekea kuungwa mkono na nchi mbalimbali wakiwemo umoja wa ulaya na wamefurahi mradi huo ambao una jumla ya Uero milioni 75 ambazo ni sawa na Bilioni 190 ni jambo kubwa ambalo litasaidia katika mipango ya program mbalimbali

“Lakini niwapongeze Veta kama sehemu ya mradi mliwasiliana na Umoja na Ulaya walipokuja kuwaona wakawa tayari kutekeleza mradi na Jiji na Veta Makao Makuu ambao walikubali mpango huo kuweza kufanyika kwenye maeneo yao na Tanga kwa moja wapo na sisi tunashukuru na kuwapongeza kwa hatua hii nzuri na muhimu kwa maendeleo na huo ndio umuhimu wa uwepo wa chuo hiki”Alisema

Aidha alitaka mchakato wa kuwapata walengwa katika mradi huo wapate vijana wanaotoka kwenye familia ambazo hazina uwezo na ambao watakaotoka wataweze kuwasaidia familia wachague mchanganyiko na wasaidiane na madiwani kuwaibuua watu ambao watakwenda kuwaheshimisha fursa hiyo na kupata kitu baadae cha kubadilisha maisha yao.

Alisema kwamba katika miaka 50 ya chuo cha Veta ndio ambao ambacho kitawakomboa watanzania hasa vijana katikati kulikuwa na wimbi la vyuo vyote za ufundi kuwa kuwa vyuo vikuu lakini misingi ya Baba wa Taifa na dhana ya ujamaa wa kujitegemea ilikuwa ni kupitia mifumo ya vyuo vya ufundi lakini na shule za amali ambazo sasa serikali imerudisha zitawakomboa vijana

Aliongeza kwamba vitawakomboa kwa sababu watatoka wakiwa na maarifa ya jinsi ya kumudu mazingira yao na kinachofanyika ni kuzuri kitasaidia vijana wao huku akiwataka chuo hicho kuendelea kuwapika vijana vizuri waandalieni stadi mbalimbali ikiwemo bustani za maua za kisasa.


Naye kwa upande wake Mshauri Mtaalamu wa Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ubelgiji (ENABEL) Thomas Aikaruwa Aliwapongeza Veta Tanga kwa kuamua kuanza safari ya maboresho kwenye chuo chao na kuwa kituo cha umahiri kwenye maeneo walioyaainisha.

Alisema kwamba Umoja wa Ulata kupitia Mpango wa Green City chini ya Mpango wa SASA watafanya kazi na Serikali ili kuchangia kwenye mikoa ya Tanga,Mwanza na Pemba lengo kusaidia kuboresha maisha ya watanzania wa kawafikia kwenye miji hiyo mitatu kwa kuboresha miundombinu inayozingatia mabadiliko ya tabia ya nchi.

Alisema pia katika kuboresha hudumu za kijamii kwa wananchi wanaopatikana kwenye mikoa hiyo kwa kuongeza ukuaji uchumi wa mwananchi wa kawaida katika mikoa hiyo katika ukuaji wa uchumi wa mwananchi huyo ambapo mradi huo chini ya shirika la Ujerumani Enable linafanya kazi kwa ukaribu na wadau muhimu katika sekta hiyo ya kukuza ujuzi hasa wadau wanaofanya shughuli zao kwenye maeneo hayo wanafanya kazi.

Aidha aliwataja wadau hao kuwa ni Veta na Veta ya Pemba na Sido Tanga na Mwanza ikiwemo sekta binafsi ambazo zinapatikana kwenye mikoa hiyo mitatu chini ya uangalizi wa Halmashauri zinazopatikana kwenye mikoa hiyo ya Tanga,Ilemela ,Nyamagana-Mwana na Chakechake-Pemba na nyengine ambazo zinavutiwa kuingia kwenye mpango huo.

Hata hivyo alisema kwamba ujuzi ni dhana muhimu katika kipindi waliochopo hasa ukizingatia mabadiliko ya mitaala ya elimu na wanategemea kutoka na ujuzi hasa mabadiliko ya kisasa na kuibua na kutengeneza ajira ili kuimarisha zilizopo ili viweze kuwa na tija na maeneo yanayotazamiwa kufikiwa.

“Maeneo tunayotazamiwa kufikiwa ni utumiaji huduma za kibiashara na kifedha na uwekezaji kuwe na ubora na mafunzo ya ujuzi yanayotolewa na taasisi zilizotajwa yanayozingata mahitaji ya sasa na ujasiriamali na bajeti ya shughuli zao ni Bilioni 190 ambazo ni kama euro milioni 75 na muda wa mradi huo ulianza mwaka 2022 na utakwenda mpaka mwaka 2027”Alisema

Mwisho.