TANAPA YATUNUKIWA TUZO YA JUU ULAYA KWA MARA YA MFULULIZO

June 01, 2025 Add Comment


Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetunukiwa tuzo ya hadhi ya juu kwa mara ya sita mfululizo iitwayo European Quality Choice Diamond ya mwaka 2025 katika hafla iliyofanyika usiku wa tarehe 29 Mei, 2025, jijini Stockholm, nchini Uswidi, kwa kutambua utendaji wake mahiri katika utalii na uhifadhi.


Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Mshauri Mtendaji Mkuu wa taasisi ya European Society for Quality Research (ESQR), Bw. Michael Harris,  kwa Balozi wa Tanzania nchini Uswidi, Mhe. Mobhare Matinyi, ambaye aliambatana na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Bw. Mussa Nassoro Kuji; Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Rodwell Ole Meing'ataki; Afisa Mkuu wa Uhifadhi, Eunice Msangi; Afisa Uhifadhi Andrew Mbai; na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania, Malik Hassan.

TANAPA ilikuwa kampuni pekee ya utalii na uhifadhi kati ya 49 kutoka nchi 42 duniani zikiwemo zingine sita za Afrika iliyotunukiwa tuzo hiyo. TANAPA ni moja ya taasisi kadhaa nchini zenye usajili wa ISO 9001:2015 ambacho ndicho kigezo cha kupimwa utendaji na ESQR kila mwaka.

GCLA KANDA YA KATI YATOA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA MAJANGA YA KEMIKALI KWA WAKAZI WA RUAHA MBUYUNI

May 31, 2025 Add Comment
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilolo, Eston Kyando (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa makundi mbalimbali ya viongozi wa Kata ya Ruaha Mbuyuni juu ya namna ya kukabiliana na majanga ya kemikali ikiwemo ajali za magari yanayosafirisha kemikali. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa shule ya msingi Mbuyuni A, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, Mei 30, 2025. Kulia ni Meneja wa Usajili wa Kemikali na Maabara za Kemia, Musa Kuzumila.

REA YAHAMASISHA WANANCHI KUTUMIA MKAA MBADALA

May 30, 2025 Add Comment
-Yasisitiza ni salama, gharama nafuu na ni rafiki wa mazingira

MAWAZIRI WA NISHATI JUMUIYA YA SADC KUKUTANA NCHINI ZIMBABWE

May 30, 2025 Add Comment




📌.*Masuala ya Umeme, Gesi, Nishati Safi kujadiliwa*


Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga ameongoza jopo la Wataalam  kutoka Wizara ya Nishati katika Kikao cha awali cha Kamati Ndogo ya Nishati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kilicholenga kujadili  maandalizi ya Mkutano wa Pamoja wa Kamati ya Mawaziri wa SADC wanaoshughulikia masuala ya Nishati utakaofanyika nchini Zimbabwe.

Kikao hicho cha awali kimefanyika tarehe 30 Mei 2025 katika Ukumbi wa Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao.

Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa SADC unatarajia kufanyika nchini Zimbabwe  Mei  30  had 04 Juni 2025 ukitanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Nishati wa SADC.

Kikao hicho cha Mawaziri  kitajadili ajenda mbalimbali ikiwemo hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme katika Kanda; Maendeleo ya sekta ndogo ya Mafuta na Gesi, Matumizi ya Nishati Safi na kujadili nafasi na utayari wa Kanda katika kutekeleza Azimo la Dar es Salaam lililotokana na Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Misheni 300.



Washiriki wengine katika kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao wametoka katika  nchi zote zilizopo katika Jumuiya ya SADC.

WAZIRI KOMBO AWASISITIZA MACHIFU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

May 30, 2025 Add Comment
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amewasisitiza Machifu wa Kanda ya Vita ya Majimaji Kusini mwa Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali wakati wakitekeleza majukumu yao ya kimila katika jamii.