WADAU WAJADILI MPANGO MAHSUSI WA NISHATI KATIKA WIKI YA NISHATI JADIDIFU

May 29, 2025 Add Comment


Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga ameongoza wadau mbalimbali kujadili utekelezaji wa Mpango Mahsusi wa Nishati wa Misheni 300. 


Mjadala huo umefanyika  katika Wiki ya Nishati Jadidifu 2025 inayoendelea jijini Dar es Salaam.

Masuala mbalimbali yamejadiliwa ikiwemo namna ya kuvutia na kushirikisha wawekezaji kutoka sekta binafsi na taasisi za kifedha, ili kufikia malengo yaliyowekwa katika Mpango Mahsusi wa Nishati  ikiwemo kuhakikisha asilimia 75 ya wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2030.





WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA JAPAN

May 29, 2025 Add Comment


_▪️Asema Japan itaendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania_

_▪️Aagiza tathmini ya barabara za Kibiti-Lindi na Morogoro-Dodoma_


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na Waziri Mkuu wa Japan, Ishiba  Shigeru ambaye amemuhakikishia kuwa nchi hiyo itaendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania jambo ambalo linalenga kuchochea ukuaji wa uchumi kutokana na fursa zitakazoendelea kupatikana kupitia mahusiano hayo.


Amekutana na kiongozi huyo leo (Alhamisi, Mei 29, 2025) katika ofisi ya Waziri Mkuu Tokyo, Japan, ambapo Mheshimiwa Majaliwa amesema ahadi hiyo inazidi kutoa fursa ya wawekezaji na wafanyabiashara wa Japan pamoja na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) kuendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kumueleza Waziri Mkuu huyo kuwa  pamoja na miradi mingine wanayotekeleza nchini, Japan kupitia JICA iangalie uwezekano wa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuzifanyia ukarabati mkubwa barabara za Morogoro-Dodoma na barabara ya Kibiti-Lindi ambayo imeharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.

Amesema Waziri Mkuu wa Japan baada ya kupata maelezo hayo ameuelekeza uongozi wa JICA pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania Youichi Mikami kwenda kutembelea barabara hizo na kuzifanyia tathmini ya uharibifu na kisha kuwasilisha taarifa ili Serikali ya Japan ione namna itakavyoshirikiana na Tanzania katika utekelezaji wake.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Japan amepongeza kuendelea kuimarika kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Japan na kwamba ameahidi kuhakikisha makampuni mbalimbali ya Japan yataendelea kufanyakazi na Tanzania ili kuisaidia katika kukuza uchumi, kuendelea masuala ya kijamii na teknolojia kwani wanatambua idadi ya watu nchini inaendelea kuongezeka.



WIZARA YA NISHATI YASHIRIKI WIKI YA NISHATI JADIDIFU JIJINI DAR ES SALAAM

May 28, 2025 Add Comment



Wizara ya Nishati imeshiriki Wiki ya Nishati Jadidifu 2025 inayoendelea jijini Dar es Salaam.

Katika picha ni Wadau na Wageni mbalimbali walipotembelea Banda la Wizara na kupata elimu juu ya masuala mbalimbali ikiwemo umeme na Nishati Jadidifu.

 Wiki ya Nishati Jadidifu inafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).



SERIKALI KUKAMILISHA UJENZI WA VETA WILAYA ZOTE

May 28, 2025 Add Comment
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe profesa Adolf Mkenda amesema serikali inaendelea na ujenzi wa vyuo vya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika Wilaya 64 nchini.

UMOJA WA ULAYA WAIPA KONGOLE REA

May 28, 2025 Add Comment
-Kwa kuwa kinara katika kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia