WAZIRI AWESO ACHAGULIWA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAWAZIRI WA ZAMCOM 2025/2026

May 16, 2025 Add Comment


Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia Mhe  Caesar Chacha Waitara, amemwakilisha Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso (Mb), Waziri wa Maji katika Mkutano wa 12 wa Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (Zambezi Watercourse Commission-ZAMCOM) uliofanyika tarehe 15 Mei 2025 jijini Windhoek, Namibia.

Katika mkutano huo wa ZAMCOM unaojumuisha nchi nane za Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Msumbiji, Namibia, Zambia na Zimbabwe, Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso (Mb) amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa ZAMCOM katika kipindi cha mwaka 2025/2026.





Serikali Kuanza Kutambua Wanafunzi Kila Hatua Kupitia Mfumo Mpya

May 15, 2025 Add Comment

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatarajia kuanzisha mfumo shirikishi wa tafiti za elimu ili kuboresha ufundishaji, ujifunzaji, na usimamizi wa takwimu ambao utarahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu kwa wadau wa elimu.

Mke wa Rais Finland Afanya “Royal Tour” Makumbusho ya Taifa Dar

May 15, 2025 Add Comment

Na Mwandishi Wetu

Mke wa Rais wa Finland, Suzanne Innes-Stubb, leo Jumanne Mei 14, 2025, amefanya “Royal Tour” kwenye Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine alifurahia sana historia ya zamadam na utamaduni wa Tanzania.

DKT.BITEKO ATETA NA SPIKA WA BUNGE LA MOROCCO

May 15, 2025 Add Comment


📌 *Tanzania, Morocco wakubaliana kuimarisha ushirikiano*


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe Dkt. Doto Biteko ametembelea Bunge la Morocco ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini humo.

Akiwa Bungeni hapo, Dkt. Biteko amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la nchi hiyo Mhe. Rachid Talbi El Alami na Naibu Spika Mhe. Lahcen Haddad katika ofisi za Bunge hilo zilizoko jijini Rabat nchini Morocco.

Pamoja na mambo mengine, wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika Sekta ya Nishati, Kilimo, Viwanda na Biashara.






CCM TANGA KUSHIRIKIANA NA TFF KUBADILISHA MUONEKANO WA UWANJA WA CCM MKWAKWANI

May 15, 2025 Add Comment

 






Na Oscar Assenga,TANGA

KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga wamefanya ziara maalumu ya ukaguzi wa uwanja wa CCM Mkwakwani ambao umefanyiwa maboresho makubwa na hivyo unaweza kutumika kwenye mchezo wa nusu fainali wa CRDB Federation Cup kati ya timu ya Yanga na JKT.

Akizungumza mara baada ya kuutembelea uwanja huo,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman alisema kwamba uwanja huo kutokana na maboresho makubwa upo tayari kwa ajili ya mchezo huo utacheza Mei 18 mwaka huu.

Alisema kwamba walifanya maboresho makubwa ya uwanja huo sehemu ya kuchezea ambayo ilikuwa na changamoto awali kwa jitihada walizifanya viongozi kwa kushirikiana na TFF kupitia Rais Karia waliwaunga mkono CCM kwa jitihada za kufanya ukarabati wa uwanja wao na TFF kugharamia majani sasa mambo yapo vizuri.

Aidha alisema lakini matarajio yao kwa kushirikiana na TFF wameshaandaa michoro namna ya kuubadilisha muonekano wa uwanja huo uwanja wa Mkwakwani kwa kuweka viti na kutengeneza jukwaa la kisasa.

“Lakini pamoja na hilo pia tutabadilisha muonekano wa vyumba vya kubadilisha nguo,vyoo nk na sasa hivi tumeshakamilisha michoro na tupo kwenye mchakato wa kutafuta wadau ili waweze kutuunga mkono

Hata hivyo alisema kwamba mchezo wa Nusu Fainali hiyo kuchezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Jijini Tanga ni heshima kubwa kwao na wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.

Mwenyekiti huyo alitoa wito kwa wapenzi wa soka nchini kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuweza kuipa sapoti nusu fainali hiyo .

Mwisho.