WAZIRI CHANA AZINDUA MRADI WA DOLA MILIONI 5.8 KUHIFADHI MISITU YA ASILIA

May 05, 2025 Add Comment

 



Na Mwandishi Wetu,Pwani.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), amezindua  mradi wa 'Kuimarisha Ustahimilivu wa Bioanuai ya Misitu ya Mazingira Asilia Tanzania dhidi ya Athari za Mabadiliko ya Tabianchi', wenye thamani ya Dola za Kimarekani 5.8 milioni.

 Mradi huo umefadhiliwa na Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Uzinduzi huo umefanyika leo, Mei 5, 2025, katika Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia wa Pugu–Kazimzumbwi, wilayani Kisarawe, mkoa wa Pwani, sambamba na uzinduzi wa Mkakati wa Kuokoa Ardhi ya Misitu Iliyoharibika.



Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Chana amesema mradi huo unalenga kuongeza ustahimilivu wa misitu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kuimarisha mifumo ya ulinzi, kusaidia shughuli rafiki kwa mazingira kama vile utalii, na kuimarisha mipaka, vituo vya ulinzi, pamoja na vifaa vya kukabiliana na majanga kama moto wa msituni.

Aidha, amesema mradi utasaidia jamii zinazozunguka misitu kwa kuwapatia shughuli mbadala za kiuchumi zitakazosaidia kupunguza utegemezi wa moja kwa moja kwenye misitu.

“Mradi huu wa miaka sita, kuanzia Septemba 2023 hadi 2029, unatekelezwa kwa ufadhili wa GEF na UNDP kwa gharama ya Dola za Kimarekani 5,837,010,” amesema Mhe. Chana.

Amesema mradi huo utatekelezwa katika misitu tisa ya hifadhi iliyoko kwenye mikoa mitano: Hassama Hills, Nou na Mlima Hanang (Manyara), Uzigua na Pugu–Kazimzumbwi (Pwani), Pindiro na Rondo (Lindi), Mwambesi (Ruvuma) na Essimingor (Arusha).


Waziri Chana ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi utasaidia kuimarisha uwezo wa hifadhi hizo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuongeza mapato ya Serikali kupitia TFS, kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na jamii za jirani na kujenga uthabiti wa mifumo ya ikolojia kwa kuunganisha hifadhi za mazingira asilia na maeneo mengine ya uhifadhi.

Aidha, Waziri amewapongeza wadau wa maendeleo na asasi za kiraia kwa mchango wao mkubwa katika juhudi za Serikali za kuhifadhi misitu, na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano huo kwa manufaa ya taifa na vizazi vijavyo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amesisitiza juu ya wananchi kutunza na kuhifadhi maliasili za misitu huku akitoa onyo kwa wanaokiuka taratibu za uhifadhi kuchukuliwa hatua kali.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shigeki Komatsubara  amesema mradi huo ni muhimu kwa Tanzania kutokana na athari mbambali zinazoikumba misitu ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, uchomaji moto hivyo utasaidia kuirisha maisha ya na vipato vya wananchi kwa kuacha kutegemea misitu.


Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Wizara ya Fedha, TAMISEMI, wilaya ya Kisarawe, Wizara ya Maliasili na Utalii, TFS, pamoja na wadau wa maendeleo.

MWISHO.

INEC YAWATAKA WANANCHI KUTUMIA SIKU ZILIZOBAKI KUBORESHA TAARIFA ZAO

May 05, 2025 Add Comment


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele (shati la drafti) akiwa katika kituo cha shule ya Msingi Mahela katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Katavi wakati akitembelea vituo mbalimbali vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mkoa huo jana. Kulia walio simama ni Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Mbinga Mjini, Ndg. Amina Hamisi Seif. (Picha na INEC).

 Na Mwandishi Wetu, Ruvuma


Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imewataka wananchi wa mikoa 15 inayotekeleza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mzunguko wa kwanza wa awamu ya pili kuzitumia siku chache zilizobaki katika mikoa yao kuhakikisha wanajitokeza kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao ili wasijekosa haki yao ya msingi ya kupiga Kura katika uchaguzi ujao mwaka huu.

Hayo yamesema na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele wakati akitembelea vituo mbalimbali vya uboreshaji wa Daftari hilo katika Katika halsmahauri za Mkoa wa Ruvuma.

“Nawasihi wananchi wa mikoa 15 ambayo awamu ya pili ya Uboreshaji Daftari inafanyika wandelee kujitokeza kuja kuboresha, waendelee kujiandikisha lakini pia kuwaondoa wale ambao hawastahili kuwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, tumebakiwa na siku chache zinazotakiwa kuendelea na zoezi,” alisema Jaji Mwambegele.

Jaji Mwambegele amesema zoezi la uboreshaji wa wa awamu ya pili linakwenda sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la awali la kudumu la wapiga Kura ambalo linatoa fursa kwa wananchi kukagua, kufanya marekebisho ya taarifa za wapiga kura na uwekaji wa pingamizi dhidi ya wapiga kura waliomo kwenye daftari ambao hawana sifa na litabandikwa katika vituo vyote vilivyotumika wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza.

Akizungumzia kuhusu mwenendo wa zoezi hilo kwa ujumla Jaji Mwambegele amesema zoezi linakwenda vizuri na mwitikio wa wananchi ni mzuri kwani maeneo aliyotembelea katika mikoa ya Iringa, Njombe na Ruvuma wananchi wamejitokeza vituoni kujiandikisha, kuboresha taarifa zao pamoja na kutoa taarifa za watu waliopoteza sifa za kuwepo kwenye Daftari hilo.

“Kwa ujumla wake zoezi linakwenda vizuri na wananchi wengi wamejitokeza kwaajili ya kuboresha taarifa zao, wamejitokeza pia kwaajili ya kuboresha taarifa zao na pia, wale ambao hawastahili kuwepo katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura wamefutwa,katika kila kituo nil;ichokwenda wameniambia kuhusu wale walio waandikisha, waboresha na wale waliowafuta,” alisema.

Uboreshaji wa Daftari unafanyika kwa mizunguko mitatu ambapo mzunguko wa kwanza unajumuisha mikoa 15, mzunguko wa pili utajumuisha mikoa 16 na mzunguko wa tatu utajumuisha vituo vya magereza na vyuo vya mafunzo.

Mikoa inayohusika kwenye mzunguko wa kwanza wa uboreshaji ni pamoja na Iringa, Geita, Kagera, Mara, Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Rukwa, Tabora, Katavi, Kigoma, Ruvuma, Mbeya, Njombe na Songwe ambapo zoezi hilo lilianza kutekelezwa tangu Mei 1 na linataraji kukamilika Mei 7 mwaka huu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Maafisa Waandikishaji kutoka Majimbo ya Nyasa, Ndg. Khalid Khalifa na yule wa Jimbo la Mbinga Mjini Ndg. Amina Hamisi Seif wamesema zoezi la Uboreshaji katika maeneo yao linakwenda vizuri na kuwahimiza wananchi kuendelea kujitokeza.

“Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa tumekwisha andikisha wapiga kura wapya 436 na kuboresha taarifa za wapiga kura 415 wakati wapiga kura 68 wamepoteza sifa na kufutwa katika Daftari la Kudumu, bado tuzazo siku hivyo niombe kutumia fursa hii kuwataka wananchi waendelee kujitokeza,” alisema Khalifa.

Katika awamu ya pili ya uboreshaji, wapiga kura wapya 1,396,609 wataandikishwa, wapiga kura 1,092,383 wataboresha taarifa zao na wapiga kura 148,624 watafutwa kwenye Daftari kwa kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye Daftari,” amesema Jaji Mwambegele.

Tume iliboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza kuanzia tarehe 20 Julai, 2024 na kukamilisha tarehe 25 Machi, 2025.



Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele (kulia) akiwa katika kituo cha shule ya Msingi Mahela katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Katavi wakati akitembelea vituo mbalimbali vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mkoa huo jana. Wapili Kulia ni Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Nyasa, Ndg. Khalid Khalifa. (Picha na INEC).

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele (Kushoto) akimkabidhi kadi ya Mpiga Kura Ndg. Acheni Maulid mkazi wa Mbamba Bay katika Halmashauri ya Wilaya ya nyasa aliyefika katika kituo cha Shule ya msingi Mbamba bay kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. (Picha na INEC).

HAKIELIMU YAPENDEKEZA ONGEZEKO LA TRILIONI 2.08 KATIKA BAJETI SEKTA YA ELIMU

May 05, 2025 Add Comment
NA EMMANUEL MBATILO, 

TAASISI ya HakiElimu imeishauri Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha angalau asilimia 15 ya bajeti ya taifa ya 2025/26 inatengwa kwajili ya sekta ya elimu ambapo wanatarajia ongezeko la shilingi trilioni 2.08 katika bajeti ya sekta ya elimu kutoka shilingi trilioni 6.17 ya mwaka 2024/25 hadi kufikia shilingi trilioni 8.25 mwaka wa fedha 2025/26.

TANGA YETU NA BODI YA FILAMU WATOA MAFUNZO KWA WAANDAAJI WA FILAMU MKOANI TANGA

May 05, 2025 Add Comment






Na Oscar Assenga, Tanga

 

Tanga Yetu kupitia mradi wa Fursa kwa Vijana (GOYN TANGA ) kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu Tanzania wametoa mafunzo kwa ajili ya utengenezaji wa filamu kwa wasanii mkoani Tanga ili waweze kuwa waandaaji wazuri ambao watafanya vizuri kupitia tasnia hiyo.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Filamu kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Ally Makata kwa niaba ya Serikali alisema kwamba wamekuja Tanga mara ya pili kutoa mafunzo kuhusu utengenezaji wa filamu kwa wasanii wa filamu mkoani Tanga.

Alisema kwamba mafunzo hayo waliyatoa kwa awamu tatu ambapo ya kwanza ilikuwa ni watu wakwenda kufanya utafiti watu wapate wazo kwamba endapo watapata muongozo nani anaweza kucheza na bajeti ya kiasi gani na nani anaweza kufadhili ikiwemo kutengeneza hadithi fupi fupi lazima mdau yoyote kwenye filamu aweza kufanya hivyo ili aweze kufanya vizuri.

 

Aidha alisema kwamba baada ya hapo awamu ya pili na tatu ni kushika Kamera kuona namna kutengeneza mwanga na watu kwenda kwenye maeneo husika na uhariri pamoja na namna ya kupanga na kutengeneza sauti ili uweza kupata picha kamili na viti vyengine.

“Tunawashukuru Tanga Yetu kwa kuweza kufadhili na kushirikiana na Bodi ya Filamu nchini kwa watayarishaji wa Mkoa wa Tanga waweze kupata maarifa kutokana na kwamba Tanga kwa asilimia kubwa  ipo chini na watayarishaji wa Tanga wanalalamika kwenye media wanaoka kazi za mikoa mengine na ikitokea tuzo mikoa mwengine inashika tuzo”Alisema

“Wakati ukiangalia Tanga kuna rasimali za kila kitu ukiangalia mandhara wana sehemu za vivutio wana mazingira mazuri tamaduni wana vyakula tamaduni watu wanaishi kila siku kwanini tusipate Filamu inayoakisi Jamii ya Mkoa wa Tanga “Alisema

Alisema kwamba ukiangalia Marehemu King Majuto ameshaandoka ambaye alikuwa anaiwakilisha vizuri mkoa wa Tanga ikiwemo Marehemu Bauji tunapata stori kulikuwa na waandishi wazuri na waigizaji wazuri lakini sasa haifanyiki hivyo shabaha kubwa ya Dkt Omari na Taasisi ya Tanga Yetu ni kuona namna Tanga inarudi upya.

 

Aliongeza kwamba ukiachana na hayo mafunzo wanaandaa mpango mkakati wa kuona mtayarishaji wa Tanga endapo ataomba Fedha DW na Taasisi mbalimbali ataulizwa historia ya sehemu alipo sasa wakipata mpango mkakati itakuwa rahisi watayarishaji wa mkoa wa Tanga kuchukua mpango mkakati na kuandaa kila wanachokiandaa na kwenda kuombea fedha.

 

Alisema wanawapatia mafunzo na maarifa ili kesho na kesho kutwa waweze kufanya vizuri mkoa wa Tanga ili waweze kufanya vziuri na kurejesha katika hali yake ya kawaida na kung’ara vziuri.

 

Awali akizungumza Mkurugenzi wa HD Consalt Omari Bakari ambao wanatekeleza mradi wa Fursa kwa vijana wa Tanga (GOYN) kupitia program ya Tanga Yetu alisema lengo kubwa ni kuhakikisha vijana wa Jiji la Tanga wanapata fursa ya kuajiriwa au kujiajiri wenyewe.

 

Alisema uchambuzi ambao waliifanya na ofisi ya Taifa ya Takwimu vijana walionekana kutokuea na mahotaji sawa kutokana kila mmoja na uwezo wake na chaguo lake mpango huo wanaoshirikiana na Bodi ya Filamu ni inalenga kusaidia kufikia lengo kwa vijana wale ambao walisema wanapenda kuwa kwenye filamu.

 

Alisema waliamua kushirikiana na Bodi ya Filamu kama Taasisi ya Serikali waliamini kama wana majukumu ya kusimamia,kuhamasisha na kutangaza hiyo sekta kwa hiyo walikubaliana  kuendelea na kusaidia hayo mafunzo yaliyoanza kwenye uzalishaji na wazo kubwa ni kuhakikisha vijana wanapata uzoefu kwenye sekta binafasi ambazo zinashirikiana na bodi ya filamu.

 

“Leo imefikia mwisho wa awamu ya pili na tutaenda kwenye awamu ya tatu kuzalisha filamu ambazo zitakwenda kwenye soko hivyo niwaombe wadau mbalimbali hao vijana wapo vizuri ni kuwaamini na kuwapa kazi ambazo wanaweza kufanya nao wataweza kuwasaidia”Alisema


RAIS SAMIA ALIPA BIL 539 UKAMILISHAJI DARAJA LA JP MAGUFULI, MRADI WAKAMILIKA ASILIMIA 99

May 05, 2025 Add Comment

Wakati Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiingia madarakani mwaka 2021, ujenzi wa daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi) mkoani Mwanza ulikuwa umefikia takribani asilimia 25 na kutokana changamoto za kutetereka kwa uchumi wa dunia baada ya janga la Uviko 19, hivyo kuwa na wasiwasi wa upatikanaji wa fedha.