Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

MHE.KAPINGA AENDELEA KUWANADO WAGOMBEA WA CCM

November 24, 2024 Add Comment

 


🗒️ *23 Novemba,2024.* 


📍 *MBINGA-RUVUMA* 🇹🇿🌍.



🔗 *Aeleza jinsi Ilani ya CCM ilivyotekelezwa kwa mafanikio makubwa.* 


🔗 *Kapinga asema maendeleo yaliyofanyika yanaonekana wazi,hayaitaji tochi.* 


📡📡Mbunge wa Vijana Taifa kupitia Mkoa wa Ruvuma na Naibu Waziri wa Nishati, *Mhe.Judith Kapinga* leo tarehe *23.11.2024* Katika Kijiji Cha *Lihale* -Kata ya *Mkako* ,Wilayani *Mbinga* ameendelea na Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa/Vijiji na Vitongoji✍️.






📡📡 *Mhe.Kapinga* amewanadi na kuwaombea Kura kwa Wananchi Wagombea wote wa CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika tarehe *27.11.2024* ,aidha Mh.Kapinga ameambatana na Viongozi wa Jumuiya ya UWT Wilaya ya Mbinga✍️.


       *Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Viti Maalumu Vijana Taifa-Ruvuma.Leo tarehe 23.11.2024.*

CHATO MSIFANYE MAKOSA KUCHAGUA VYAMA VYENGINE -DKT.BITEKO

November 23, 2024 Add Comment



📌 *Rais Samia Avunja Rekodi Miradi ya Maendeleo Chato*


📌 *Asema CCM Itabeba Vyote*


📌 *Kalemani Ataja Mabilioni ya Miradi Chato*


📌 *Asema CCM Inatekeleza Ahadi*


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wananchi wa Chato kuchagua wagombea wa CCM ili kuendeleza miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya yao.


Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 23,2024 wakati akihutubia katika  Kampeni zinazoendelea za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Wilaya ya Chato zilizofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Bwanga, vilivyopo mkoani Geita. 


Amesema CCM ina nia ya kuendelea kuleta maendeleo huku  akivitaka vyama vingine vishindane kwa hoja sio kwa matusi na kuwa nyenzo za kuunganisha  Watanzania sio kuwagawa.


“ Nawaomba muwasikilize vyama vingine lakini msifanye kosa la kuwachagua maana wanataka vyeo tu, msikubali watu wanaowaambia mkunje ngumi hawana ilani iliyopitishwa na wananchi wala bajeti wanataka muwachague wakafanye kazi gani?,” amehoji Dkt. Biteko.



Ameendelea kusema Uchaguzi wa Mwaka 2024,  CCM imejipanga kushinda na si kubahatisha kwa kuwa na mipango yake imeanza kwa wanachama wake kujitokeza kwenye uandikishaji daftari la wapiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.


“ Chato waliojiandikisha kwenye daftari la kupiga kura walifika zaidi ya 200,000 na  bila shaka wataenda kupiga  kura, CCM tuna uwezo wa kuleta maendeleo kwenye wilaya yenu, viongozi watakaochaguliwa wataenda kufanya kazi kwa sababu ilani ipo, CCM wana ilani na mipango wengine hawana,” ameeleza Dkt. Biteko.

 

Aidha, amesema tangu Rais Samia aingie madarakani CCM imekuwa na kauli mbiu ya kazi iendelee huku ikiendeleza kwa juhudi kubwa miradi ya maendeleo kwa maslahi ya nchi .


Ametaja miradi hiyo  kuwa ni mradi wa kufua wa umeme wa  Bwawa la Julius Nyerere ambao sasa unafanya kazi, treni ya umeme ya kisasa (SGR) inafanya kazi kutoka Dar es salaam hadi Dodoma, kuimarisha shirika la ndege kwa kuongeza idadi ya ndege.



Fauka ya hayo, Dkt. Biteko amesema CCM inaheshimu Uchaguzi huo wa Serikali Mtaa na ndio maana viongozi wake wote wamesambaa katika  maeneo mbalimbali kueleza umuhimu wa uchaguzi huo.


“ CCM tuna sababu za kuomba kura kwa sababu tumepiga kazi na inaoonekana watu wa Chato tupigie kura kuchagua wagombea wa CCM katika vitongoji vyote na vijiji hakuna kumwachia mtu kwa kuwa wengine hawana ilani wala mipango,” amefafanua Dkt. Biteko.


Mbunge wa Chato, Mhe. Dkt. Medard Kalemani ametoa shukrani kwa Rais Samia kwa jitihada zake za kuiletea maendeleo wilayani Chato.


Amebainisha  katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Chato imepata shilingi bilioni 197.28 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maendeleo. “Tumepata shilingi milioni 100 kwa ajili ya kujenga kituo cha mabasi, kwenye kituo cha afya Rais Samia ametupa fedha kwa ajili ya kukikarabati,”


Amesisitiza “ Hapa Bwanga awali kulikuwa na shida ya umeme tunakushukuru sasa umeme umefika katika vitongoji na vijiji 15. Nataka nikuhakikishie kwa fedha tulizopata za miradi mikubwa kumi ikiwemo mradi wa uwanja wa ndege ambao unaendelea vizuri ndege zinatua, ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mipango na Fedha kimekamilika na mwezi ujao kinafunguliwa, ujenzi wa maktaba ya kanda inayogharimu shilingi bilioni 7.2 ambayo imeshaezekwa,” 


Amewahimiza wananchi wa Bwanga kuchagua wagombea wa CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuendeleza  maendeleo Bwanga na Chato kwa ujumla


MWISHO

ISSA GAVU AANIKA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA KATIKA MKOA WA GEITA

November 22, 2024 Add Comment


KATIBU wa Halmashauri Kuu(NEC) Oganaisheni na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Issa Gavu ameelezea hatua kwa hatua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika Mkoa wa Geita pamoja na mikoa mingine nchini.

Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na kuboresha Kituo Cha mabasi Geita kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanaokwenda kupata huduma katika Kituo hicho hawapati kero wala usumbufu na tayari fedha Sh.bilioni 14 zimetengwa kwa ajili ya Kituo hicho.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara alipokuwa akizindua kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Gavu amesisitiza Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imejipanga kuboresha kituo cha mabasi ili wananchi wapate huduma na tayari utaratibu wa kutafuta zabuni ili kumpata mkandarasi imeanza na muda si mrefu mradi utaanza kutekelezwa.

"Lengo letu ni kutaka kuona jamii ya Watanzania kila mmoja katika huduma zake anapata huduma iliyosafi na salama bila usumbufu wowote.Katika maeneo ya Mji wa Geita yako maeneo yaliyokuwa hajakamilika katika uimarishaji wa barabara za lami hivyo Serikali ya CCM imetanga fedha kwa ajili ya kuanza mradi wa ujenzi wa kilometa 17 za lami katika Mji huu wa Geita

"Lengo ni kuimarisha miundombinu ya barabara za lami katika Mji wa Geita ili kuupandisha hadhi Mji wetu.Katika upande wa elimu tayari Serikali ya CCM imejenga takriban shule 180 katika Mkoa wa Geita na shule hizo ni mpya ziko za msingi na Sekondari .Ipo shule ya wasichana yenye thamani ya sh.bilioni tatu...

"Hii ni kuonesha Serikali inamjali mtoto wa kike katika umuhimu wa kupata elimu lazima tuendelee tuendelee na kutuamini kwamba mipango yetu ni kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa faifa ya jamii kwa watu wa kizazi cha leo na kesho,"amesema Gavu.

Ameongeza kuwa miradi hiyo ikitunzwa itakuwa na faida kubwa kwa jamii huku akielezea pia hatua ambazo Serikali imechukua katika kuboresha huduma za afya kwani imejenga hospitali kubwa yenye thamani ya Sh.bilioni 20 katika Mji wa Geita ili kuimarisha huduma za afya kwa wananchi.

Pia amesema Serikali ya CCM imeendelea kujenga zahanati,vituo vya afya pamoja na hospitali katika Mkoa huo na Mikoa mbalimbali nchini,hivyo amewaomba wananchi kuendelea kuwapa imani hiyo na wataendelea kuboresha maisha ya wananchi ili kila mwananchi afurahie uwepo wa Serikali ya CCM.

Kuhusu huduma ya upatikanaji umeme,Gavu amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya umeme katika Mkoa wa Geita na mikoa mingine nchini na kusisitiza Chama Cha Mapinduzi kimedhamiria kuendelea kuboresha huduma muhimu katika Jamii ya Watanzania .


BUKOMBE WANATAKA MAENDELEO NA MAENDELEO NI CCM-DKT BITEKO

November 21, 2024 Add Comment



*📌 Asema Vyama Vishindane kwa Sera na Utekelezaji wa Ahadi*


*📌WanaCCM Bukombe Waaswa Kuimarisha Ushirikiano*


*📌 Azindua Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Bukombe*


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa kwa miaka yote wananchi wa Wilaya ya Bukombe wamekuwa na imani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na kiu ya maendeleo.


Amesema wananchi hao wana haki ya kuchagua kati ya maneno au maendeleo na  wamekuwa wakitamani maendeleo kwa kuwa na shule, barabara na zahanati.



Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 21, 2024  wakati akifungua Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Wilaya ya Bukombe zilizofanyika katika Kata ya Igulwa, Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita.


“ Tunapozindua kampeni zetu tuna wajibu wa kuchagua maneno au maendeleo, tutashindanisha vyama kwa sera na kuonesha tuliyofanya kwa kipindi kilichopita. Tumekuja leo kuwaambia sisi tuko upande wa maendeleo na wengine wako upande wa maneno kama mwakilishi wenu nimekuja kuwaambia tuchague maendeleo, tuchague CCM,” amesema Dkt. Biteko.


Amesisitiza “ Tuliwahi kupata viongozi wa chama kingine na sasa tuna wajibu wa kupima kati yao na CCM mabadiliko yako chama gani,”







Akielezea hali ya uandikishaji wapiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mtaa, amesema kuwa mwaka 2024 Bukombe imefanikiwa kuandikisha idadi kubwa ya wapiga kura ambayo ni 228,659 ikiwa ni rekodi ya juu katika mkoa na ukanda huo hali inayodhihirisha ushindi kwa CCM na hasa kutokana na utekelezaji wa ilani yake.


Halikadhalika, Dkt. Biteko amesema asilimia 70 ya vitongoji vina wagombea wa CCM huku vyama vingine vikishindwa kuweka  wagombea.


“ Novemba 27, 2024 wote tukapige kura tunatakiwa kumshukuru Rais Samia kwa upendo na kwa kufanya  jitihada nyingi za kutujengea barabara, shule za msingi na sekondari, vyuo vya VETA, shule ya amali na mengineyo kwa haya yote twende tukawapigie kura wagombea wa CCM,” amesema Dkt. Biteko.



Pamoja na hayo amewaasa wananchi wa Bukombe kuhubiri umoja, amani na upendo hata baada ya uchaguzi kuisha sambamba na wagombea hao kuhudumia wananchi wa Bukombe.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Geita, Nicholaus Kasendamila amesema kuwa kazi ya CCM katika uchaguzi ni kushinda kwa ngazi zote za kata, vijiji, vitongozi.




Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Geita, Alexandrina Katabi amewataka wanachama wa CCM Wilaya ya Bukombe kuendelea kuimarisha umoja na ushirikiano wao hasa wakati huu wa kuelekea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.


Diwani wa Kata ya Bugelenga, Leonard Lubigisa akizungumza kwa niaba ya madiwani amewataka wanachama wa CCM kupiga kura ifakapo Novemba 27, 2024.


Aidha, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kupelekea maendeleo katika Jimbo hilo na kuhamasisha wananchi kuichagua CCM kwa jitihada zake za ujenzi wa barabara pamoja na miradi mingine.


KATIBU MKUU WA NLD AZINDUA RASMI KAMPENI, ATOA WITO KWA VIONGOZI VYAMA VA SIASA KUFANYA SIASA ZA KISTAARABU

November 21, 2024 Add Comment




Na Oscar Assenga,HANDENI.

 

KATIBU Mkuu wa Chama cha NLD Doyo Hassan Doyo amezindua rasmi kampeni za wagombea wa chama hicho kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kata ya Kwedukwazu wilayani Handeni huku akitoa wito kwa viongozi wa chama hicho hapa nchini wafanye siasa za kistaarabu ambazo haziendi kutweza utu wa mtu.

 

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu ambapo vyama vya siasa ambazo zimeweka wagombea zitachuana ili kuweza kuwapata washindi ambao wataongoza Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji na wajumbe wa mitaa katika maeneo mbalimbali nchini.

 

Doyo aliyasema hayo mara baada ya kuzindua rasmi kampeni za chama hicho katika Kijiji cha Kwedikwazu Magharibu Kata ya Kabuku wilayani Handeni mkoani Tanga ambapo katika pamoja na mambo mengine aliwanadi wagombea ambao watachuana na vyama vyengine kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

 

Alisema anatoa wito huo kwa sababu chama cha siasa kina kazi kubwa ya kuwaunganisha watanzania na chama ambacho kitawa sambaratisha wasikipe nafasi katika uchaguzi huo ambao ni muhimu kwa maendeleo.

 

“Nitoe wito kwa Chama changu cha NLD sehemu tunazokwenda kufanya kampeni tufanye siasa za Kistaarabu ambazo zinakwenda kuwaunganisha watanzania na sio vyengivyo”Alisisitiza Katibu Mkuu huyo wa chama cha NLD.

 

Aidha pia alitoa wito kwa vyama vyote za siasa ambazo vimesimamisha wagombea katika uchaguzi huo wasifanye kampeni za kukwaza watu bali viheshimu watu na vinadi sera ili watanzania waweze kuamua chama gani kinaweza kuwasaidia katika kipindi cha miaka mitano ngazi ya mtaa na vitongoji.

 

“Huu ni wito nautoa kwa viongozi wa chama cha NLD nchi mzima wahakikisha wanafanya kampeni za kistaarabu na wasifanye zile ambazo zinakwenda kukwaza watu bali waheshimu watu na tunadi sera ili uchaguzi ukiisha waendelee kuheshimiana”Alisema  

 

Alisema wameamua kuzindua kampeni hizo katika Kijiji hicho kutokana na kwamba kwenye vitongoji 10 NLD imepata wagombea vitongoji vyote wakiwemo wajumbe, Mwenyekiti na wale wa viti maalumu ambao watachukua na vyama vya upinzani katika kinyang’anyiro hicho.

 

Awali Mwenyekiti wa NLD wilaya ya Handeni Rajabu Zakaria Doyo alimuomba Rais Dkt Samia Suluhu watupie macho kwenye ngazi ya usimamizi wa uchaguzi kwenye wilaya kwa sababu kuna katatizo ambako wenzao wanakileta wakati wa uchaguzi.

                       

Alisema kwa sababu wanapokwenda kusimamia watu kwa bunduki kwani watu hawagombani na wasimamizi ni mawakala ambao wamewateua na wao wanawasainisha na kisheria.

 

“Chumba cha kura hairuhusiwi mtu kuja na bunduki katika chumba cha kura wala kueleza kwamba wao ni viongozi wakubwa kwa sababu kuna watu wameteuliwa kusimamia uchaguzi huo lakini kubwa tumejipanga kufanya kampeni za kistaarabu”Alisema  Mwenyekiti Rajabu..