Na Oscar Assenga,TANGA TIMU ya Mchezo wa Riadhaa ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imeng’ara katika Mashindano ya Shimiwi yanayoendelea Jijini Tanga. Wachezaji wa timu ya Elimu ilianza kwa kasi katika mchezo huo wa Riadhaa ambapo wakimbiaji wake walikuwa hari kubwa ya kukimbiza upepo ili kuweza kupata ushindi katika mashindano hayo. Katika mchezo huo timu ya wanaume imefanya vizuri kwa upande wa mita 100 kupokezana vijiti huku kwenye zile za mita 200 wakiibuka washindi wa pili. Kwa upande wa michezo mengine timu za Wizara hiyo walipambana mpaka kufikia hatua ya nane bora kwa mchezo wa kuvuta kamba ,mpira wa miguu,mpira wa pete . Akizungumza kuhusu mashindano hayo Makamu Mwenyekiti ywa timu ya Elimu Sports Deogratius Wenga alisema kwamba mashindano hayo yamekuwa na ushindani mkubwa.
|
WAZIRI MCHENGERWA AIPONGEZA SIMBA KWA KUENDELEZA USHINDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA
michezo




Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameipongeza Timu ya Simba kwa kushinda kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba imeshinda mabao 2-0 dhidi ya timu Nyasa Big Bullet ya Malawi katika mchezo wa marudiani uliochezwa leo Septemba 18, 2022 kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mchengerwa ameambatana na Naibu Spika Mhe. Iddi Zungu, Katibu Mkuu wa Wizara yake Dkt. Hassan Abbasi na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Amesema watanzania na wanachama wa Simba wanafurahi kuona wanafanya vizuri katika mashindano haya ambapo amefafanua kuwa Mhe. Rais pia anaipongeza timu hiyo.
Ameongeza kuwa timu hiyo imeonyesha uzalendo ambao unapaswa kuendelezwa ili kuitangaza Tanzania Kimataifa.
Ameitaka timu hiyo kutoridhika na ushindi walioupata leo na badala yake iendelee kufanya mazoezi zaidi ili kujinoa hatimaye timu hiyo iingie fainali na kuweza kurejesha kombe nyumbani.
"Ninatoa wito kwa timu yetu kutobweteka na ushindi tulioupata leo, watanzania wanakiu ya ubingwa wa kombe hili. Tunahitaji kujituma na kutanguliza uzalendo ili tuwape raha watanzania". Amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kufanya uwekezaji katika michezo ili kuwasaidia wananchi kueluka na magonjwa hivyo kujenga afya zao.
Kapteni wa timu ya Simba John Boko amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele kwenye michezo.
TANGA PRESS CLUB WAFANYA BONANZA LA KUHAMASISHA SENSA NA KUTAMBUA JUHUDI ZA RAIS SAMIA SULUHU KATIKA MAENDELEO
michezo
Na Mwandishi Wetu,TANGA.
Bonanza la Mama Tumeikita lenye lengo la kuhamasisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Mkoani Tanga ikiwemo kutambua jitihaza za Rais Samia Suluhu katika maendeleo ya Taifa hapa .
Bonanza hilo ambalo liliandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga *TPC*limefanyika mwishoni mwa wiki Jijini Tanga kwenye viwanja vya Disuza kwa kushirikisha viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa Bonanza hilo Mkuu wa Mkoa Mgumba alisema aliupongeza uongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga chini ya Mwenyekiti wake Lulu George kwa kuanza na kuratibu bonanza hilo ambalo lilikuwa la aina yake.
Alisema ubunifu ambao umefanywa na uongozi wa klabu hiyo unapaswa kuungwa mkono huku akisema bonanza hilo limefanikiwa sana huku akiwataka viongozi hao kuhakikisha linakuwa endelevu mara kwa mara na kuwahaidi ushirikiano.
“Niwapongeze Tanga Press Club kwa ubunifu huu mkubwa mlioufanya kwa kuhamasisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi na kutambua juhudi za Rais kuwaletea maendeleo wa Tanga limefanikiwa sana nimpongeza Mwenyekiti wa TPC na viongozi wengine kwa kufanikisha bonanza hilo ambalo limewakutanisha pamoja wanajamii wote wa Tanga,viongozi wa mkoa wilaya mpaka vitongoji na waandishi wa habari”Alisema
Alisema kwamba amefurahishwa kwamba na kupendwa na ujumbe uliobebwa kwenye bonanza hilo mama huku akisisitiza umuhimu wa jamii ya wana Tanga kuhakikisha wanaendelea kushiriki zoezi la Sensa ya watu na Makazi ikiwemo kuendelea kuwahabarisha wana Tanga.
Awali akizungumza wakati wa Bonanza hilo Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa aliushukuru uongozi wa Tanga Press Club kuweza kuliandaa bonanza hilo ambalo limewakutanisha wadau mbalimbali kuishiriki katika michezo ambayo ni muhimu kiafya.
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka waandishi wa habari mkoani humo waendelee kuboresha mahusiano baina yao kwa wao na taasisi mbalimbali za serikali na kupitia wao wanaweza kuwa na mabonanza mbalimbali huku akiwaomba waone umuhimu wa kufanya hivyo.
.TUTAISHANGAZA DUNIA -TIMU YA JUMUIYA YA MADOLA
michezo

.jpg)
WAZIRI MCHENGERWA AITEMBELEA TIMU YA JUMUIYA YA MADOLA,AIFUNDA
michezo


