Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

WAZIRI MCHENGERWA ATOA SALAMU AFRIKA

May 25, 2022 Add Comment

 



Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohammed Mchengerwa

Na Shamimu Nyaki - WUSM, Dodoma 


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohammed Mchengerwa amewaasa watanzania kulinda na kuhifadhi rasilimali na kumbukumbu ambazo ni ushahidi wa Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika katika maeneo waliyopo ambayo kumbukumbu hizo zinapatikana.

Katika taarifa aliyoitoa kwa Vyombo vya Habari leo  Mei 25, 2022 jijini Dodoma, Mhe. Mchengerwa amesema  Siku ya Afrika ambayo huazimishwa Mei 25 kila Mwaka,ni siku muhimu kwa waafrika wote ambapo kwa mwaka huu  imebebwa na Kauli Mbiu isemayo "Urithi wa Ukombozi, Fahari ya Afrika na Kazi Iendelee".

"Kuthamini utanzania wetu  ni jambo la msingi na ndiyo kielelezo na sifa iliyosababisha Umoja wa Afrika (AU) zamani (OAU) kuichagua Tanzania kuwa Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi wa Bara la Afrika na kuipa hadhi ya kuwa Mratibu wa Harakati za Ukombozi hadi nchi zote za Afrika zilipopata Uhuru mwaka 1994" amefafanua Mhe.Mchengerwa.

Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa, ni wajibu wa jamii ya waafrika kuenzi kwa vitendo mashujaa wa Tanzania waliojitoa mhanga Kwa ajili ya Afrika chini ya Uongozi wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Katika kuadhimisha siku hiyo, watanzania wameaswa kutembelea Ofisi ya Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika  ili kujifunza na kuona ushahidi waTanzania katika kuikomboa Afrika.

BONANZA LA MBUNGE WA SEGEREA LAFANA

December 04, 2017

 


Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa amejumuika na wakazi wa jimbo lake katika  bonanza lilijomuisha michezo mbalimbali. Bonanza hilo lililofanyika katika uwanja wa Sigara uliopo Tabata lilikuwa ni hitimisho la mashindano ya Bonnah Cup 2017 ambapo fainali ilikuwa ni kati ya Kimanga Bodaboda na Sigara FC huku timu ya Bodaboda ikiibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4.