Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

DKT. BITEKO AZINDUA MPANGO WA UTEKELEZAJI AJENDA YA WANAWAKE, AMANI NA USALAMA

August 19, 2025 Add Comment

📌 Azitaka Wizara na Taasisi kutenga Bajeti kusimamia utekelezaji wa Mpango huo

📌 Awataka Wanawake kupambana katika maeneo waliyopo

📌 Awashukuru wadau wa maendeleo uandaaji wa Mpango huo

Na WMJJWM- Dar Es Salaam

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Mashaka Biteko amezindua Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutekeleza Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama 2025-2029.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mpango huo Agosti 19, 2025 uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani (TPTC) kilichopo Kunduchi mkoani Dar Es Salaam, Dkt. Biteko amezitaka Wizara na Taasisi za Serikali na Wadau mbalimbali wa maendeleo kuhakikisha wanatenga Bajeti ya utekelezaji wa Mpango huo ili kutimiza malengo yake.

"Naomba nitoe rai kwa Wizara zote zenye dhamana ya agenda hii; Tanzania Bara na Zanzibar; mkasimamie na kutekeleza mpango huu kama ilivyokusudiwa ili kufikia malengo stahiki" amesema Dkt. Biteko

Aidha Dkt. Biteko amesema katika utekelezaji wa Mpango huo amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakiwa Wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama kwenye maeneo yao kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Mpango huo kwa kushirikiana na wadau waliopo.

"Niwaombe kuhakikisha kuwa mnatoa elimu na kuhamasisha, ushiriki wa wanawake na wanaume katika hatua zote za kuzuia, kutatua migogoro na ujenzi wa amani, ulinzi na usalama." amesisitiza Dkt. Biteko

Akitoa salamu za Wizara Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema katika kuandaa Mpango huo, uainishaji wa maeneo mahsusi ya vipaumbele vya Mpango umezingatia maudhui ya Azimio Na. 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Ameongeza kuwa Mpango huo unabainisha maeneo manne (4) ya kipaumbele na kuwasilisha masuala ya msisitizo katika utekelezaji ikiwemo eneo la kuzuia linalosisitiza umuhimu wa kujumuisha mitazamo ya kijinsia katika mikakati ya kuzuia migogoro na mbinu za tahadhari za mapema, eneo la ushiriki linalosisitiza haja ya ushiriki wa wanawake katika kufanya maamuzi katika ngazi zote katika michakato ya amani, utatuzi wa migogoro na kujenga amani.

Akiyataja maeneo mengine kuwa ni eneo la ulinzi linalotoa wito wa kuimarishwa kwa hatua za kuwalinda wanawake na wasichana dhidi ya unyanyasaji wa kingono na kijinsia wakati na baada ya migogoro na eneo la Msaada na Urejeshaji wa Hali linalohimiza utekelezaji wa mbinu au jitihada zinazozingatia usawa wa kijinsia katika juhudi za usaidizi na uokoaji na wakati wa urejeshaji wa hali ya ustawi na utulivu baada ya migogoro.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi huo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Stergomena Tax amesema Tanzania imetambua kuwa ili kuimarisha amani Wanawake lazima washirikishwe katika Ajenda hii hivyo uwepo wa Mpango huo utaweka mikakati mahususi ya kushirikisha  wanawake katika amani na usalama na kuimarisha juhudi za Kitaifa katika kuzuia migogoro kukuza amani jumuishi na kulinda  Haki za Wanawake na wasichana.

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe amesema Ajenda Wanawake Amani na Usalama ni muhimu kwa maendeleo ya wanawake na Watanzania wote hivyo katika kutekeleza Ajenda hii Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeweka mikakati na mipango mbalimbali katika kuhakikisha Wanawake wanashirikishwa katika masuala ya amani na usalama na kukuza Usawa wa Kijinsia na  Ustawi wa Wanawake.

Naye Mkurugenzi wa Kanda wa UN Women  Anna Mutabati amesema katika utekelezaji wa Mpango huo Tanzania haianzi mwanzo bali inaendeleza mipango na mikakati iliyopo inayotekelezwa kuhusu masuala ya Wanawake Amani na Usalama chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo utaleta mabadiliko zaidi katika nyanja mbalimbali.

MWISHO

DKT. BITEKO AZINDUA MRADI UTAKAOWAKWAMUA VIJANA KIUCHUMI KATIKA MAENEO YANAYOPITIWA NA BOMBA LA MAFUTA GHAFI (EACOP)

August 18, 2025 Add Comment





📌 Unahusisha kuongezea vijana ujuzi, kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha, na kuondoa vikwazo vya ujasiriamali na ajira binafsi

📌 Ataka ujuzi unaotolewa kwa vijana uende sambamba na utoaji wa mitaji

📌 Awaasa Vijana kuchangamkia fursa na kuwa waaminifu wanapopata nafasi

 📌 Wanawake 6,130, Wanaume 4,905 na Makundi maalum 1,226 kufikiwa


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo amezindua Mpango wa Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Vijana (YEE) ambao unagusa maeneo yanayopitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) ikiwa ni jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali katika kuhakikisha kuwa jamii zilizo karibu na miradi zinanufaika na miradi hiyo.



Akizindua mradi huo katika Kijiji cha Bukombe, wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita tarehe 18 Agosti 2025, Dkt. Biteko amesema mradi huo wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi ni moja ya miradi iliyopangwa kuwezeshwa na Kampuni ya EACOP kwa kipindi cha ujenzi na baada ya ujenzi ikiwa ni sehemu ya Uwajibikaji wa Kampuni hiyo kwa jamii. 



Amesema mradi huo umepangwa kuwafikia zaidi ya vijana 12,261 ambapo miongoni mwao wanawake ni 6,130; wanaume 4,905 na makundi maalumu ni 1,226 katika awamu ya kwanza inayohusisha Mikoa ya Geita, Kagera, Tabora na Tanga. 


" Tunapozindua mradi huu hatuna budi kuwashukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda. Viongozi wetu hawa kwa nia yao  ya dhati na moyo wa uzalendo wameuendeleza na kuusimamia kikamilifu mradi huu wa EACOP ambao umefikia asilimia 65, tumefikia hapa sababu ya msukumo wao wa kutekeleza mradi huu" Amesema Dkt. Biteko
Ameeleza kuwa tangu kuanza kwa mradi wa EACOP mwaka 2022 hadi sasa, jumla ya Watanzania 9,194 wamepata nafasi za kufanya kazi ndani ya mradi na hivyo kuwa fursa kwao ya kujipatia kipato, mwaka 2024 kampuni ilitoa mafunzo maalumu kwa Vijana 170 na kuwapatia kazi kwenye mradi, Vijana wengine 110 wapo katika masomo na wanatarajiwa kujumlishwa pia katika Mradi huo pamoja na kutoa ufadhili wa Vijana 238 katika vyuo mbalimbali nchini. 
Amesema wananchi wanaopitiwa na miradi wanayo haki ya kunufaika na miradi lakini wana wajibu wa kulinda miundombinu ya mradi na kuufanya kuwa ni sehemu yao kwani unachangia pia kubadilisha maisha ya wananchi.
 Pia, Dkt. Biteko ameipongeza kampuni ya EACOP  na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kusimamia kwa ufanisi mradi huo huku akisisitiza kuwa, ili wananchi waone mradi huo ni sehemu yao lazima waone faida zake  hivyo miradi kama ya YEE inawapa chachu wananchi kulinda miundombinu ya EACOP kwa  wivu mkubwa.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesisitiza kuwa, kampuni mbalimbali zinazotekeleza miradi kuhakikisha kuwa hawaweki mkazo  kwenye kuongeza ujuzi tu kwa wananchi bali wanawapatia mitaji ili waweze kufanya vizuri zaidi.

Aidha, amewaasa vijana kuchangamkia fursa zinazotokea kwenye miradi, wajitume, wawe waaminifu pale wanapopata fursa na kueleza kuwa Serikali itaendelea kuwatengenezea fursa  ili wajikwamue kiuchumi na kuleta maendeleo nchini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi amesema Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengeneza mipango mikakati ya kuhakikisha vijana wanapewa fursa za ajira na mitaji kwenye maeneo mbalimbali ambapo mpango wa YEE ni kielelezo cha matokeo ya mipango hiyo.
Ameeleza kuwa, kumekuwa na programu mbalimbali ikiwemo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo kupitia programu hiyo zaidi ya shilingi trilioni tatu zilitolewa kwa Watanzania  takriban milioni 24 ikiwemo Wanawake, Vijana na Makundi maalum kwa lengo la kuwawezesha kujikwamua kiuchumi

Mkuu wa Mkoa Geita, Martine Shigella akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa inayopitiwa na mradi wa EACOP amesema kuwa mradi wa EACOP ni miongoni mwa miradi mikubwa ambayo wananchi wa Geita wamenufaika nayo kwa namna mbalimbali ikiwemo ajira za moja kwa moja na muda na mfupi pamoja na  mnyororo wa thamani kupitia biashara ya vyakula, mbogamboga, matunda n.k
Amesema Mpango wa uwezeshaji wa vijana kiuchumi ni matunda ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameendelea kuhakikisha vijana wanapata elimu na ujuzi hivyo mpango wa YEE unaongeza chachu hiyo ya utoaji elimu na ujuzi kwa wananchi wakiwemo vijana.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema utekelezaji wa mradi wa EACOP wenye urefu wa km 1443 ni moja ya miradi 17 inayotekelezwa na Wizara ya Nishati ikiwemo mradi wa Julius Nyerere ( MW 2,115) ambao umekamilika, miradi ya umeme ya Ruhudji, Rumakali na Malagarasi pamoja miradi mingine ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia ukiwemo wa Eyasi Wembere.
Katika mradi wa EACOP amesema Serikali imechangia shilingi trilioni 1.12 ambazo ni hisa za Tanzania na kuna kampuni za kitanzania 200 ambazo zinafanya kazi mbalimbali katika mradi ambazo zitalipwa jumla ya shilingi trilioni 1.325 ikiwa ni moja ya matunda ya uwepo wa mradi huo nchini.

Akieleza sababu za kufanyika.kwa uzinduzi wa mradi wa YEE wiiayani Bukombe amesema kuwa Bukombe  kuna  kituo kikubwa zaidi cha kusukuma mafuta yatakayotoka nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga, kuna kambi kubwa ya mradi wa EACOP na pia kilometa 20 za bomba hilo la mafuta zinapita katika eneo la Bukombe.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Makame ameeleza kuwa, TPDC imeendelea kushirikiana na kampuni ya EACOP kuhakikisha kuwa mahitaji ya wananchi yanabainishwa na kuzingatiwa katika utekelezaji wa mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

Ameeleza kuwa mahitaji yaliyoainishwa katika mradi wa YEE yaliandaliwa kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa kwa ngazi ya vijiji, Kata na Halmashauri zilizopo maeneo linapopita bomba la mafuta. 
Awali Clare Haule - Meneja wa Uwekezaji na Uwajibikaji kwa Jamii katika kampuni ya EACOP alisema mradi wa YEE umeanzishwa kwa kutambua kwamba zaidi ya asilimia 65 ya idadi ya watu wa Tanzania ni vijana chini ya umri wa miaka 35. Hata hivyo, vijana wengi hasa katika maeneo ya vijijini wanakumbana na vikwazo vingi kama vile ukosefu wa ajira, ukosefu wa mafunzo ya ufundi stadi , na ugumu wa kupata mitaji ya kuanzisha au kukuza biashara.
Alisema awamu ya kwanza ya Mradi wa YEE  utawawezesha kiuchumi vijana katika mikoa ya Geita, Kgera, Tabora na Tanga pamoja na mikoa mingine inayobaki itanufaika katika awamu ya pili ambayo ni Singida, Shinyanga, Dodoma na Manyara ambapo vijana watapewa ujuzi  unaolingana na mahitaji ya soko, kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha, na kuondoa vikwazo vya ujasiriamali na ajira binafsi.
Aliongeza kuwa, Mradi wa YEE ni sehemu ya Sera ya Uendelevu ya EACOP, chini ya nguzo ya Vizazi Vijavyo, inayolenga kujenga uwezo wa vijana na kuongeza upatikanaji wa fursa za kiuchumi katika jamii zinazoguswa na mradi.
Mwisho.

TARURA MUSOMA WAPONGEZWA UJENZI WA MIRADI KULINGANA NA THAMANI YA FEDHA

August 18, 2025 Add Comment


Na Mwandishi Wetu, Mara.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Ismail Ali Ussi amewapongeza wafanyakazi wa TARURA wilaya ya Musoma kwa kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanajenga miradi ya miundombinu ya barabara kulingana na thamani halisi ya fedha.

Ndugu Ussi ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara ya Nyabisarye Mahakama kuu Kanda ya Musoma yenye urefu wa Mita 700 kwa kiwango cha lami .

Ussi amesema kuwa Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa lengo la kuwarahisishia wananchi huduma katika maeneno yao ili waweze kufanya shughuli zao za kiuchumi na kujiingizia kipato.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Wilaya ya Musoma Mhandisi Mohamed Etanga amesema jumla ya shilingi Milioni 600.97 zimetengwa kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Nyabisarye- Mahakama Kuu yenye urefu wa Mita 700 kwa kiwango cha lami .

Amebainisha kuwa ujenzi wa barabara hiyo ulianza Oktoba mwaka jana na unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba, 2025.

Mhandisi Etanga ameongeza kusema kuwa barabara hiyo endapo itakamilika itakuwa kiunganishi cha Kata ya Bweri na Kata ya Rwamlimi na kuwa kiungo kikubwa kwa wananchi katika kupata mahitaji ya kijamii kwa wepesi.




WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKISAFIRI KWA TRENI YA UMEME YA KIWANGO CHA KIMATAIFA (SGR) KUTOKA DODOMA KUELEKEA DAR ES SALAAM LEO AGOSTI

August 18, 2025 Add Comment


 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisafiri kwa Treni ya umeme ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam, Agosti 18, 2025.



SERIKALI TUNAJIVUNIA MCHANGO WA TAASISI ZA DINI KIMAENDELEO- DKT.BITEKO

August 17, 2025 Add Comment


📌 Dkt. Biteko amwakilisha Makamu

wa Rais, Dkt Philip Mpango maadhimisho ya miaka 125 Parokia ya Kome - Geita


📌 Rais Samia achangia Tsh.Milioni 50 Ujenzi wa mradi wa maji Parokia ya Kome


📌 Maaskofu Waishukuru Serikali kwa ushirikiano na Taasisi za dini


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali  itaendelea kuziunga mkono na kushirikiana na taasisi zote za dini ili kuleta na kuchagiza maendeleo na Ustawi wa wananchi.

Dkt. Biteko amesema hayo Agosti 17, 2025 wakati akimwakilisha  Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango kuwa mgeni maalum katika maadhimisho ya  miaka 125 ya Ukristo na Uinjilishaji katika Parokia ya Kome, Jimbo Katoliki la Geita.

“ Niseme Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zote za dini katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na hii ni kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo” amesema Dkt. Biteko na kuongeza kuwa Serikali inafarijika kuyokana na mchango wa taasisi za dini kuwaletea wananchi maendeleo katika maeneo yao.

Sambamba na ibada hiyo ya Jubilei, Dkt. Biteko ameongoza Changizo kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kwa ajili ya huduma katika makazi ya Masisita, Parokia ya Kome.

Akizungumza mara baada ya misa, Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhasham FLavian Kassala Maombi ya Baraka kwa mchakato wa kupata viongozi na mchakato wa kupata viongozi sahihi katika uchaguzi Mkuu ujao mwezi Oktoba, 2025.


Mhasham Askofu Kassala ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya awamu ya sita kufuatia ushirikiano wa Serikali kwa taasisi za dini ambazo zimekuwa chachu ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini

Amesema huduma ya maji safi na salama katika Kisiwa cha Kome bado ni changamoto hivyo, ameiomba Serikali kufanikisha mpango wa upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wa Kome.


“ Pamoja na kwamba hapa ni kisiwa na tumezungukwa na maji, huduma ya maji safi bado ni ndogo na wananchi wenye uwezo wa kupata maji ni wachache,” amesema Askofu Kassala

Amesema Kanisa liko katika jitihada za kusogeza huduma za jamii kwa kuongeza watawa zaidi ambo watatoa huduma za jamii na hiyo wanahitaji huduma za haraka.



Dkt. Biteko amesema serikali itafanya upembuzi ili kuhakikisha huduma hiyo ya maji ili kuhakikisha watawa wanapata maji.

Amewaomba wakazi wa Kome kuzidisha moyo wa ushirikiano sambamba na kuboresha mazingira na kupanda miti ili kulinda na kurejeaha uoto wa asili.


Aidha, amechangia kiasi cha shilingi milioni 10 huku akiwasilisha mchango wa shilingili milioni 50 kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya kufanikisha azma ya kufanikisha upatikanaji wa huduma ya maji katika makazi ya watawa Kome.

Awali akihubiri katika ibada ya maadhimisho ya miaka 125 tangu kuanzishwa kwa utume katika Parokia ya Kome, Askofu Mkuu wa Jumbo Kuu la Mbeya, Mhasham Gervas Nyaisonga amewataka waumini kushikamana, kuvumoliana na kujenga maelewano katika jamii.


“ Tunapoadhimisha miaka 125 ya utume tunitahidi kuelewq kuwa tunatakiwa kustawisha umoja na utulivu miongoni mwetu, sisi ni wadhaifu tuna mapungufu tumgeukie Mungu na kuomba nguvu.” anesema Askofu Mkuu Nyaisonga.

Akizungumzia uchaguzi Mkuu ujao, Nyaisonga amewataka wakatoliki kufanya maombi maalum kwa saa 24 kuanzia Agosti 23-24 mwaka huu ili kufanikisha uchaguzi wa amani utakaowezesha upatikanaji wa viongozi bora.



MWISHO