Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts
WAZIRI KOMBO AKUTANA NA WAHARIRI, AELEZA MATUKIO MUHIMU YATAKAYOJIRI MWEZI MEI 2025
habariWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amefanya mkutano maalum na wamiliki pamoja na wahariri wa vyombo vya habari kwa lengo la kueleza mwelekeo mpya wa Wizara pamoja na matukio muhimu yatakayojiri katika mwezi Mei 2025.
Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam ambapo ajenda kuu ilikuwa ni uzinduzi wa Sera mpya ya Mambo ya Nje, sambamba na ratiba ya ziara za viongozi wa kimataifa zitakazofanyika nchini.
Akihutubia mkutano huo, Waziri Kombo amesema kuwa uzinduzi rasmi wa Sera mpya ya Mambo ya Nje utafanyika Mei 19, 2025. Amefafanua kuwa sera hiyo ni zao la maboresho ya Sera ya mwaka 2001, yaliyoanza kutekelezwa mwaka 2024, kwa lengo la kuiwezesha Tanzania kukabiliana na changamoto mpya za kisiasa, kiuchumi na kijamii katika mazingira ya ndani na ya kimataifa.
Waziri Kombo ameeleza kuwa vipaumbele vya sera hiyo ni pamoja na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika medani ya kimataifa kupitia diplomasia ya uchumi, kulinda maslahi ya taifa, na kukuza ushirikiano na mataifa pamoja na taasisi za kimataifa. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha mazingira ya ndani yatakayowezesha utekelezaji mzuri wa sera hiyo.
Katika kuelekea utekelezaji wa sera hiyo, Waziri Kombo amesema kuwa Serikali imeandaa mikakati mahsusi, ikiwemo kushirikisha kikamilifu Watanzania waishio nje ya nchi (diaspora), kutumia Kiswahili kama bidhaa ya taifa, pamoja na kujumuisha masuala ya mazingira, usawa wa kijinsia na maendeleo ya vijana katika ajenda za kidiplomasia.
Mbali na uzinduzi wa sera hiyo, Waziri Kombo ametangaza kuwa Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa viongozi wa mataifa mbalimbali katika mwezi Mei. Amebainisha kuwa Rais wa Msumbiji, Mhe. Daniel Chapo, atafanya ziara ya kitaifa kuanzia Mei 7 hadi 9, Rais wa Finland, Mhe. Alexander Stubb, anatarajiwa kuzuru nchini kwa siku tatu kuanzia tarehe 16 hadi 19 Mei, huku Rais wa Namibia naye akitarajiwa kuwasili nchini Mei 21, 2025.

MHE. CHATANDA AMPONGEZA RAIS KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI
habari
Na Mwandishi Wetu..
Mwenyekiti wa UWT- CCM Taifa, Mhe. Mary Pius Chatanda amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 25 inayotekelezwa wilayani Rufiji na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.
Mbali na kumpongeza Mhe. Rais Samia, pia amempongeza Mbunge wa Rufiji kwa kusimamia utekelezaji wake ambapo amesema miradi hiyo imesimamiwa vizuri na ina tija kubwa kwa wananchi.

"Hapa naomba niungane na watanzania wote kumpongeza Rais wetu kipenzi Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo ameifanya nchi nzima, na hapa leo Rufiji tunashuhudia kazi nzuri ambayo imetekelezwa kupitia miradi hii" amesisitiza Mhe Chatanda
Mhe Chatanda ambaye yupo kwenye ziara ya siku mbili katika jimbo la Rufiji amekagua mradi wa ujenzi wa daraja la Mbambe linalojengwa kwa urefu wa mita 81 na ujenzi wa barabara ya lami inayounganisha barabara kuu ya kilomita 3 itakayogharimu bilioni 24.1.

Mkataba wa daraja hilo ulisainiwa na Wakala wa Barabara Tanzania na Mkandarasi M/S Nyanza Road Works Ltd ya Mwanza ambapo kazi hiyo inatarajia kukamilika katika kipindi Cha miezi 6 kuanzia sasa.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa daraja hilo Mhe. Mchengerwa alifafanua kuwa mradi wa ujenzi wa daraja hilo ni moja ya mikakati ya Serikali ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii wilayani Rufiji maeneo jirani.

Rashid Salum Mkazi wa Ikwiriri amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo ambapo amesema kukamilika kwake kutakuwa msaada mkubwa kutokana na adha kubwa walihokuwa wakipata hapo awali.
Aidha, Mhe. Chatanda ameshuhudia utiaji saini wab mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji vya Mloka, Mbinju Mvuleni na Ndundutawa ambapo pia ameshuhudia zoezi la kupewa mabati 45 na Mhe. Mbunge vijana wa bodaboda wa kijiji cha Mloka ili kuezekea eneo la kuegesha bodaboda zao.
Akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ( RUWASA) Wilaya ya Rufiji Mhandisi Alkam Omari pamoja na uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na Serikali katika kuwapatia wananchi maji safi na salama, mahitaji ya maji yamezidi kuongezeka ambapo amesema mradi huu unakwenda kuwa suluhisho.

MATHIAS CANAL ASHINDA TUZO YA SAMIA KALAMU AWARDS, WAZIRI ULEGA AMPA SHAVU MBELE YA RAIS SAMIA
habariMwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa WazoHuru Media Group Limited Ndg Mathias Canal ameshinda Tuzo mbili za SAMIA KALAMU AWARDS sekta ya Ujenzi na chombo bora cha mtandaoni.
Pamoja na zawadi ya Cheti, Ngao, Tsh Milioni 10, lakini pia Mathias Canal amezawadiwa safari ya kwenda nchini Japani pamoja na kufanya kazi ya kusafiri nchi nzima kueleza kwenye vyombo vya habari mafanikio na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025.
Tuzo hizo zimetolewa leo tarehe 5 Mei 2025 katika ukumbi wa Super Dome Masaki Jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan
Tuzo hizo zimetolewa kwa wanahabari watanzania kwa lengo la kuhamasisha, kuhimiza na kukuza wigo wa uchakataji, utangazaji na uchapishaji wa maudhui ya ndani kupitia vyombo vya habari.
Tuzo hizi zitahusisha maudhui yaliyochapishwa kupitia magazeti, redio, televisheni, majukwaa ya mtandaoni pamoja na tuzo kwenda kwa vyombo vya habari. Tuzo hizi zinahusisha habari zilizochapishwa kati ya Januari 01 hadi Oktoba 26, 2024.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi Mhe Abdalah Ulega, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Innocent Bashungwa (Mb) amesema kuwa pamoja na zawadi ya Tuzo pia Waziri Ulega amempa zawadi ya kufanya kazi katika wizara hiyo hivyo akaripoti Wizarani kwa ajili ya kuanza kazi.
Aidha, utoaji wa tuzo hizi umelenga kuchochea uandishi wa makala zilizofanyiwa utafiti na uchambuzi kuhusu maendeleo ya nchi, uwajibikaji, uzalendo na kujenga chapa na taswira ya nchi.

RAIS SAMIA ASHIRIKI HAFLA YA SAMIA KALAMU AWARDS 2025 JIJINI DAR ES SALAAM
habariRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Viongozi, Wadau wa habari pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa Tuzo za Samia Kalamu Awards2025 kwa Waandishi wa Habari katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Mei, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za Samia Kalamu Awards 2025 kwa Waandishi wa Habari iliyofanyika katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Mei, 2025.

Subscribe to:
Posts (Atom)