Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

NYAMGUMA MAHAMUD AIBUKA MSHINDI HABARI ZA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

May 06, 2025 Add Comment



*📌Ni kupitia Tuzo za Uandishi wa Habari za  Samia Kalamu Awards*


*📌Wizara ya Nishati yatambua mchango wake*


📌 *Yamzawadia fedha taslimu, jiko linalotumia umeme kidogo, kompyuta mpakato na uniti za umeme za mwaka mmoja*


📌 *Mhandisi Mramba asema Tuzo ni kielelezo cha kuunga mkono juhudi za Rais Samia uhamasishaji Nishati Safi ya Kupikia*

Nyamguma Mahamud, Mwandishi wa Habari  kutoka Mlimani FM ameibuka kidedea katika Tuzo za Uandishi wa Habari za Samia Kalamu Awards 2025 kupitia kipengele cha habari za Nishati Safi ya Kupikia ambapo Wizara ya Nishati imetambua mchango wake kwa kumpa zawadi mbalimbali ili kuendelea kuhamasisha utoaji wa elimu ya Nishati Safi ya Kupikia.

Hafla ya utoaji wa Tuzo hizo imefanyika jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Dkt. Samia Suluhu Hassan.



Mohamud amekabidhiwa zawadi zake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.

Mshindi huyo amekabidhiwa fedha taslimu shilingi milioni tano, kompyuta mpakato, jiko linalotumia umeme kidogo na uniti za umeme za mwaka mzima.

"Tunatambua  masuala aliyoyaandika katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia, kwahiyo tumemzawadia pia jiko la umeme la kisasa linalotumia umeme mdogo pamoja na umeme wa kutumia nyumbani kwake kwa mwaka mmoja," amesema Mha. Mramba

Amesema Tuzo ya Nishati Safi ya Kupikia ni kielelezo cha  kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika  kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Samia Kalamu Awards  imeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwa na kaulimbiu ya "Uzalendo Ndio Ujanja'

TANROADS IMEKAMILISHA UJENZI WA KM 109.49 ZA LAMI NCHINI, UJENZI WA KM 275.51 UNAENDELEA-WAZIRI ULEGA

May 05, 2025 Add Comment
Serikali imekamilisha Ujenzi kilomita 109.49 za barabara nchini kwa kiwango cha lami huku ikiendelea na ujenzi wa Kilomita 275.51, hali kadhalika ujenzi wa madaraja matano (5) unaendelea na ujenzi wa madaraja mengine matano (5) upo katika hatua za maandalizi.

WAZIRI CHANA AZINDUA MRADI WA DOLA MILIONI 5.8 KUHIFADHI MISITU YA ASILIA

May 05, 2025 Add Comment

 



Na Mwandishi Wetu,Pwani.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), amezindua  mradi wa 'Kuimarisha Ustahimilivu wa Bioanuai ya Misitu ya Mazingira Asilia Tanzania dhidi ya Athari za Mabadiliko ya Tabianchi', wenye thamani ya Dola za Kimarekani 5.8 milioni.

 Mradi huo umefadhiliwa na Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Uzinduzi huo umefanyika leo, Mei 5, 2025, katika Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia wa Pugu–Kazimzumbwi, wilayani Kisarawe, mkoa wa Pwani, sambamba na uzinduzi wa Mkakati wa Kuokoa Ardhi ya Misitu Iliyoharibika.



Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Chana amesema mradi huo unalenga kuongeza ustahimilivu wa misitu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kuimarisha mifumo ya ulinzi, kusaidia shughuli rafiki kwa mazingira kama vile utalii, na kuimarisha mipaka, vituo vya ulinzi, pamoja na vifaa vya kukabiliana na majanga kama moto wa msituni.

Aidha, amesema mradi utasaidia jamii zinazozunguka misitu kwa kuwapatia shughuli mbadala za kiuchumi zitakazosaidia kupunguza utegemezi wa moja kwa moja kwenye misitu.

“Mradi huu wa miaka sita, kuanzia Septemba 2023 hadi 2029, unatekelezwa kwa ufadhili wa GEF na UNDP kwa gharama ya Dola za Kimarekani 5,837,010,” amesema Mhe. Chana.

Amesema mradi huo utatekelezwa katika misitu tisa ya hifadhi iliyoko kwenye mikoa mitano: Hassama Hills, Nou na Mlima Hanang (Manyara), Uzigua na Pugu–Kazimzumbwi (Pwani), Pindiro na Rondo (Lindi), Mwambesi (Ruvuma) na Essimingor (Arusha).


Waziri Chana ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi utasaidia kuimarisha uwezo wa hifadhi hizo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuongeza mapato ya Serikali kupitia TFS, kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na jamii za jirani na kujenga uthabiti wa mifumo ya ikolojia kwa kuunganisha hifadhi za mazingira asilia na maeneo mengine ya uhifadhi.

Aidha, Waziri amewapongeza wadau wa maendeleo na asasi za kiraia kwa mchango wao mkubwa katika juhudi za Serikali za kuhifadhi misitu, na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano huo kwa manufaa ya taifa na vizazi vijavyo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amesisitiza juu ya wananchi kutunza na kuhifadhi maliasili za misitu huku akitoa onyo kwa wanaokiuka taratibu za uhifadhi kuchukuliwa hatua kali.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shigeki Komatsubara  amesema mradi huo ni muhimu kwa Tanzania kutokana na athari mbambali zinazoikumba misitu ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, uchomaji moto hivyo utasaidia kuirisha maisha ya na vipato vya wananchi kwa kuacha kutegemea misitu.


Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Wizara ya Fedha, TAMISEMI, wilaya ya Kisarawe, Wizara ya Maliasili na Utalii, TFS, pamoja na wadau wa maendeleo.

MWISHO.

INEC YAWATAKA WANANCHI KUTUMIA SIKU ZILIZOBAKI KUBORESHA TAARIFA ZAO

May 05, 2025 Add Comment


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele (shati la drafti) akiwa katika kituo cha shule ya Msingi Mahela katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Katavi wakati akitembelea vituo mbalimbali vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mkoa huo jana. Kulia walio simama ni Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Mbinga Mjini, Ndg. Amina Hamisi Seif. (Picha na INEC).

 Na Mwandishi Wetu, Ruvuma


Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imewataka wananchi wa mikoa 15 inayotekeleza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mzunguko wa kwanza wa awamu ya pili kuzitumia siku chache zilizobaki katika mikoa yao kuhakikisha wanajitokeza kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao ili wasijekosa haki yao ya msingi ya kupiga Kura katika uchaguzi ujao mwaka huu.

Hayo yamesema na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele wakati akitembelea vituo mbalimbali vya uboreshaji wa Daftari hilo katika Katika halsmahauri za Mkoa wa Ruvuma.

“Nawasihi wananchi wa mikoa 15 ambayo awamu ya pili ya Uboreshaji Daftari inafanyika wandelee kujitokeza kuja kuboresha, waendelee kujiandikisha lakini pia kuwaondoa wale ambao hawastahili kuwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, tumebakiwa na siku chache zinazotakiwa kuendelea na zoezi,” alisema Jaji Mwambegele.

Jaji Mwambegele amesema zoezi la uboreshaji wa wa awamu ya pili linakwenda sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la awali la kudumu la wapiga Kura ambalo linatoa fursa kwa wananchi kukagua, kufanya marekebisho ya taarifa za wapiga kura na uwekaji wa pingamizi dhidi ya wapiga kura waliomo kwenye daftari ambao hawana sifa na litabandikwa katika vituo vyote vilivyotumika wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza.

Akizungumzia kuhusu mwenendo wa zoezi hilo kwa ujumla Jaji Mwambegele amesema zoezi linakwenda vizuri na mwitikio wa wananchi ni mzuri kwani maeneo aliyotembelea katika mikoa ya Iringa, Njombe na Ruvuma wananchi wamejitokeza vituoni kujiandikisha, kuboresha taarifa zao pamoja na kutoa taarifa za watu waliopoteza sifa za kuwepo kwenye Daftari hilo.

“Kwa ujumla wake zoezi linakwenda vizuri na wananchi wengi wamejitokeza kwaajili ya kuboresha taarifa zao, wamejitokeza pia kwaajili ya kuboresha taarifa zao na pia, wale ambao hawastahili kuwepo katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura wamefutwa,katika kila kituo nil;ichokwenda wameniambia kuhusu wale walio waandikisha, waboresha na wale waliowafuta,” alisema.

Uboreshaji wa Daftari unafanyika kwa mizunguko mitatu ambapo mzunguko wa kwanza unajumuisha mikoa 15, mzunguko wa pili utajumuisha mikoa 16 na mzunguko wa tatu utajumuisha vituo vya magereza na vyuo vya mafunzo.

Mikoa inayohusika kwenye mzunguko wa kwanza wa uboreshaji ni pamoja na Iringa, Geita, Kagera, Mara, Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Rukwa, Tabora, Katavi, Kigoma, Ruvuma, Mbeya, Njombe na Songwe ambapo zoezi hilo lilianza kutekelezwa tangu Mei 1 na linataraji kukamilika Mei 7 mwaka huu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Maafisa Waandikishaji kutoka Majimbo ya Nyasa, Ndg. Khalid Khalifa na yule wa Jimbo la Mbinga Mjini Ndg. Amina Hamisi Seif wamesema zoezi la Uboreshaji katika maeneo yao linakwenda vizuri na kuwahimiza wananchi kuendelea kujitokeza.

“Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa tumekwisha andikisha wapiga kura wapya 436 na kuboresha taarifa za wapiga kura 415 wakati wapiga kura 68 wamepoteza sifa na kufutwa katika Daftari la Kudumu, bado tuzazo siku hivyo niombe kutumia fursa hii kuwataka wananchi waendelee kujitokeza,” alisema Khalifa.

Katika awamu ya pili ya uboreshaji, wapiga kura wapya 1,396,609 wataandikishwa, wapiga kura 1,092,383 wataboresha taarifa zao na wapiga kura 148,624 watafutwa kwenye Daftari kwa kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye Daftari,” amesema Jaji Mwambegele.

Tume iliboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza kuanzia tarehe 20 Julai, 2024 na kukamilisha tarehe 25 Machi, 2025.



Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele (kulia) akiwa katika kituo cha shule ya Msingi Mahela katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Katavi wakati akitembelea vituo mbalimbali vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mkoa huo jana. Wapili Kulia ni Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Nyasa, Ndg. Khalid Khalifa. (Picha na INEC).

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele (Kushoto) akimkabidhi kadi ya Mpiga Kura Ndg. Acheni Maulid mkazi wa Mbamba Bay katika Halmashauri ya Wilaya ya nyasa aliyefika katika kituo cha Shule ya msingi Mbamba bay kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. (Picha na INEC).

HAKIELIMU YAPENDEKEZA ONGEZEKO LA TRILIONI 2.08 KATIKA BAJETI SEKTA YA ELIMU

May 05, 2025 Add Comment
NA EMMANUEL MBATILO, 

TAASISI ya HakiElimu imeishauri Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha angalau asilimia 15 ya bajeti ya taifa ya 2025/26 inatengwa kwajili ya sekta ya elimu ambapo wanatarajia ongezeko la shilingi trilioni 2.08 katika bajeti ya sekta ya elimu kutoka shilingi trilioni 6.17 ya mwaka 2024/25 hadi kufikia shilingi trilioni 8.25 mwaka wa fedha 2025/26.