Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

DKT.BITEKO AWAPONGEZA WABUNGE KWA KUWASEMEA WATANZANIA

March 24, 2025 Add Comment


📌 *Asema Serikali itaendelea kuwawezesha wazawa kushiriki miradi ya nishati*


📌*Asema sekta ya nishati imepiga hatua kubwa*


*Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati*


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewapongeza waheshimiwa wabunge kwa kuihimiza Serikali kuendelea kuwezesha wazawa kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya sekta ya nishati.


Dkt. Biteko amesema hayo leo Machi 24, 2025 wakati akijibu hoja za wabunge katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini kuhusu randama ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2025/26 kilichofanyika bungeni Dodoma.

“ Nakubaliana na wabunge kuhusu kuangalia wazawa na kuwapa nguvu ili waweze kushiriki katika miradi ya nishati, tumekuwa tukifanya hivyo lakini tutaendelea kuangalia wazawa wenye uwezo ili tufanye nao kazi. Ninawashukuru  sana waheshimiwa wabunge kwa kuwasemea Watanzania ili washiriki katika miradi,” amesema Dkt. Biteko

Ameongeza kuwa licha ya kuwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Serikali itaangalia zaidi namna ya kusaidia wazawa katika sekta ya nishati, huku akitolea mfano hatua iliyopigwa katika sekta hiyo. 

Amesema kuwa kwa sasa Serikali imeliwezesha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuwa na uwezo kuzalisha na kusambaza umeme nchini kwa kuimarisha mifumo na miundombinu mbalimbali.


“ Mwaka huu unaopita Watanzania 53,000 wamepata ajira katika sekta hii. Tumepokea pia maoni ya waheshimiwa wabunge kuhusu uwepo wa wazawa kwenye kila kampuni inayopewa kazi na kuangalia upya mfumo wa utoaji zabuni,” amesema Dkt. Biteko.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema kuwa mara baada ya kukamilisha mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere, Serikali inaanzisha miradi mipya ya kuzalisha umeme kwa kuwa mahitaji ya juu ya umeme yamekuwa yakiongezeka hadi kufikia megawati 253 mwaka 2025.

Aidha, kupitia kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dkt. Mathayo David kimejadili kuhusu randama ya bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2025/26.


WIZARA YA NISHATI YATAJA VIPAUMBELE VYA BAJETI YA MWAKA 2025/2026

March 24, 2025 Add Comment


*📌 Rukwa, Kagera, Lindi. Mtwara kuunganishwa na gridi ya Taifa.*


*📌 Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kuendelea kuhamasishwa*


*📌 Serikali kuendelea kuimarisha utendaji wa Taasisi, Mashirika  chini ya Wizara ya Nishati,*


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametaja  vipaumbele vya Wizara  ya Nishati katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 ikiwemo kuendelea kutekeleza miradi ya uzalishaji, usafirishaji,  usambazaji  umeme na kufikisha gridi ya Taifa katika Mikoa iliyosalia ya Rukwa, Kagera, Lindi na Mtwara;

Akiwasilisha vipaumbele hivyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Njshati na Madini, leo jijini Dodoma, Dkt. Biteko amesema  vipaumbele hivyo vimezingatia mpango wa Taifa wa Nishati wa mwaka 2025 hadi 2030.


“Mhe. Mwenyekiti vipaumbele hivi vimezingatia mpango wa Taifa wa Nishati wa mwaka 2025 - 2030 (National Energy Compact 2025 - 2030) utakaosaidia upatikanaji na uunganishaji wa umeme kwa wananchi, kuongeza mchango wa nishati jadidifu katika uzalishaji wa umeme na ushiriki wa Sekta Binafsi katika maendeleo ya Sekta ya Nishati ”. Amesema Dkt. Biteko

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema Serikali imewajengea wazawa uwezo mkubwa wa kutekeleza miradi ya umeme huku akitolea mfano wa ajira kwenye miradi ya umeme kufikia idadi ya  53,000.

Amesema  Dunia inahitaji nishati na mahitaji ya umeme yamekuwa yakiongezeka kwa kasi hivyo Serikali itaendelea kuongeza vyanzo vya kuzalisha umeme ili kukidhi mahitaji ya Watanzania.

Awali, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu alisema kuwa katika kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa umeme wa uhakika Wizara itaendelea kuimarisha Gridi ya Taifa (National Grid Stabilization Project) pamoja na kufanya matengenezo na ukarabati wa mitambo ya kuzalisha umeme;

“Mhe. Mwenyekiti tutandelea na usambazaji wa nishati katika Vitongoji, maeneo ya migodi, kilimo, viwanda na pampu za maji pamoja na vituo vya afya ili kuwezesha shughuli za

uzalishaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.” Aliongeza Lyatuu

Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia Lyatuu alisema Serikali itaendelea kuhamasisha na kuwezesha watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034) na mpango wa Taifa ya Nishati wa mwaka 2025 - 2030 (National Energy Compact 2025 - 2030).

Aliongeza  kuwa Serikali itaendelea na shughuli za utafutaji, uendelezaji na usambazaji wa mafuta na gesi asilia pamoja na kutekeleza miradi ya kielelezo na kimkakati ya mafuta na gesi asilia

ikiwemo Mnazi Bay Kaskazini, Eyasi - Wembere, pamoja na mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi asilia kuwa Kimiminika (Liquefied Natural Gas - LNG Project).


Mradi mwingine ni ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania (East African Crude Oil Pipeline - EACOP).


Vile vile, amesisitiza kuwa Serikali itaendela kuimarisha utendaji wa Taasisi na Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya TANESCO, REA, TPDC, PBPA, EWURA na PURA pamoja na Kampuni Tanzu ili yatoe huduma bora kwa wadau, kuimarisha mapato pamoja na tija na ufanisi katika uendeshaji;


Amesema lengo lingine ni kuongeza  kiwango cha upatikanaji wa umeme kutoka cha sasa cha asilimia 78.4 hadi kufikia asilimia 100 ifikapo mwaka 2030.


Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. David Mathayo ameipongeza Serikali kwa kuja na vipaumbele vitakavyowawezesha watanzania kuwa na nishati ya uhakika.

IAA YAJIDHATITI KUWEKEZA KWENYE MADARASA MTANDAO MWAKA 2025/2026

March 22, 2025 Add Comment
























MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka amesema IAA katika mwaka wa fedha 2025/2026 imejipanga kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni nne(4bilioni) katika teknolojia za kufundishia na kujifunzia ikiwa ni pamoja na madarasa mtandao (smart classes).


Prof. Sedoyeka ameyasema hayo wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) leo Machi 21,2025 katika Kampasi ya Arusha, ziara iliyolenga kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu ya Chuo inayoendelea.


Amesema lengo la uwekezaji ni kuboresha mazingira ya kujifunzia kuendana na kasi ya maendeleo ya TEHAMA katika kuwafikia wanafunzi wengi kwa wakati mmoja, " kupitia 'smart classes' mwalimu ataweza kufundisha akiwa katika Kampasi mojawapo Kati ya Arusha, Dar es Salaam, Babati, Dodoma na Songea na wanafunzi wakajifunza popote walipo".


Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Japhet Hasunga amesema uwekezaji utasaidia IAA kuwa Chuo mfano katika kutoa Elimu Kitaifa na kimataifa.


Ameongeza kuwa kupitia madarasa mtandao hata wanafunzi kutoka nje ya nchi wataweza kusoma na yatasaidia wanafunzi kupata Elimu katika ubora unaofanana kwa kuwa Mwalimu mmoja kutoka katika Kampasi moja ataweza kufundisha watu wengi kutoka maeneo tofauti kwa wakati mmoja.


Kwa upande wake mjumbe wa Kamati ya PAC, Mhe. Cendester Sichalwe ambaye ni mhitimu wa IAA, ametoa wito kwa wazazi na Watanzania wote kukiamini Chuo cha Uhasibu Arusha na kukifanya kuwa chaguo lao la kwanza kwa kuwa watakaposoma au kuleta watoto wao watapata Elimu Bora na inayoishi.


"Mimi nimesoma IAA kwa zaidi ya miaka saba naifahamu IAA, natoa wito kwa wanaohitaji kusoma chuo kuja IAA; Chuo hiki kina vielelezo vyote vya kumfanya mhitimu kukabili soko la ajira Kitaifa na Kimataifa; mimi nilivyomaliza Chuo ajira yangu ya kwanza ni kwenye mashirika ya Kimataifa na nimekuwa nikifanya kazi huko pia kabla sijawa mbunge", amesema Sichalwe.


Kadhalika, Mhe. Sichalwe ameongeza kuwa uboreshaji wa miundombinu inayoendelea kufanyika IAA kupitia mapato ya ndani na fedha kutoka serikali Kuu umelenga kuwafanya Watanzania kupata mazingira rafiki yatakayowawezsha kupata Elimu Bora itakayowawezesha kutoa mchango katika maendeleo ya Jamii na Taifa kwa ujumla.

BALOZI DKT. NCHIMBI AFIKA NYUMBANI KWA FAMILIA YA MAREHEMU MARY SULLE KUWAPA POLE

March 21, 2025 Add Comment

  

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na familia ya aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Bi. Mary Sulle, alipofika kuwapatia pole na kuwafariji Alhamis tarehe 20 Machi 2025. Bi Sulle aliyefariki usiku wa kuamkia tarehe 18 Machi 2025, anatarajiwa kuzikwa leo Ijumaa 21 Machi 2025, nyumbani kwao Karatu.






MNEC JUMAA ASEMA MIAKA MINNE YA RAIS DKT SAMIA IMEKUWA YA MAFANIKIO MAKUBWA , ATAJA MAMBO MAKUBWA MANNE MUHIMU

March 21, 2025 Add Comment

 

Na Gustaphu Haule, Pwani.

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi Hamoud Jumaa( MNEC), amesema kuwa miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan imekuwa na mafanikio makubwa kwa Taifa na Wananchi wake.

Jumaa amesema mafanikio hayo yametokana na sera na mikakati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imekuwa ikilenga kuongeza ushirikiano na maendeleo ya jamii kwa ujumla.

Kauli hiyo ya Jumaa imekuja ikiwa ni sehemu ya kumpongeza Rais Samia kwa kazi alizofanya katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake tangu aliporidhi kiti hicho kutoka kwa mtangulizi wake Hayyati John Pombe Magufuli (JPM) aliyefariki Machi 2021.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa (MNEC) katikati akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka (kushoto) na Kulia ni Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa.

Jumaa amesema kwa maoni yake Rais Dkt. Samia amefanikiwa kutokana na kusimamia mambo makubwa manne ambayo kimsingi yamesaidia kuleta tija na faida kwa Watanzania na Taifa nzima kiujumla.

Jumaa, ametaja jambo la kwanza kuwa ni ushirikiano katika jamii, ambapo amesema Serikali imehamasisha ushirikiano wa jamii katika maamuzi yanayohusu maendeleo ya elimu,afya na miundombinu.

Amesema jambo hilo ,limewapa Wazazi na wanajamii nafasi ya kutoa maoni na kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao bila kushurutishwa wala kulazimishwa.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa (MNEC) kulia akizungumza na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa
(kushoto).

Jumaa, amesema jambo la pili ni kuimarisha miundombinu,ambapo Rais Samia amefanikiwa katika ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya na Shule hasa katika maeneo yasiyopatikana huduma bora.

Amesema, katika suala la kuimarisha miundombinu imesaidia jamii kupata huduma bora za afya na elimu na kwamba imechangia kuboresha maisha ya kila siku ya Wananchi.

Jambo la tatu, ni kuwezesha kiuchumi,Jumaa amesema kuwa Rais Samia amekuwa na dhamira ya dhati ya kuwainua kiuchumi Wananchi wake na katika kudhihirisha hilo amerudisha mikopo isiyokuwa na riba sambamba na kuendesha programu mbalimbali za ujasiriamali.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa (MNEC) Kulia akiteta jambo na Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani Kite Mfilinge(kushoto)

Amesema kuwa,katika hilo Rais Samia ametoa fursa kwa jamii kujitegemea kiuchumi ambapo imewasaidia wazazi, Wanawake na Vijana kujenga biashara ndogondogo na kuboresha hali ya maisha.

Jumaa ametaja jambo la nne kuwa ni Kukuza Maadili na Umoja wa Jamii ambapo Rais Samia ameanzisha program za elimu ya maadili na nidhamu ambazo kwa kiasi kikubwa zimejikita katika kuimarisha uhusiano na umoja katika jamii.

Amesema suala la maadili na umoja limewasaidia wazazi na watoto kuishi katika mazingira yenye heshima , ushirikiano na jamii.

Hatahivyo,Jumaa amesema kwa ujumla juhudi hizo zinaongeza ushawishi wa Jamii katika kufanya maamuzi muhimu na kuchangia katika maendeleo endelevu huku zikisaidia kujenga jamii yenye ustawi wa kijamii na uchumi.