Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

MAENEO YA KIJAMII YAMEPEWA KIPAUMBELE KUFIKIWA NA UMEME - KAPINGA

March 18, 2025 Add Comment

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini umetoa kipaumbele kwenye maeneo yanayotoa huduma za kijamii ikiwemo Shule, Taasisi, vituo vya afya, zahanati na maeneo ya visima vya maji kwa sababu ni maeneo yanayotoa huduma kwa jamii.

Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Machi 18, 2025 katika Vijiji vya Lwangu na Welela vilivyopo katika Halmashauri ya Njombe wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kukagua miradi ya umeme vijijini pamoja na kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.

"Kipaumbele ni Taasisi kwa sababu zinatoa huduma zinazotunufaisha sisi wote, tunataka umeme ukatumike kwenye vituo vya afya, zahanati, kwenye visima vya maji lakini pia kwenye shule". Amesema Mhe. Kapinga.

Ameongeza kuwa, kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini hufanyika tathmini ili kuyabaini maeneo yanayotoa huduma za kijamii huku akibainisha hakuna maeneo yanayo rukwa.

WANANCHI NJOMBE WAIOMBA TANESCO, REA KUONGEZA KASI YA KUWAUNGANISHIA UMEME

March 18, 2025 Add Comment

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Melela Mkoani Njombe wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakikagua maendeleo ya Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini katika vijiji vya Mkoa wa Njombe tarehe 18 Machi 2025.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Mathayo Davidi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtwango mkoani Njombe wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakikagua maendeleo ya Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini katika vijiji vya Mkoa wa Njombe tarehe 18 Machi, 2025.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Khatib Kazungu akifafanua jambo kwa wananchi wa Kijiji cha Lwangu Mkoani Njombe wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakikagua maendeleo ya Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini katika vijiji vya Mkoa wa Njombe tarehe 18 Machi 2025.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wakala wa Nishati Vijijini(REA), Mhandisi Jones Olotu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lupende Mkoani Njombe wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakikagua maendeleo ya Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini katika vijiji vya Mkoa wa Njombe tarehe 18 Machi 2025.

 Hamasa ya kuunganishiwa umeme yatokana na kasi ya maendeleo katika sehemu zenye huduma ya umeme

Kapinga asema ifikapo 2030 Wananchi wote watakuwa wamefikiwa na huduma ya umeme

NJOMBE

Wananchi wa Mkoa wa Njombe ambao bado hawajafikiwa na huduma ya umeme wameiomba Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuongeza kasi ya kuwaunganishia umeme katika kaya zao ili waweze kuutumia kwa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Hayo yameelezwa kupitia Viongozi wa Vijiji vya Melela, Mtwango, Lwangu, Lupende na Melela wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyolenga kukagua maendeleo ya mradi wa usambazaji umeme vijijini katika vijiji vya Mkoa wa Njombe tarehe 18 Machi 2025.

Viongozi hao wamesema wananchi wameingia hamasa zaidi ya kuunganishiwa umeme baada ya kuona maendeleo yanazidi kuimarika katika baadhi ya Kaya ambazo tayari zimeunganishiwa umeme.

Aidha, wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita ambayo imetoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ukiwemo umeme katika maeneo yao ambapo kwa miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakiona kasi kubwa ya maendeleo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amewatoa hofu wananchi hao kwa kuwaeleza kuwa azma ya Serikali ni kuhakikisha inafikisha umeme kwa wananchi wote ifikapo 2030.

Ameeleza kuwa maendeleo katika maeneo yote hupelekwa kwa hatua kama ilivyo kwa miradi ya umeme lakini lengo la Serikali ni wananchi wote wafikiwe na huduma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mathayo David amewasisitiza wananchi kuendelea kutandaza nyaya katika nyumba zao ili miradi ya umeme uiakapowafikia waunganishwe kwa haraka.

Ameeleza kuwa, wananchi ambao hawahitaji kusuka nyaya wafike katika ofisi za TANESCO Ili wapatiwe kifaa cha umeme tayari( UMETA) kwa gharama ya Shilingi elfu 27,000 tu.

WAZIRI MAVUNDE AGAWA MITUNGI YA GESI KWA MAMALISHE ZAHANATI NA HOSPITALI JIJINI DODOMA

March 18, 2025 Add Comment

📌 *Ni sehenu ya utekekezaji wa Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia*

Waziri wa Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde leo amegawa  Mitungi ya Gesi kwa Mamalishe, Zahanati na Hospitali Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya utekelezqji wa Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Kutoka Wizara ya Nishati  tukio lilihudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia, Bw. Ngeleja Mgejwa.

FAMILIA YA MZEE KING MAJUTO YATOA MSAADA WA FUTARI KWA WATOTO YATIMA TANGA

March 18, 2025 Add Comment

>Yamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuendelea kuenzi mchango wa Mzee wao.

Na Oscar Assenga, TANGA

FAMILIA ya Marehemu Mzee King Majuto leo wametoa msaada wa futari katika kituo cha kulea Watoto Yatima cha Goodwill Foundation kilichopo mkoani Tanga ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali kuisaidi Jamii.

Hatua ya msaada huo ni sehemu ya familia hiyo kurudisha kwa jamii baada ya kupokea fedha taslimu kutoka kwa Rais Milioni 30 ikiwa ni kutambua mchango wa mzee wao katika Tasnia ya Filamu hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya kugawa msaada huo Mke wa Marehemu King Majuto,Asha Mbwana Yusuf  alisema wamekwenda kukabidhi sadaka kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo hicho ikiwa ni kuwapunguzia makali ya maisha.

“Tumeona kwenye mwezi mtukufu wa ramadhani mara nyingi katika mwezi huo heri nyingi unazozifanya mwenyezi Mungu anazipokea kwa kushirikiana na Familia tumeona tulifanyie hilo kwa pamoja kuwafikia watoto yatima”Alisema

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Wasanii wa Filamu Mkoa wa Tanga Mohamed Amri Majuto alisema waliamua kufanya hilo kutokana na kwamba huo ni mwezi mtukufu wa ramadhani na kumuenzi baba yao Mzee Amri Athumani Amri Maarufu King Majuto kwa kutoa sadaka hiyo kwa watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu.

“Hii itakuwa ni furaha kwa mzee alipo na sisi kama familia tunajisikia faraja na mioyo yao imekuwa misafi na haya mambo tumekuwa tukilifanya kila wakati na hata mwezi Agosti kila mwaka tumekuwa tukilifanya kumbumbuka mzee wetu kule kwenye malazo yake”Alisema Mohamed Amri Majuto ambaye pia ni Mtoto wa Mzee Majuto.

Awali akizungumza mtoto mwengine wa Mzee Majuto Othumani Amri alisema lengo kubwa ni kutoa shukrani za dhati Rais Samia Suluhu kuwakabidhi fedha taslimu milioni 30 nao wakaona wafanye suala la kumuenzi mzee kutoa sadaka kwenye kituo cha Watoto Yatima.

“Tunamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kumuenzi mzee wetu pamoja na kutukabidhi kiasi cha Milioni 30 na sisi wakaamua kuenzi mzee wao kwa kutoa sadaka kwenye kituo cha watoto yatima hivyo wanamshukuru kwa kumuenzi mzee wao”Alisema

Awali akizungumza ni Katibu wa Taasisi ya Nasimama na Mama Popote Alipo Raphael Kiango alisema wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu na wameona ni matunda ya moja kwa moja yanayotokana na Serikali ya awamu ya sita kwa kuthamini mchango wa wasanii ambao hawapo nao kwenye ulimwengu wa sasa.

Alisema lakini wameamua kumpa tunzo ya heshima na kumpatia kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya familia na hivyo kuleta chachu hamasa kwa wasanii jambo ambalo limepelekea familia hiyo kuamua kutoa sadaka.

“ Tunaishukuru Serikali kwa kumpatia tuzo ya heshima Mzee Wetu King Majuto na kutoa kiasi cha Fedha Milioni 30 hivyo kwetu sisi imekuwa ni faraja kubwa kuona namna jina lake linaishi na tunampongeza Rais Dkt Samia Suluhu ,Wizara ya Habari ,Utamaduni Sanaa na Michezo kuwathimini wasanii hata wale ambao wametangulia mbele za haki”Alisema

Hata hivyo kwa upande wake Mkurugenzi wa Goodwill foundation Sayyed Muhdhar alisema lengo la kuanzishwa taasisi hiyo ni kuisaidia jamiii ikilenga yatima, wazee wasiojiweza na wahitaji huku wakiishukuru familia ya Marehemu Mzee King Majuto kwa kuweza kumfanya mzee majuto kuendelea kuishi.

Alisema kwamba ujio wao umekuwa mzuri kutokana na kuendelea kuenzi aliyokuwa akiyafanya mzee wao kwa kujitolea ikiwemo kuipongeza familia yao kwa kuendelea kumuenzi kumfanya aendelee kuishi.

Mwisho.