Showing posts with label elimu. Show all posts
Showing posts with label elimu. Show all posts

MAHAFALI YA 54 UDSM : PROF. ANANGISYE AWASIHI WAHITIMU KULETA MABADILIKO NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII

October 05, 2024 Add Comment

 MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye, amewahimiza wahitimu wa chuo hicho kutokaa wanasubiri ajira za serikalini pekee, bali pia kuangalia fursa nyingine za kiuchumi kwa kutumia maarifa na ujuzi waliyojifunza.


Akizungumza katika Mahafali ya 54 ya chuo hicho, Prof. Anangisye alisema elimu inawainua wahitimu na kuongeza thamani yao katika jamii, hivyo ni muhimu kutumia maarifa hayo kutatua changamoto zinazowakabili Watanzania.

Aliwakumbusha wahitimu umuhimu wa kuwa wabunifu na kuchangia katika maendeleo ya taifa, akirejea kauli ya Mwalimu Julius Nyerere kuhusu matumizi ya rasilimali katika kuwekeza katika elimu.

Alisisitiza kuwa wazazi na wadau wanapaswa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwekeza katika elimu.

Prof. Anangisye alitoa wito kwa wahitimu kurejea ofisini kwa kuzingatia sheria na maadili ya utumishi wa umma, akisisitiza umuhimu wa kuwa na uadilifu katika kazi zao.

Alimshukuru Mkuu wa Chuo, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete, pamoja na Baraza la Chuo na wadau kwa mchango wao katika mafanikio ya mahafali haya.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Balozi Mwanaidi Maajar, aliwasihi wahitimu kuwa na busara na kuongeza bidii katika kutafuta fursa halali za kujiendeleza, huku akisisitiza umuhimu wa kujifunza kutoka kwa changamoto za maisha.






BENKI YA NMB YACHANGIA VIFAA VYENYE THAMANI YA MILIONI 60 SHULE TANO ZA MSINGI WILAYA YA MUHEZA

October 01, 2024 Add Comment




Na Oscar Assenga, Muheza


BENKI ya NMB nchini imetoa imechangia vifaa vyenye thamani ya Milioni 60 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya elimu kwa shule tano za Msingi katika wilaya ya Muheza mkoani Tanga ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali


Msaada huo ulikabidhiwa kwa Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko na Afisa Mkuu wa Udhibiti wa Benki ya NMB Doreen Joseph katika Halfa iliyofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayanu humo katika wakati Juma la Elimu uliokwenda sambamba na uzinduzi wa Kampeni ya Mtoto wa leo Samia wa Kesho.

Alivitaja vifaa hivyo ambavyo benki hiyo imechangia kuwa ni Madawati 200 kwa shule ya Msingi Kwemkamba ,Magusuru,Mdote,Ngomeni na Mwembeni ambapo kila shule itapata madawati 50 ,vifaa yengine ni vitanda 40 vya double deka na magodoro 80 kwa ajili ya shule ya Msingi Ngomeni .

Alisema pia wamekabidhi vitanda 32 na magodoro 64 kwa ajili ya msingi Masuguru ambayo vitakuwa chachu katika kuhakikisha wanatatua changamoto ambazo zilikuwepo awali katika shule hizo.

“Nikushukuru Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko pamoja na Serikali kwa kazi kubwa inayofanywa kuendelea kuleta maendeleo nchini na sisi Benki ya NMB tupo tayari kushirikiana na Serikali katika kuendeleza maendeleo”Alisema .

Aidha alisema kwamba utoaji wa vifaa hivyo ni sera ya Benki hiyo kuendelea kurudisha kwa jamii ambayo ni sehemu ya faida wanayoipata kama benki inatoka kwa wadau na jamii hivyo hiyo sehemu yao wanatakiwa kurudisha kwa jamii.

“Benki ya NMB inatambua juhudi za serikali katika kusimamia elimu kwa nguvu zote zilizowekwa ili kuboresha utoaji wa mijini na vijiji ikiwemo utoaji wa elimu bure tunaipongeza Serikali kwa hilo sisi kama wadau furaha yetu ni kuunga mkono juhudi hizo za maendeleo kuisaidia jamii yetu”Alisema

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo Naibu Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko alisema kampeni hiyo ya Mtoto wa leo ni Samia wa kesho muhimu ambayo inaonyesha walivyoamua kuwekeza kwenye msingi wa muhimu wa watoto kujiamini na hatimaye kuweza kutimiza ndoto ya kuwa viongozi bora wa baadae.

Naibu Waziri Mkuu huyo aliwataka pia wazazi na walimu kushirikiana kuwaandaa wanafunzi wao kuwa viongozi na wazazi bora kwa siku zijazo huku akieleza kwamba Serikali imewekeza katika sekta ya elimu ili kupata matokeo na maendeleo yanayoendana na uwekezaji huo.

Naye kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Zainabu Katimba alisema Serikali imejipanga kuwaandaa viongozi bora wa kesho kwa kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu na miundombinu mbalimballi ikiwemo mazingira bora ya kujifunzia.


TEA & TOTALENERGIES MARKETING LTD WAKABIDHI MADWATI 130 WILAYANI KIBITI

September 25, 2024 Add Comment

 Kampuni ya TotalEnergies Marketing Ltd kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wamekabidhi madawati 130 katika shule ya Msingi Jaribuni Mpakani na Shule ya Msingi ya Kitundu za Wilayani Kibiti Mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ushirikiano baina yao katika kuboresha miundombinu ya elimu nchini.


Hafla ya kukabidhi madawati hayo iliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo katika Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani tarehe 24 Septemba 2024.

Akizungumza katika hafla hiyo Kanali Kolombo ameahidi kuwa madawati hayo yatatunzwa vizuri kwa manufaa ya wanafunzi wa shule hiyo na kuongeza kuwa Wilaya ya Kibiti imekuwa ikinufaika na miradi kadhaa ya TEA ukiwemo wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Kitundu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd Bi. Getrude Mpangile amesema madawati hayo 130 ni sehemu ya madawati 200 yenye thamani ya Sh. Milioni 25.9 yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa shule tatu za Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.

Kufuatia msaada huyo Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani imepata madawati 65, Shule ya Msingi Kitundu madawati 65 na Shule ya Msingi Makuburi ya Jijini Dar es Salaam imepata madawati 70.

Bi. Ambangile ameeleza matumaini yake kwamba msaada huo utasaidia kuweka hamasa kwa wanafunzi kujifunza kwa bidii na hivyo kuchangia kukuza ufanisi na ufaulu wa shule zilizonufaika na madawati hayo.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa TEA, CPA Mwanahamisi Chambega amekumbusha shule zilizonufaika na msaada huo wa madawati kuyatunza vyema.

“Miongoni mwa majukumu ya TEA ni kutafuta raslimali fedha kutoka kwa wadau mbali mbali na kuzigawa katika taasisi za elimu ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia hivyo tunawakumbusha kutunza vifaa hivo”. Amesema CPA Chambega.


Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati katika Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani.
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo (Kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa TEA, CPA. Mwanahamisi Chambega katika hafla ya kukabidhi madawati katika Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani.
Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa Total Energies Marketing Tanzania Ltd Bi. Getrude Mpangile (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa TEA CPA. Mwanahamisi Chambega katika hafla ya kukabidhi madawati katika Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani wakifuatilia hafla ya kukabidhiwa madawati 


Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd Bi. Getrude Mpangile akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kitundu ambayo pia imenufaika na msaada wa madawati 
Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Bi. Zakayo Mtenduka (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa TEA, CPA. Mwanahamisi Chambega katika hafla ya kukabidhi madawati katika Shule ya Msingi Jaribu Mpakani
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo katika picha ya pamoja na viongozi waliohudhuria hafla ya kukabidhi madawati katika Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani.
 

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa TEA, CPA. Mwanahamisi Chambega akitoa salaam katika hafla ya kukabidhi madawati katika shule ya Msingi Jaribuni Mpakani.

SERIKALI YAAHIDI KUKUZA SEKTA YA UTALII KUPITIA NaPA

September 16, 2024 Add Comment

 

Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Arusha.

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesema miongoni mwa maeneo ya vipaumbele vya Wizara chini ya Mfumo wa Anwani za Makazi ni kushiriki kikamilifu katika kukuza Sekta ya Utalii nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 15 Septemba, 2024 na Bw. Mulembwa Munaku, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara hiyo, wakati akizungumza na washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Jijini Arusha.
Washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano Bw. Mulembwa Munaku (mwenye koti la Buluu Katikati) na Wataalamu wa Mfumo wa Anwani za Makazi tarehe 15 Septemba, 2024. 
Mafunzo hayo yamefanyika Katika jengo la Kituo cha Utalii Ofisi za Hifadhi ya Ngorongoro, Jijini Arusha.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari yameanza tarehe 12 Septemba, 2024 yakitarajiwa kuhitimishwa tarehe 16 Septemba, 2024, yana lengo la kuwawezesha wataalamu hao kuwa na ujuzi wa kutoa Anwani za Vivutio vya Utalii vilivyopo kwenye Hifadhi ya Ngorongoro.

“Maendeleo ya aina yeyote yanategemea sana utaalamu, hivyo wataalamu mnaopata mafunzo haya mnao wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa, adhma ya Serikali ya kukuza utalii inachochewa kupitia matumizi ya Mfumo wa NaPA”, amesema Bw. Munaku na kuongeza kuwa;
“Kupitia zoezi hili, wataalamu mfikirie namna bora ya kuimarisha, kuchochea na kuvutia watalii wa ndani (wananchi) na watalii wa nje kwa ujumla wake”.

Kwa upande wake Mratibu wa Mfumo wa Anwani za Makazi Kitaifa, Mhandisi Jampyon Mbugi, amesema hatua hiyo inalenga kuongeza wigo wa kutangaza huduma na vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ili kuvutia watalii kutembelea maeneo hayo na hivyo kuongeza pato la Taifa.

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA UBORESHAJI WA MITAALA UDSM KUKIDHI MAHITAJI YA SOKO LA AJIRA

September 12, 2024 Add Comment

 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepongeza juhudi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kuboresha mitaala yake ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira. 

Hayo yamebainishwa leo Septemba 10, 2024 Jijini Dar es  Salaam na kamati hiyo wakati ilipofanya ziara kwenye Chuo hicho kukagua utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya kiuchumi (HEET). 

Kamati hiyo ilibaini kwamba hatua hii ya kufanya mapitio ya mitaala imekuwa na mchango mkubwa katika kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Sekiboko amesema kwa muda mrefu ajira imekuwa kilio cha vijana licha ya kusoma elimu ya juu, hivyo tathmini ya aina hiyo ni muhimu ili kuhakikisha elimu inayotolewa ndiyo inahitajika kwenye soko la ajira.

"Kilichofanyika ni kizuri maana tusijifungie kwenye kutoa elimu bila kujifanyia tathmini kujua elimu inayotolewa inatatua changamoto zinazotuzunguka? Je mhitimu kwa ngazi ya chuo kikuu ana uwezo wa kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii.

“Tumefurahishwa pia na taarifa kwamba mnafanya tafiti ila tunachotaka matokeo ya tafiti hizi yawekewe wazo ili ziwe msaada kwenye jamii isiwe tafiti zinafanyika na kuishia kwenye makabati," amesema Mhe. Sekiboko.

Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian amesema tayari chuo hicho kimefanya mapitio ya mitalaa 60 kwa ngazi ya shahada ya kwanza na ya pili na iko katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kutumika.

Aidha amesema utekelezaji wa mradi wa HEET katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, unahusisha ujenzi wa majengo mawili ambayo ni bweni lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40 na kukamilisha jengo la utawala na taaluma.

Amesema jengo la utawala na taaluma litakuwa na madarasa manne yenye uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 216, ukumbi wa mikutano wenye uwezo wa kuchukua watu 150, ofisi ya wafanyakazi, na maabara tano.

Pamoja na hayo Prof. Killian amesema ujenzi wa majengo mbalimbali ya mradi ulianza Februari ,2024 na utakamilika baada ya miezi 18 na utagharimu kiasi cha Tsh. 11, 194,677,531.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Husna Juma Sekiboko akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara kutembelea utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) leo Septemba 10, 2024 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ilipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Septemba 10, 2024.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ilipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Septemba 10, 2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Husna Juma Sekiboko, (mwenye ushungi) akiongozana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian pamoja na Wajumbe wa Kamati wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Husna Juma Sekiboko, (mwenye ushungi) akiongozana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian pamoja na Wajumbe wa Kamati wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Juma Sekiboko wakikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Taaluma na Utawala unaotekelezwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Juma Sekiboko wakikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Taaluma na Utawala unaotekelezwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.
Ujenzi wa engo la Taaluma na Utawala ukiendelea katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga akizungumza jambo na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Juma Sekiboko kufanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Juma Sekiboko wakikagua mradi wa ujenzi wa bweni unaotekelezwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.