Showing posts with label elimu. Show all posts
Showing posts with label elimu. Show all posts

BILIONI 161.4 ZA RAIS DKT SAMIA ZAIWEZESHA TANGA UWASA KUTEKELEZA MIRADI 20 YA KIMKAKATI

March 22, 2024 Add Comment

MKUU wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah wa kwanza kushoto akikapata utepe kuashiria makabidhiano ya mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji Taka wilayani Muheza pamoja na kukabidhi Vyoo vilivyojengwa ikiwa ni sehemu ya Ujenzi wa Mradi huo kwa shule ya Sekondari Bonde,Shule ya Msingi Mdote na Soko la Majengo wilayani Muheza uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Kulia Diwani wa Kata na anayefuatia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani

MKUU wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo
Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shaban akizungumza kuhusu mradi huo

Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Bonde akieleza taarifa yake wakati wa makabidhiano hayo
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Bonde wakiwa kwenye halfa hiyo ya makabidhiano

Na Oscar Assenga, MUHEZA

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa ) wamesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Serikali imewawezesha ujenzi wa miradi ya kimkakati 20 ya maji safi yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 161 ambayo imekuwa chachu kubwa kuwezesha wananchi kupata huduma ya maji safi na hivyo kuondokana na changamoto walizokuwa nazo awali.

Hayo yalisemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Mhandisi Rashid Shaban wakati wamekabidhi mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji Taka wilayani Muheza pamoja na kukabidhi Vyoo vilivyojengwa ikiwa ni sehemu ya Ujenzi wa Mradi huo kwa shule ya Sekondari Bonde,Shule ya Msingi Mdote na Soko la Majengo wilayani Muheza.

Mhandidi Shaban alisema pamoja na hilo pia ipo miradi 6 ya maji taka yenye thamani ya Bilioni 4.2 ukiwemo wa ujenzi wa miundombinu ya kupokea na kuchakata majitaka wenye thamani ya Bilioni 1 ambao umetekelezwa na hivyo kusaidia kuondosha kero ambayo ilikuwa ikiwkumba wananchi.

Alisema kutokana na uwezeshwaji huo kwa sasa mamlaka hiyo inatoa huduma ya maji safi na salama kwa wastani wa asilimia 92.5 ya wakazi wa Jiji la Tang (96.1%), Pangani (70%) na Muheza (71%) ambapo miaka mitatu iliyopita kabla ya utawala wa Serikali ya awamu ya sita huduma ya maji ilikuwa inapatikana kwa wastani wa asilimia 83.2 ya wakazi hao (Tanga 89%, Muheza 33% na Pangani 60%).

Aidha alisema hivi sasa maji safi yanapatikana kwa wastani wa saa 15 kwa siku katika miji ya Muheza ambapo miaka mitatu iliyopita huduma ya maji ilikuwa inapatikana kwa wastani wa masaa matatu na wakati mwengine siku moja baada ya Juma Zima.

Akizungumzia huduma ya uondoshaji wa maji Taka, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema huduma hiyo hufanywa kupitia mtandao wa mabomba unaowahudumia wakazi wapatao 20,615 sawa na asilimia 5.2 ya wakazi Tanga Mjini, Maeneo ya Muheza, Pangani na maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Tanga ambayo hufanywa kwa kutumia mifumo mingine ya uondoshaji majitaka ikiwemo vyoo vya shimo na vyoo vya kunyonywa na magari vikishajaa.

Hata hivyo akielezea ujenzi wa vyoo na ombi la kukabidhi kwa watumiaji ,Mhandisi Rashid alisema kwamba kwa kua mradi huo unahusiana na usafi wa mazingira,Tanga Uwasa iliona ijenge aina hiyo ya vyoo ili kuonesha mfano wa vyoo bora vinavyotakiwa kujengwa katika jamii ikiwemo faida ambazo zinapatikana kupitia mradi huo.

Alisema faida ni kuwaepusha uchafuzi wa maji ya ardhini, uwepo wa huduma karibu na wananchi kupitia gari la kunyonya majitaka toka na hivyo kuondoa changamoto ya utupaji mbali na wakati mwengine katika maeneo yasiyorasmi.

“Pia kupungumza changamoto ya ufinyu wa vyoo katika shule za Msingi Mdot,Shule ya Sekondari Bonde na Soko la Majengo ambapo gharamaa nafuu kwani kutumia eneo dogo la ardhi na hudumu muda mrefu pia upatikanaji wa mbolea inayoweza kutumika kwa kilimo lakini tunaishukuru Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kuwezesha ujenzi wa mradi huu”Alisema

“Sisi Tanga Uwasa tumeona ujenzi wa vyoo umekamilika na vipo tayari kutumika tunadhani hakuna haja ya kuendelea kusubiri hadi ujenzi wa miundombinu pale Kilapula ukamilike ikiwa wanafunzi na wananchi sokoni wanauhitaji mkubwa hivyo tunakuomba ukabidhi vyoo hivi kwa uongozi wa shule ya Sekondari Bonde, Shule ya Msingi Mdote na Soko la Majengo vianze kutumika na hivyo kusaidi kupunguza changamoto iliyopo ya uhitaji wa matundu ya vyoo”Alisema

Awali akizungumza mara baada ya kupokea mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji Taka wilayani Muheza pamoja na kukabidhi Vyoo vilivyojengwa ikiwa ni sehemu ya Ujenzi wa Mradi huo kwa shule ya Sekondari Bonde, Shule ya Msingi Mdote na Soko la Majengo wilayani Muheza, Mkuu wa wilaya ya Muheza ZainabuAbdallah alisema miaka mitatu ya nyuma hali ya upatikanaji wa maji ilikuwa ni asilimia 33 lakini miaka mitatu sasa hivi himefikia 71 hiyo ni kazi kubwa anayoifanya Rais Dkt Samia Suluhu.

Katika miaka mitatu ya Rais Dkt Samia wamefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ya kikamkati 20 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 161.4 ya Maji Safi na Maji Taka miradi sita yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 4.2 ambapo hiyo ni kazi kubwa na nzuri inayofanya na Rais Samia.

Alisema wamefika katika hafla hiyo kuungana na Tanga Uwasa katika tukio hilo huku akimpongeza Waziri wa Maji Jumaa Aweso kutokana na kazi kubwa anayofanya kuhakikisha huduma ya maji kwenye mkoa wa Tanga inakuwa nzuri na Muheza wanatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa miundombinu ya maji taka wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1 ambapo kwenye mradi ho wamepata gari la maji taka, gari ya usimamizi wa mradi na wamepata matundu ya vyoo,shule ya sekondari na Msingi pamoja na Soko .

MWisho


WAZIRI JAFO AONGOZA KAMPENI YA UPANDA MITI ZAIDI YA 450 SHULE YA DAR ES SALAAM GIRLS SEC.

March 15, 2024 Add Comment

 NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV


WAZIRI wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt.Suleiman Jafo,ametoa pongezi kwa wanafunzi wa shule ya wasichana Dar es salaam Sekondari kupanda miche ya miti zaidi ya 450 katika eneo la shule hiyo iliyopo katika halmashauri ya manispaa ya Ubungo.

Kuelekea miaka 60 ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt.Selemani Jafo ameongoza zoezi la upandaji miti zaidi ya Mia tano katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Dar es Salaam.

Pongezi hizo amezitoa leo Machi 15,2024, alipotembelea shuleni hapo kuhamasisha kampeni yake ya upandaji miti ambapo amesema kila mtu anawajibu wa kupanda miti hivyo basi wameona ni vyema kushirikisha wanafunzi wote nchini kufanya zoezi hilo lidumu kuwa endelevu katika vizazi vyao.

Aidha Dkt,Jafo amewashukuru mawakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kwa juhudi zao za kuzalisha miche ya miti kwa ajili ya kupanda nchini ili kuondokana na adha ya mabadiriko ya tabia ya nchi ambayo yamepelekea kupungua kwa mvua na kuongezeka kwa kina Cha bahari.

"Tumeshuhudia dunia nzima joto linaongezeka ambapo joto hili linasababisha athari kubwa katika maisha ya wanadamu na viumbe mbalimbali lakini sehemu nyingine ukame umeshamiri,mvua ambazo hazina utaratibu zinasababisha mafuriko"Dkt,Jafo amesema

Amesema uharibifu wa mazingira umesababisha changamoto ya uchumi,umeme kukatika kutokana na ukosefu wa mvua za kutosha kwa ajili ya uzalishaji wa umeme,jambo ambalo limeibua upungufu wa uzalishaji nishati hiyo.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa katika maelezo ya nchi na ilani ya chama cha mapinduzi imeagiza kila halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kwa mwaka kwa lengo la kupanda miti zaidi ya milioni 200 katika halmashauri zote ambapo katika taasisi za serikali wanafunzi kushiriki kufanya zoezi hilo.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Jaffar Nyaigesha ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya kujenga madarasa ya shule hiyo ya wasichana.

Kampeni hiyo ya upandaji miti imefadhiliwa na Benki ya NMB ambao wamekuwa wadau wakubwa wa Uhifadhi wa mazingira nchini,ambapo wanachama wa chama Tawala (CCM),Mabarozi wa mazingira,Pamoja na Mawakala wa huduma za misitu(TFS) wamehudhuria katika tukio hilo.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiongoza wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Dar es Salaam kupanda miti zaidi ya 450 katika utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akizungumza katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti wakati alipotembelea katika shule ya Sekondari ya wasichana Dar es Salaam leo Machi 15,2024.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Jaffar Nyaigesha akizungumza katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti wakati Waziri Jafo alipotembelea katika shule ya Sekondari ya wasichana Dar es Salaam leo Machi 15,2024.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Dar es Salaam wakiwa katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti ambayo inaongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo ambapo ametembelea shule hiyo na kuongoza upandaji wa miti zaidi ya 450 leo Machi 15,2024.



Baadhi ya walimu wa shule za sekondari katika halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wakiwa katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti ambayo inaongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo ambapo ametembelea shule ya Sekondari ya Wasichana Dar es Salaam na kuongoza upandaji wa miti zaidi ya 450 kwenye shule hiyo leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akitoa cheti cha shukrani kwa baadhi ya wadau wa mazingira katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti wakati alipotembelea katika shule ya Sekondari ya wasichana Dar es Salaam leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira wakati wa utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa halmashauri ya manispaa ya Ubungo wakati wa utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule za sekondari za halmashauri ya manispaa ya Ubungo wakati wa utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana Dar es Salaam wakati wa utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti katika shule hiyo leo Machi 15,2024.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

BARRICK YAJITOSA KUTOA HAMASA NA MOTISHA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI NCHINI KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

March 15, 2024 Add Comment

 

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa, akiwa na wanafunzi wa kike waliofanya vizuri katika somo la hisabati muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi za laptop kutoka Barrick.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk. Franklin Rwezimula (kushoto) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa kwa niaba ya kampuni.
Mmoja wa wasichana waliofanya vizuri katika somo la hisabati, kutoka sekondari akipongezwa baada ya kupokea zawadi la Laptop kutoka Barrick
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari mkoani Morogoro walishiriki katika maadhimisho hayo
Wanafunzi wakishiriki kujibu maswali ya chemshabongo katika hafla hiyo.
---
Kampuni ya dhahabu ya Barrick nchini, imedhamini madhimisho ya Siku ya Hisabati Duniani ambapo kwa hapa nchini yalifanyika mkoani Morogoro kwa kuandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania ambacho kinashirikiana na Serikali kuongeza ufaulu wa masomo ya hisabati katika shule za msingi na Sekondari nchini.

Kwenye kilele cha maadhimisho hayo , Barrick ilieleza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha elimu nchini ikiwemo kufanikisha ufaulu wa masomo ya sayansi na TEHEMA mashuleni ili taifa lisibaki nyuma katika ulimwengu wa sayansi ya teknolojia

Pia imedhamiria kutoa hamasa na motisha kwa watoto wa kike watakaofanya vizuri katika masomo ya sayansi na kutoa wito kwa wasichana kujiamini na kuondoa dhana ya kwamba masomo ya sayansi ni kwa ajili ya wavulana.

Katika hafla hiyo wanafunzi wa kike watatu waliofanya vizuri katika somo la hisabati lililoandaliwa na Chama cha Hisabati nchini mwaka jana walizawadiwa na laptop za kisasa kila mmoja na kampuni ya Barrick .Wanafunzi hao wanatokea katika sekondari za Lumumba-Zanzibar,Canosa na Marian.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk.Franklin Rwezimula, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, alisema Serikali inaendeea kufanya mikakati mbalimbali kuhakikisha ufaulu wa somo la hesabu na masomo mengine ya sayansi unaongezeka na aliwapongeza wadau mbalimbali wanaounga mkono jitihada za Serikali katika kufanikisha suala hili.

RPC MANYARA AKERWA NA VITENDO VYA UKATILI, KUINGIA MTAANI KUTOA ELIMU

February 09, 2024 Add Comment

 Na John Walter -Manyara


Ukatili wa kijinsia unasalia kuwa kitendo cha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu duniani kote.

Nchini Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa raia wa kwanza kuonesha wazi kukerwa na wanaofanya vitendo hivyo viovu na kuagiza vyombo vinavyohusika kusimamia kikamilifu kuvitokomeza.

Ukifika mkoani Manyara ukatili unazungumzwa kila uchwao lakini bado wapo wasiosikia hali ambayo imemlazimu Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Manyara George Katabazi kulazimika kuingia mtaani na kwenye vijiji kuzungumza na wananchi akisisitiza kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na vitendo vingine vya uhalifu kwa kutoa taarifa kabla tukio halijatokea.

Mkoa wa Manyara ni Miongoni mwa mikoa inayotajwa kuongoza kwa matukio ya ukatili vikiwemo vipigo, ubakaji na mauaji.

Februari 6 mwaka huu majira ya asubuhi katika kijiji cha Magugu, Binti (19) mwenye ulemavu wa kutokusikia na kuongea, alibakwa na mtu mmoja anayedaiwa aliwahi kuhukumiwa jela miaka 30 mwaka 2022 kwa Kosa la kumbaka Binti huyo huyo na baadaye kuachiliwa huru baada ya kukata rufaa.

Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Magugu wilayani Babati, Katabazi amesema vitendo vya Ukatili haswa ubakaji vinavyofanyika katika kata ya Magugu na maeneo mengine ya mkoa wa Manyara sio vya kunyamaziwa kwa kuwa vinaharibu taswira ya mkoa.

Jeshi hilo limeahidi kumtafuta na kumkamata mtuhumiwa huyo ili kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria kujibu tuhuma zinazomkabili.

ZIC,WADAU WAENDESHA MAFUNZO KUHUSU BIMA YA KIISLAM KWA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

ZIC,WADAU WAENDESHA MAFUNZO KUHUSU BIMA YA KIISLAM KWA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

October 31, 2023 Add Comment


Facebook




Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo pamoja na wageni waalikwa wakati akizunduza semina ya siku moja kwawawakilishi hao iliyoendeshwa na Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) kwa kushirikiana na wadau wengine visiwani humo ikilenga  kuwajenga uelewa wajumbe hao kuelekea uanzishwaji wa huduma  mpya ya Bima ya Kiislamu ‘Takaful’. Wanaomsikiliza ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango –Zanzibar  Mhe. Dkt Saada Mkuya (wa tatu kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima Zanzibar(ZIC) Bw Arafat Haji (Kushoto) na wadau wengine.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango –Zanzibar  Mhe. Dkt Saada Mkuya akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar  pamoja na wageni waalikwa wakati wa semina ya siku moja kwa wawakilishi hao iliyoendeshwa na Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) kwa kushirikiana na wadau wengine visiwani humo ikilenga  kuwajenga uelewa wajumbe hao kuelekea uanzishwaji wa huduma  mpya ya Bima ya Kiislamu ‘Takaful’.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima Zanzibar(ZIC) Bw Arafat Haji akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na wageni waalikwa wakati wa semina ya siku moja kwa wawakilishi hao iliyoendeshwa na shirika hilo kwa kushirikiana na wadau wengine visiwani humo ikilenga  kuwajenga uelewa wajumbe hao kuelekea uanzishwaji wa huduma  mpya ya Bima ya Kiislamu ‘Takaful’.

 

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa na wadau wa Bima ya Kiislamu ‘Takaful’.

……………………………………

Na Mwandishi wetu-Zanzibar

Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) kwa kushirikiana na wadau wengine visiwani humo limeendesha mafunzo ya kujenga uwezo kwa wajumbe wa Baraza la wawakilishi Zanzibar ikiwa ni moja ya hatua muhimu kuelekea utoaji wa huduma yake mpya ya Bima ya Kiislamu ‘Takaful’.

Mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika eneo Chukwani nje kidogo ya jiji la zanzibar, yalitanguliwa na mafunzo ya siku moja kwa mawakala wa bima visiwani humo yaliyofanyika visiwani Pemba huku lengo likiwa ni kuwaandaa wadau muhimu kuelekea kuanza matumizi ya bima ya kiislaam nchini.

Akizindua mafunzo hayo Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid alisema  kuna umuhimu mkubwa wa kuleta mabadiliko katika kukuza huduma za bima ya kiislamu nchini huku akibainisha kuwa tayari nchi nyingi duniani zimeshafanya mabadiliko ya sheria za kifedha na kodi hivyo hatua hiyo itaweza  kuweka mazingira bora ya kukuza na kustawisha huduma hizo.

“Ni imani yangu kuwa mfumo huu utaenda kuleta mabadiliko makubwa katika sekta za kibima hivyo ni wajibu wa serikali kuweka mikakati imara ili kuhakikisha  wanachi walio wengi wananufaika” alisema, 

Zaidi Mh Zubeir  aliwahamasisha wajumbe wa baraza hilo kuhakikisha wanayatumia vema mafunzo hayo ili kujijengea uelewa wakutosha ili pia na wao waweze kupeleka uelewa huo kwa wananchi.

“Naamini pia kupitia uelewa huo mtaweza kuuliza maswali ya kina pamoja na kutoa maoni yenu muhimu kuhusu huduma hii ili wataalamu waweze kuyazingatia na kuyatekeleza kwa maslahi ya wananchi wetu hapa Zanzibar na taifa kwa ujumla,’’ alisisitiza.

Aidha Mh Zubeir alitoa wito kwa Mamlaka mbalimbali zinazohusika katika kufanikisha mpango huo zikiwemo taasisi za kifedha na mamlaka husika kuhakikisha zinafanya juhudi za makusudi ili kuruhusu utoaji wa huduma hiyo haraka iwezekanavyo lakini pia kwa ufanisi unaotakiwa ili iwe na tija zaidi hususani kwa wananchi wa kipato cha chini.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima Zanzibar(ZIC) Bw Arafat Haji alisema kupitia mkakati wa uendeshaji wa mafunzo hayo Shirika hilo linaamini kuwa taarifa muhimu kuhusu huduma hiyo mpya zitawafikia walengwa wote kote nchini ili waweze kuichangamkia pindi itakapowafikia.

“Ni matumaini yetu kuwa ujio wa huduma hii ya Bima ya Kiislamu yaani ‘Takaful’ itakuwa ni suluhisho sahihi la kuwavutia wananchi wengi zaidi visiwani Zanzibar na maeneo mengine ya nchi ambao kimsingi wanahitaji huduma ya Bima ila wanashindwa kutokana na imani za kidini.’’ Alisema

Alibainisha kuwa wananchi wengi wa visiwa vya zanzibar wamekua wakisuasua kuingia katika mifumo ya bima kwa kujiepusha na riba ambazo zimekuwa zikienda kinyume na silaka na dini zao.

Akitoa shukrani zake kwa niaba ya serikali na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango –Zanzibar  Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum pamoja na kuwapongeza wadau hao wakiwemo ZIC alisema semina hiyo imeendeshwa kwa kundi muhimu  kwa kuwa wajumbe hao wanawakilisha maelfu wa wananchi hatua itakayorahisisha usambazaji wa elimu hiyo.

 “Baada ya mafunzo haya sisi kama viongozi wa serikali pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi tunabaki na jukumu kubwa la kuhakikisha elimu hii haibaki miongoni mwetu bali inawafikia wananchi tunaowawakilisha huko majimboni na hicho ndio kitu kinachofuata baada ya hapa. Huduma hii ni muhimu sana kwa wananchi wetu na tutahakikisha inawafikia kama ilivyokusudiwa,’’alisisitiza.

Mbali na ZIC wadau wengine waliohusika katika utoaji wa mafunzo hayo kuhusu Bima hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ni pamoja na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ),  Kituo cha Usimamizi wa Masuala ya Huduma za Kifedha za Kiislamu na Ushauri Tanzania (CIFCA) na Benki ya Maendeleo ya Kiislamu(IsDB).