Showing posts with label afya. Show all posts
Showing posts with label afya. Show all posts

MBUNGE UMMY AUNGANA NA TAASISI YA SHITTA KUTOA SADAKA WAGONJWA BOMBO HOSPITALI KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA KUCHINJA

June 18, 2024 Add Comment





MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aungana na Umoja wa Taasisi za Kiislamu Mkoani Tanga (SHITTA) kutoa sadaka kwa wagonjwa waliolazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo) kusherehekea sikukuu ya Eid Al_Adha kwa ajili ya kuchinja.

Mbunge Ummy alisema kwamba kushiriki kwa pamoja kutoa chakula kwa wagonjwa, kwenye Hospital hiyo  ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Eid Al Adha kutawawezesha wagonjwa nao waweze kufurahia siku hiyo 

Akiwa Hospitalini hapo Mbunge Ummy alionyesha  furaha yake kutambulishwa shirikisho hilo  ambalo linaziunganisha Taasisi za dini ya kiislamu katika mkoa wa Tanga huku akiwatoa wito kwa taasisi nyengine kuona umuhimu wa kutoa sadaka kwa wahitaji ikiwemo wagonjwa.

"Kwa kweli nimefurahi sana kushirikiana na Taasisi hii,wakati mwingine mimi kama mbunge napata shida kuzungumza na taasisi moja moja ,lakini kama nataka kukutana na taasisi za kiislamu naweza kuitafuta SHITTA ambayo inaweza kuniletea taasisi zote",Alisema mbunge wa Jimbo hilo Ummy Mwalimu.

NHIF YATUMIA MAONYESHO YA 11 YA BIASHARA NA UTALII KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU VIFURUSHI VYAO

June 02, 2024 Add Comment

 




 Na Oscar Assenga, TANGA

 

MFUKO wa Taifa wa Bima  ya Afya Tanzania (NHIF) Mkoani umeshirikia maonyesho ya 11 ya Biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara ili kutoa elimu kuhusu huduma wanazotoa ikiwemo vifurushi  wanavyovitoa.

 

Banda la Mfuko huo limekuwa lililopo kwenye maonyesho hayo limekuwa ni kivutio kwa wananchi ambao wamefika kupima afya zao na kupata ushauri namna ya kuepukana na magonjwa yasiyoyakuambikizana.

 

Pia wananchi hao wamekwenda kwa ajili ya kuona namna ya kujiunga na vifurushi mbalimbali vinavyotolewa na mfuko huo ili kuweza kunufaika na matibabu bure pindi wanapougua.

KIKAO CHA KUTATHIMINI MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA CHAFANYIKA JIJINI TANGA

May 21, 2024 Add Comment





Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Imani Clemence akizungumza wakati wa kikao
 cha wadau wa huduma za waraibu (MAT) mkoani Tanga kimefanyika Jijini hapa kwa ajili ya kujadili maendeleo ya utoaji wa huduma hizo.


Mkurugenzi Mshirika wa Huduma za Jamii –Huduma za Kinga (THPS) Dkt Appolinary Bukuku akizungumza katika kikao hicho





Afisa kutoka Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Kaskazini Sara Ndaba akizungumza jambo wakati wa kikao hicho



Na Oscar Assenga, TANGA.

KIKAO cha wadau wa huduma za waraibu (MAT) mkoani Tanga kimefanyika Jijini hapa kwa ajili ya kujadili maendeleo ya utoaji wa huduma hizo.

Kikao hiki kilihudhuriwa na wawakilishi kutoka Kamati ya Usalama ya Mkoa, Timu za Menejimenti ya Afya za Mkoa na Halmashauri (R/CHMT), wawakilishi kutoka Asasi za Kiraia, wanufaika wa huduma za MAT, watoa huduma za afya, na maafisa wa Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS).

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bw. Imani Clemence alisema Serikali kushirikiana na wadau mbalimbali, wakiwemo THPS imeweka nguvu kubwa katika kuboresha huduma  za waraibu kuhakikisha wanapata huduma bora ili afya zao ziweze kuimarika na wafikie hali ambayo wanaweza kuishi maisha ya kawaida na kushiriki katika kujenga uchumi.

Bw. Clemence alisema hadi sasa waraibu 1,094 wamejiandikisha kwa ajili ya kuanza huduma mkoani hapa, lakini 683 pekee ndio wanaendelea na huduma.
“Kuna waliohitimu, waliohama, waliopotea na wengine waliokufa”, alisema Bw. Clemence.

Bw. Clemence alishukuru Shirika la THPS ambalo limetoa mchango mkubwa sana katika kutoa kuduma za MAT, matunzo na tiba kwa WAVIU na huduma za Kufua Kikuu, kupitia mradi wa Afya Hatua unaofadhiliwa na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) kupitia Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (U.S. CDC).

“Tutaendelea kuwapa ushirikino katika miradi inayoendelea kutekelezwa mkoani Tanga wakati wote mtakapokuwa  mkiitaji na niwashukuru wadau wote tunaoshirikiana nao kwenye pambano dhidi ya dawa za kulevya”Alisema

Akizungumza  katika kikao hicho, Mkurugenzi wa THPS, Dkt Appolinary Bukuku alisema Shirika la THPS litaendelea kuchangia katika juhudi za Serikali ili watanzania wote waweze kufikiwa na huduma bora za afya.

“Tunatambua kuna watu wameingia katika uraibu, lakini huko nyuma walikuwa na uwezo wa kufanya kazi kama sisi lakini kutokana na athari walizokutana nazo wameshindwa kufanya kazi na kutengwa na jamii. Huduma  hizi zinazolewa na Serikali na wadau zitawasdia kuwawezesha kurudi katika Maisha yao ya awali”, alisema

Naye kwa upande wake Afisa kutoka Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Kaskazini Sara Ndaba alisema kwamba wanalishukuru Shirika la la (THPS) kwa kuandaa kikao hicho cha wadau kwani wamekuwa wakiwasadia kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya.

Alisema katika kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali  wakiwemo viongozi wa Dini,Jeshi la Polisi,Jeshi Magereza na Wizara ya afya wote wanapambana kwenye vita dhidi ya dawa za kulevya na mkoa umethirika na dawa za kulevya.

Hata hivyo alisema kwamba uwepo wao utasaidia kukabiliana na  tatizo hilo na Tanga ikaondokana na tatizo la dawa za kulevya kwa maana hali bado sio shwari kutokana na kwamba  kituo cha MAT kinahudumia waraibu zaidi watu 683 kila siku mpaka sasa kutoka kwa Asasi za kiraia ambazo zimekuwa zikiwaibua na kuwapeleka kwenye kituo .

Wapokea huduma za MAT nao walipata fursa ya kuzungumza kuhusu maisha yao ya uraibu na jinsi huduma wanazopatiwa zinavowasaidia kurudi katika maisha ya kawaida. Hadithi zao zilikuwa ukumbusho wa umuhimu wa kuendelea kusaidia na kupanua huduma za MAT katika mkoa wa Tanga.

Ushirikiano kati ya wadau mbalimbali na juhudi za pamoja zinahitajika katika kushughulikia matumizi mabaya ya dawa na uraibu kwa ufanisi.

DOZI MOJA YA CHANJO YA HPV INATOSHA KUMKINGA MSICHANA KUPATA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

April 23, 2024 Add Comment

 Na WAF - Mwanza


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema dozi Moja ya chanjo ya HPV inatosha kumkinga msichana kupata ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi na kuwataka wazazi/walezi kuwapeleka watoto kupata chanjo hiyo.

Waziri Ummy amesema hayo leo Aprili 22, 2024 kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Dozi moja ya chanjo ya HPV kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 iliyozinguliwa katika viwanja vya Furahisha Wilayani Ilemela Mkoa wa Mwanza.

“Wataalamu wetu ambao wanatoka kwenye Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) wametuhakikishia kuwa dozi moja ya chanjo ya HPV inatosha kumkinga msichana kupata Saratani ya Mlango wa Kizazi”. Amesema Waziri Ummy

Amesema, awali dozi zilizokuwa zinatolewa mbili, ya kwanza inatolewa leo na baada ya miezi Sita inatolewa nyingine hii ilikua inapelekea mabinti wengi kutorudi kupata dozi ya pili, Sasa hivi tumeamua kutoa dozi moja ya HPV kwa kuwa inatosha kuwakinga wasichana kuja kupata maambukizi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi.

Aidha, Waziri Ummy amesema Saratani inayoongoza kuwatesa Watanzania ni Saratani ya Mlango wa Kizazi ambapo amesema katika kila wagonjwa 100 wanaougua Saratani, wagonjwa 23 ni wagonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi.

“Inafuata Saratani ya mfumo wa chakula asilimia 11, Saratani ya Matiti asilimia 10.4, Saratani ya tezi dume asilimia 8.9 kwa hiyo ukiaangalia hapo Saratani inayoongoza ni Saratani ya Mlango wa Kizazi”. Amesema Waziri Ummy

Waziri Ummy ametoa wito kwa wazazi na walezi wote nchini, kuhakikisha watoto wanapata chanjo zote wanazopaswa kupata kwa kuwa lengo kubwa la chanjo ni kuwakinga na magonjwa yakiwemo haya ya Saratani pamoja na kuwakinga na vifo vinavyoweza kuzuilika na chanjo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. Saidi Mtanda amesema watahakikisha watoto wote wenye umri wa kuanzia miaka 9-14 wanapata chanjo hiyo ili kufikia malengo.

“Kwa mwaka 2022/23 Mkoa wa Mwanza ulifanikiwa kuchanja watoto zaidi ya laki Mbili sawa na asilimia 107 kati ya walengwa waliotarajiwa kuchanjwa ni laki 191,440 wenye umri chini ya Mwaka Mmoja, tumefikia malengo na kuyavuka”. Amesema Mhe. Makilagi








VICTORIA GWARA: SHUJAA WA HEDHI SALAMA ANAYEIPIGANIA JAMII YAKE

April 18, 2024 Add Comment

Mohammed Hammie Rajab.

Hedhi salama si jambo linalozungumzwa kwa kiasi kikubwa hususani katika jamii nyingi za kitanzania, hii ni kutokana na imani za kidini, mila pamoja na tamaduni.

Licha ya kuwepo kwa kampeni na harakati nyingi zenye lengo la kuelimisha wanawake na wasichana juu ya hedhi salama hapa nchini, lakini bado kumekuwa na changamoto ya ufikaji wa elimu hiyo hasa maeneo ya vijijini.

Jitihada zinazofanywa na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya hedhi salama ni kielelezo tosha cha kuisaidia serikali pale ambapo kumekuwa na ufinyu wa ufikiwaji wa maeneo hayo kwa ajili ya kutoa elimu.

Victoria Gwera kutokea kijiji cha Mgudeni wilayani Kilombero mkoani Morogoro ni miongoni mwa wanawake waliowahi kufikiwa na elimu ya hedhi salama, mafunzo aliyoyapata kutokea shirika la CEMDO lililopo Ifakara mkoani humo.


Bi Victoria Gwera akiwa kwenye tabasamu. Moja ya picha iliyopigwa akiwa kijijini kwake Mgudeni anapoishi.

Mbali na elimu hiyo, Victoria na washiriki wengine walipatiwa pia mafunzo ya kutengeneza tauli za kike (pedi) kwa kutumia vitenge pamoja na sabuni ambazo kwa mujibu wa lengo la mafunzo hayo zingewasaidia kwenye usafi wakati wote wa hedhi.

Baada ya mafunzo hayo Victoria aliamua kufanya kitu cha kipekee kwa jamii yake ambacho mpaka sasa kinaendelea kuacha alama.

“Niliporudi kijijini baada ya kupata mafunzo, niliamua kuanza kutengeza pedi na sabuni kwa ajili ya matumuzi yangu na jamii kwa kuuza kwa bei rahisi” anasema Victoria wakati wa mazungumzo maalumu na mwandishi wa makala hii.

Anasema ilimchukua muda wa miezi miwili tu kufanyia kazi mafunzo ya utengenezaji wa pedi hizo na sabuni, kuzijaribu, kuzitumia yeye mwenyewe kwanza kabla ya kupata wazo la kuanza kusaidia wanawake na wasichana wanaokumbana na changamaoto ya gharama za pedi wakati wa hedhi.

(Bi Victoria Gwera akiwa kwenye shughili zake za utengenezaji wa tauli za kike nyumbani kwake Mgudeni.

Victoria angeweza kuyapiga teke maarifa aliyoyapata na kusingekuwa na mtu wa kumuuliza, huenda pia ilikuwa hivyo kwa washiriki wingine, lakini yeye kuna kilichomsukuma mpaka akaamua kufanya kitu cha pekee.

“Wakati nipo msichana mdogo niliwahi kupatwa na changamoto ya kukosa pedi, gharama zilikuwa kubwa kulinganisha na hali ya familia yetu, hivyo kila nikikumbuka hali hiyo huwa naumia. Sitaki wasichana na wanawake wengine hapa kijijini wapitie yale niliyowahi kupitia mimi na ndio maana nikaamua kutengeza hizi pedi na sabuni na kuuza kwa bei rahisi” anasema Victoria.

Inaelezwa kuwa moja kati ya nyenzo za msingi ili kufanikisha hedhi salama ni elimu sahihi, upatikanaji wa taulo za kike (pedi), sabuni pamoja na maji safi na salama, vitu ambavyo Victoria mbali na kuvikamilisha, pia anawasaida wanawake wenzake kukamilisha.

“Mimi nimepata mafunzo ya hedhi salama, kwa hiyo ninapokwenda kuuza hizi pedi huko maeneo ya kijijini huwa natoa na elimu pia. Inawasaidia sana wasichana wanaoingia kwenye hedhi kwa mara ya kwanza” anasisitiza Victoria.

Kwa kutumia baiskeli, Victoria husafiri zaidi ya kilomita tano kwa siku ili kuwafikia wateja wake, wengi kutokea kijiji alichopo na vijiji jirani ambavyo anaamini bado elimu ya hedhi salama haijafika kwa kiwango kikubwa. Pedi tatu akiuza kwa kiasi cha shilingi za kitanzania elfu moja.


Bi Victoria Gwera akielekea kwenye biashara yake ya kuuza tauli za kike na sabuni

Takwimu zinaonyesha kuwa nchini Tanzania wanawake Milioni 13,750,122 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 hupata hedhi kila Mwaka. Ikielezwa kuwa idadi hiyo ni kubwa na hivyo jamii ina kila sababu ya kuhakikisha kuwa kundi hilo linapata huduma bora wakati wa hedhi ikiwemo kuhakikisha uwepo wa maji, sabuni na taulo za kike ili kufanya hedhi iwe salama kwao.

Hivi karibuni Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwenye maadhimisho ya wiki ya hedhi salama duniani alitoa wito kwa jamii kuwa na uelewa kuwa hedhi sio balaa, ugonjwa wala sio laana bali ni mabadiliko ya hali ya kawaida yanayomtokea mwanamke au msichana mara baada ya kubalehe kama ishara kwenye mfumo wa maumbile yake ya uzazi.

Victoria Gwera anawakilisha wanawake wengine wengi nchini Tanzania ambao wamekuwa wakifanya jitihada za kuikomboa jamii yao na changamoto ya hedhi salama kwa kuonekana ama kutoonekana. Hivyo ni vyema serikali na wadau wengine kuenzi na kuendeleza jitihada hizi ili kuwanusuru wanawake na wasichana.

Mwisho

Mohammed Hammie Rajab
A Human Rights to Water Journalist
(Equal Water Voice To All)
Phone: +255719000010