BAKARI KIMWANGA MWENYEKITI MPYA DCPC

March 01, 2025


CHAMA Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es salaam (DCPC), kimefanya uchaguzi na kumchagua Mhariri  Mkuu wa Gazeti Machinga, Bakari Kimwanga kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa kura 68 na hapana ni nane na zilizoharibika ni tano.



Akizungumza baada ya kuchaguliwa na wanachama wa klabu hiyo  alisema anahitaji kwenda kubadilisha klabu hiyo.


Matokeo hayo, yametangazwa na  Mwenyekiti wa Kamati huru ya uchaguzi Wakili wa Kujitegemea, Raphael Awino.

Katika uchaguzi uliofanyika leo Februari 28, 2025, jijini  Dar e salaam.

Mbali na Kimwanga, klabu hiyo imemchagua  Mary Geofrey,  kuwa Makamu Mwenyekiti Kwa kura 70 za ndiyo na saba za hapana na nne zimeharibika.

Kwa upande wa wajumbe watano, waliochaguliwa ni Selemani Jongo (69), Penina Malundo (62), Andrew Msechu (67) na Khamis Miraji (59) na Veronika Mrema (69).

Uchaguzi umefanyika kwa Amani na utulivu, jambo ambalo Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Raphael Awino amelisifu kuwa la mfano. 

Naye Katibu wa Tume Huru ya uchaguzi,     Janet Jovin amepongeza pia kwa uchaguzi uliofanyika kwa Amani

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »