📌 *Inalenga kuharakisha matumizi ya Nishati Endelevu katika Ukanda wa SADC*
📌 *Dkt.Kazungu ashiriki akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati*
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya Umeme na Nishati Jadidifu, Dkt. Khatibu Kazungu ameshiriki ufunguzi wa maadhimisho ya kwanza ya Wiki ya Nishati Endelevu (Sustainable Energy Week) kwa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) inayofanyika Gaborone nchini Botswana akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko
Maadhimisho hayo yalifunguliwa rasmi na Mheshimiwa Wakili Duma G. Boko, Rais wa Jamhuri ya Botswana na kuhudhuriwa na Mawaziri na Viongozi waandamizi wa nchi za SADC na Taasisi mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya Nishati.
Wiki hiyo ya Nishati Endelevu iliyobeba Kauli Mbiu “Kuharakisha Suluhisho la Nishati Endelevu kwa Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika - SADC” imelenga kuwezesha majadiliano na kuunda ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi ili kuwezesha upatikanaji wa nishati endelevu
Mawaziri wa Masuala ya Nishati wa Jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC), Watendaji Wakuu katika sekta ya Nishati kutoka maeneo mbalimbali duniani, Watunga sera na wavumbuzi wa teknolojia mbalimbali za kisasa za nishati Endelevu wanakutana kwa lengo la kujadili, kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya kuharakisha matumizi ya nishati endelevu katika ukanda wa nchi za SADC.
Aidha wiki hiyo pia inahusisha mijadala mbalimbali na mikutano ya pembeni (Bilateral meetings)
Katika maadhimisho hayo Dkt. Kazungu ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. James Bwana, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mhandisi Innocent Luoga na Mtaalam wa Masuala ya Nishati Jadidifu Mhandisi Justine Malaba.
EmoticonEmoticon