Na Paskal Mbunga,Tanga.
MAFANIKIO na Umaarufu wa Bandari ya Tanga sasa umeongezeka zaidi baada ya Meli kubwa za Mizigo kuanza kuitumia Bandari na hivyo kuongeza idadi ya Mizigo inayopokelewa Bandarini hapo.
Baadhi ya Meli hizo ni pamoja na Annegrit na Xio hoi Tong 50 ambazo zote zimepakua mizigo Bandari ya Tanga yenye jumla ya zaidi ya Tani 2500 mingi ya mizigo hiyo ni magari makubwa yapatayo 700.
Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake mara tu baada ta kupokea meli ya Xin Hoi Tong 50 iliyobeba magari makubwa 350 na mizigo mengine, Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha alizipongeza kampuni za Meli za usafirishaji mizigo zinazotumia Bandari ya Tanga kwani zimesaidia kuzalisha nafasi za kazi Bandarini hapo .
Mrisha alitoa pongezi maalumu kwa kampuni ya SSS Sea Front serkali.tika fuko kuu la akisema imefanikisha kwa kiwango kikubwa kuongeza mapato ya serikali ambapo kiasi cha shs. Bilioni 18 ziliweza kuingizwa katika Fuko Kuu la Serikali kwa kipindi cha miezi mitatu . Aliongeza kwamba Tanga imefaidika pia kwa kuongeza nafasi za kazi bandarini. .
Katika mwaka wa 2023/2024 Bandari ya Tanga imefanikiwa kuingiza mizigo na Bidhaa zenye uzito wa Metrik tani 1,190,480 ambapo hiyo ni ongezeko kubwa la mizigo bidhaa zilizotokana na ujio wa meli ambazo katika kipindi cha mwaka 2022/2023 jumla ya Meli 197 za mizigo ya tani 83,225 zilitia nanga Bandarini ukilinganisha na meli 307 zilizotia nanga Bandarini hapo zikiwa na mizigo tani 333,370 ambapo katika mwaka wa 2023/2024 mpaka sasa”Alisema Mrisha na kuongeza kwamba mapato ya Serikali yalifikia Bilioni 18 katika kipindi cha miezi 3.
Mrisha aliitaja baadhi ya mizigo inayoingia Bandarini hapo ikiwa ni pamoja na madini ya shaba uzito wa tani 33,000, madini ya sulpher ya uzito wa tani 104,000 na mengine ya Ammonia yenye uzito wa tani 41,000..
Akizungumza mwishoni mwa mwezi uliopita, wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma za meli za kampuni hiyo ya SSS, Meneja Mkuu wa Uwakala wa Meli wa Kampuni ya Sea Front Shipping Services, Bw. Neelakandan CJ, aliihakikishia Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) na Serikali kwa jumla kwamba watafanya kazi kwa pamoja na kuhaidi kuongeza idadi ya meli zitakazopitia bandari ya Tanga,
EmoticonEmoticon