Rasmi, Hatifungani ya Kijani ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) yaorodheshwa katika Soko la Hisa la nchini Luxembourg.
Tukio hilo limeshuhudiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Eng. Mwajuma Waziri, viongozi mbalimbali wa Wizara ya Maji, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na baadhi wa wajumbe wa Menejimenti ya TangaUWASA, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, pamoja na uwakilishi kutoka CMSA na UNCDF.
Hatifungani ya Kijani ya TangaUWASA yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 53.12 ambayo imelenga kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa wananchi inakuwa ni Hatifungani ya kwanza Afrika Mashariki kusajiliwa katika soko la hisa nchini Luxembourg.
EmoticonEmoticon