DED TANGA ATANGAZA NEEMA KWA WASHINDI WA SHINDANO LA SAMIA CHALLENGE

October 27, 2024






Na Paskal Mbunga, TANGA

WASHINDI wa Shindano la Samia Challenge wametangaziwa neema mpya na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mhandisi Juma Hamsini baada ya kutangaza kuwaongezea milioni 1 kila moja kutoka kwenye Mshahara wake.

Aliyasema hayo Octoba 26 mwaka huu wakati wa kuhitimisha Shindano hilo ambalo lilifanyika kwenye ukumbi wa Samia uliopo eneo la Kange Jijini Tanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

Shindano hilo liliandaliwa na African Antri-Violence Journalist na kuhudhuriwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Tanga Japhari Kubecha, Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu, Mstahiki Meya wa Jiji hilo Abdurhaman Shillow na wadau wengine wa maendeleo.

“Niwapongeze kwa kubuni Shindano hili la Samia, huu ni ubunifu mzuri Mh. Mkuu wa wilaya niseme kwamba hao washindi nitawaongezea Sh.Milioni 1 kutoka kwenye mshahara wangu kama mchango na siku ya Alhamisi mtafika kwa DC mje mchukue”Alisema

Aidha Mkurugenzi huyo alisema kwamba huo ni mwanzo tu lakini Shindano hilo kwa mwaka 2025 litakuwa bora zaidi ili kutuwezesha kuangalia utekelezaji wa ilani kwa wilaya ya Tanga na Mkoa na wana jukumu la kuonyesha kila ambalo linatekelezwa wilaya ya Tanga.

“Niwaambieni kwamba nitafanya kila juhudi kuhakikisha vijana wanaosoma shule , kwamba shida zao muhimu kwenye familia zao nitagharamia mimi mpaka watakapomaliza shule na tutawaongezea zaidi mshindi wa kwanza laki mbili na wa pili laki moja”Alisema Mkurugenzi huyo.

Hamsini aliwafahamisha waliohudhuria hafla hiyo kwamba serikali imetenga jumla shilingi bilioni 200 kwenda katika Mfuko Maalumu kwa ajili ya Vijana , Wanawake na Walemavu ili kuwakwamua kiuchumi. Halmashauri ya Tanga imetengewa shilingi bilioni 4.5 kwa madhumuni hayo.

Shindano hilo lililoshi rikisha wadau wengi wakiwemo wanafunzi wa Sekondari lilitarajiwa kutoa washindi watatu. Mshindi wa kwanza akiondoka na shilingi laki tano, wa pili na watatu wakigawana shilingi laki mbili unusu kila mmoja. Zawadi iliyopangwa katika shindano hilo ni jumla ya shilingi milioni moja.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa wilaya ya Tanga, Mh. Japhari Kubecha alisema Wanatanga na Watanzania kwa ujumla wana haki ya kumsifu na kumpongeza Rais Samia kwa ubunifu wake katika kuleta maendeleo ambayo yanaonekana ndani na nje ya nchi.

Mbunge wa jimbo la Tanga Ummy Mwalimu alisema kasi ya maendeleo inayofanywa na Rais Samia katika Mkoa wa Tanga sio ya kutafuta kwa tochi, bali zinaonekana kwa macho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »