Kamishna
Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya
(DCEA), Aretas Lyimo akizungumza wakati wa mkutano wa wamiliki wa nyumba
za upataji nafuu (Sober houses) uliofanyika Dodoma leo Jumatano
Septemba 11,2024.

***
Watanzania
wamehimizwa kujitoa kuwekeza kwenye huduma za kuwasaidia waraibu wa
Dawa za Kulevya kwa kuanzisha nyumba za upataji nafuu ili kuokoa nguvu
kazi ya taifa iliyopotea kwenye dimbwi la matumizi ya Dawa haramu za
Kulevya.
Hayo
yamesemwa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na
Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, wakati wa mkutano wa wamiliki wa
nyumba za upataji nafuu (Sober houses) uliofanyika Dodoma leo Jumatano
Septemba 11,2024.
Lyimo amesisitiza umuhimu wa kuongeza idadi ya vituo hivyo ili kukabiliana na tatizo la uraibu wa dawa za kulevya nchini.
"Tunahitaji
Sobar houses zaidi, hasa katika maeneo ambayo huduma hii haipatikani
kwa urahisi. Idadi ya wateja wa dawa za kulevya nchini ni kubwa kuliko
uwezo wa vituo vilivyopo sasa hivi", amesema
Kamishna
Jenerali Lyimo amewataka wamiliki wa nyumba za upataji nafuu
(Soberhouses) kuhamasisha wenzao kufungua vituo vipya, akibainisha kuwa
kila mtanzania ana nafasi ya kuchangia katika juhudi za kupambana na
uraibu wa dawa za kulevya
"Kufungua
Soberhouse sio lazima uwe umewahi kuwa mtumiaji wa dawa za kulevya.
Muhimu ni kufuata taratibu zilizowekwa na serikali", ameongeza.
Kwa
upande wao, wamiliki wa nyumba za upataji nafuu wameeleza changamoto
mbalimbali wanazokabiliana nazo, ikiwemo ukosefu wa utambuzi na
rasilimali za kutosha.
Mwenyekiti
wa mtandao wa wamiliki wa nyumba za upataji nafuu Hamisi Shuwira,
ameomba serikali kutoa vitambulisho vya utambuzi kwa wamiliki wa Sober
houses ili kurahisisha kazi yao ya kuwasaidia wateja.
Katibu
wa mtandao huo, Saidi Bandawe, amesema ni muhimu kwa wamiliki wa Sober
houses kufuata taratibu zilizowekwa na kutoa taarifa za mara kwa mara.
Ameongeza kuwa kupambana na uraibu wa dawa za kulevya ni jukumu la kila Mtanzania, si serikali pekee.
Kamishna
Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya
(DCEA), Aretas Lyimo akizungumza wakati wa mkutano wa wamiliki wa nyumba
za upataji nafuu (Sober houses) uliofanyika Dodoma leo Jumatano
Septemba 11,2024.
EmoticonEmoticon