Mshindi wa Milioni 10 Ukonga apokea chake

April 26, 2017
Ofisa wa benki ya NMB Makao Makuu jijini Dar es Salaam kushoto, akimkabidhi moja ya karatasi muhimu baada ya kufanikiwa kumfungulia akaunti mshindi wa Biko, Ijue Nguvu ya Buku, Nicholaus Mlasu aliyeibuka na ushindi wa Bahati Nasibu ya Biko mwishoni mwa wiki. Makabidhiano ya fedha za ushindi huo yalifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven. Picha zote na Mpiga picha Wetu.

Milioni 10 za Biko ‘Nguvu ya Buku’ zamfikia Nicholaus Mlasu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ZAWADI ya juu ya Sh Milioni 10 inayotolewa na Bahati Nasibu ya Biko, Ijue Nguvu ya Buku imetolewa jana na kukabidhiwa mshindi Nicholaus Mlasu, mkazi wa Ukonga Mombasa, Manispaa ya Ilala, huku akipokea fedha zake Makao Makuu ya Benki ya NMB, jijini Dar es Salaam jana.

Fedha za mshindi huyo ziliingizwa moja kwa moja kwenye akaunti yake iliyofunguliwa kwenye benki hiyo kwa ajili ya kijana huyo kujipanga vizuri kabla ya kuanza kuzitumia fedha hizo kwa maendeleo yake.
Meneja Masoko wa Biko Tanzania waendeshaji wa Bahati Nasibu kwa njia ya ujumbe wa maneno kwenye simu za mikononi, Goodhope Heaven kulia akizungumza jambo wakati wa kumfungulia akaunti mshindi wao wa Sh Milioni 10 na kumkabidhi fedha hizo jana Makao Makuu ya benki ya NMB, jijini Dar es Salaam. Katikati ni mshindi huyo Nicholaus Mlasu akifuatiwa na Ofisa wa NMB Makao Makuu.

Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema kwamba mbali na kutoa fedha hizo kila mwisho wa wiki, pia wanaendelea kutoa pesa za papo kwa hapo ambapo ongezeko la washiriki ni kubwa.

Alisema wale wanaoshinda papo hapo fedha kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja hupokea kwenye simu zao wanazotumia ambazo ni Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money, ikiwa ni baada ya kuingia kwenye kipengele cha lipa bili, kuingiza namba ya kampuni 505050 na kuingiza namba ya kumbukumbu 2456.
Meneja Masoko wa Mchezo wa Bahati Nasibu ya Biko, Ijue Nguvu ya Buku, Goodhope Heaven kulia akimkabidhi Sh Milioni 10 mshindi wao wa wiki Nicholaus Mlasu, Jijini Dar es Salaam jana. Makabidhiano hayo yalifanyika Makao Makuu ya benki ya NMB ambapo pia benki hiyo ilimfungulia akaunti ya kuhifadhi fedha zake alizokabidhiwa na Biko.
Mshindi wa Sh Milioni wa Bahati Nasibu ya Biko kutoka Ukonga Mombasa, jijini Dar es Salaam, Nicholaus Mlasu, akifurahia burungutu lake baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam jana.
Nicholaus Mlasu akifurahia pesa zake Sh Milioni 10.
“Kwa wiki mbili tumeshalipa Zaidi ya Sh Milioni 50 kwa Watanzania wanaoishiriki bahati nasibu yetu ya Ijue Nguvu ya Buku ambapo wiki iliyopita pia tulimkabidhi mshindi wetu wa Sh Milioni 10, Christopher Mgaya na leo tumemkabidhi bwana Mlasu fedha zake.

“Biko tunasema kila mtu anaweza kushinda kwa kuhakikisha kwamba anacheza mara nyingi Zaidi ili ashinde zawadi za papo kwa hapo pamoja na kujiwekea nafasi nzuri ya kuibuka na Sh Milioni 10 katika droo kubwa ya wiki inayochezeshwa kila mwisho wa wiki jijini Dar es Salaam sambamba na kuwapa ushauri wa kitaalam wale wanaoshinda fedha hizi ili wazitumie vizuri na kuboresha uchumi wao kwa kutumia vyema fedha za ushindi wa Biko,” Alisema.

Naye Mlasu alisema kwamba licha ya kushiriki bahati nasibu za kila aina, lakini mchezo wa Biko umemkosha Zaidi kwa sababu hauna mlolongo mrefu na zawadi zake zikiwa ni za haraka, jambo linaloweza kuwanufaisha washiriki wake, hivyo ni wakati wa kila Mtanzania kucheza Biko.

“Nimefurahishwa zaidi jinsi Biko inavyochezeshwa na ndio maana nilipo pokea simu ya Kajala Masanja anayechezesha droo kubwa ya wiki nilianza kuhisi huenda bahati imeniangukia ukizingatia kwamba kwa jinsi nilivyokuwa nacheza Biko niliamini kuna siku nitapata ushindi,” Alisema Mlasu.

Bahati Nasibu ya Biko inaendeshwa kwa mtindo wa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu za mikononi kwa kufanya miamala ya kifedha kuanzia Sh 1000, huku kila Sh 1000 ikiwa na nafasi mbili ikiwamo ya ushindi wa papo kwa hapo sambamba na kuingia kwenye droo kubwa ya wiki ya kutafutwa mtu mmoja wa kushinda Sh Milioni 10 ambapo tayari Mgaya na Mlasu wamekabidhiwa fedha zao kwa ajili ya kuzitumia kwa manufaa yao.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »