Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akifananua jambo kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari Kanda ya Ziwa.
Mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku mbili Jijini Mwanza kuanzia hii leo, yamelenga kuwajengea uelewa wanahabari juu ya Sheria Mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na Kanuni zake za mwaka 2017 na yamewahusisha wanahabari kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Mara na Simiyu.
Sengiyumva amebainisha kwamba mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wanahabari katika kutimiza vyema majukumu yao bila kukinzana na sheria za habari na hata haki kuhusu uhuru wa kujieleza pamoja na vyombo vya habari.
Washiriki wa mafunzo hayo yanayofadhiliwa na Taasisi ya Friedrick Ebert Stiftung (FES) Tanzania, wamebainisha kwamba elimu waliyoipata itawasaidia katika utendaji wa majukumu yao kwani wengi wao walikuwa wakitatizwa na sheria mpya ya huduma za habari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2017.
#BMGHabari
Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Jesse Kwayu, akiwasilisha mada kuhusu nafasi ya vyombo vya habari kwenye michakato mbalimbali ya sheria nchini ikiwemo sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016
Mwakilishi wa Metro Fm Mwanza, Alphonce Kapela, akichangia mada wakati wa mafunzo hayo
Mwakilishi wa gazeti Majira mkoani Mwanza, Judith Ndibalema, akichangia mada kwenye mafunzo hayo
Washiriki wamefurahishwa na mafunzo hayo yanayofadhiliwa na Taasisi ya Friedrick Ebert Stiftung (FES) Tanzania na kubainisha kwamba yatawasaidia katika utendaji wa majukumu yao kwani wengi wao walikuwa wakitatizwa na sheria mpya ya huduma za habari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2017.
EmoticonEmoticon