Wafugaji
wametakiwa kufuga kwa njia za kisasa kulingana na malisho badala ya
kuwa na mifugo mingi huku wakikosa mahali pa kulishia.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate
Ole Nasha alipotembelea mnada uliopo mjini Mhunze wilayani Kishapu
mkoani Shinyanga.
Ole
Nasha alisema si vyema wafugaji kuwa na mifugo mingi wakati hakuna
rasilimali za kufugia kama nyasi ambazo katika maeneo mengi zipo chache
hivyo kushindwa kukidhi mahitaji.Alisema
pamoja na changamoto hizo Serikali kwa upande wake inaendelea na
jitihada za kutatua changamoto hizo zinazowakabili wafugaji hapa nchini.
Aidha,
Naibu waziri aliwataka wafanyabishara wa mifugo katika mnada wa Mhunze
kujenga utamaduni wa kulipa ushuru wa Serikali badala ya kukwepa.Alisema
kitengo cha kutorosha ng’ombe kukwepa kulipa ushuru wa mnada
kunaikosesha Serikali mapato hivyo kushindwa kuwapa huduma.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha (mwenye Kaunda
suti ya bluu) akikagua ng’ombe ndani ya mnada wa Mhunze alipofanya
ziara katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha akizungumza na
wananchi katika viwanja vya mnadani alipozuru mnada mji mdogo wa
mhunzewilayani Kishapu.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha (wa pili
kulia) akifurahia jambo wakati mkutano wa hadhara katika viwanja vya
mnadani. Wengine pichani kuanzia kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo, Katibu Tawala Wilaya, Shadrack
Kangese na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu,
Stephen Magoiga.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi akiwasikiliza wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo katika mnada wa Mhunze.
Sehemu
ya umati wa wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na
Uvuvi, William Tate Ole Nasha (hayupo pichani) wakati akiwahutubia
viwanja vya mnadani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akizungumza katika mkutano huo wa hadhara.
Mkuu
wa Idara ya Mifugo Wilaya ya Kishapu, Dk. Alphonce Bagambabyaki
(kushoto) akitoa maelezo kuhusu mnada huo kwa ujumbe wa Naibu Waziri wa
Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole (wa pili kulia). Wengine
pichani ni Leonard Basil kutoka Idara ya Uzalishaji na Masoko wizarani na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Stephen Magoiga (kulia).
EmoticonEmoticon