MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA 30 LA KIMATAIFA LA WANASAYANSI LILILOANDALIWA NA TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU

October 04, 2016
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
 .....................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amelalani vikali mauaji ya watafiti WAWILI wa kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian cha Arusha na dereva MMOJA waliokuwa kazi katika kijiji cha Mvumi Makulu wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo 4-Oct-2016 wakati akifungua kongamano ya 30 la Kimataifa la Wanasayansi lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais amesema kuwa tukio hilo ni baya na amewahakikishia watafiti wanaoshiriki kongamano hilo kuwa serikali itachukua hatua stahiki kwa watu  waliofanya kitendo hicho cha kinyama ili kukomesha tabia hiyo.
“Haiwezekani hata kidogo watu kufanya mauaji hayo ya kikatili na waachwe bila kuchukuliwa hatua kali za kisheria alisisitiza Makamu wa Rais”
Akizungumzia masuala ya utafiti, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na watafiti hao hivyo serikali itaendelea kutoa mchango wake wa hali na mali ili kuhakikisha watafiti hao wanafanya kazi zao kwa ufanisi unaotakiwa.
Makamu wa Rais pia amewahimiza wafadhili waendelee kusaidia watafiti hasa wanaofanya tafiti za afya nchini kwa sababu tafiti hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa namna ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
Amesema kuwa watafiti wanamchango mkubwa katika kuleta maendeleo kupitia matokeo ya tafiti zao nchini hivyo jitihada hizo ni muhimu zikaimarishwa ipasavyo.
 Kongamano hilo la 30 la Kimataifa la Wanasayansi lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu -NIMR- linajumuisha watafiti mbalimbali kutoka Ulaya,Afrika na Amerika.
Katika kongamano hilo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameshiriki katika zoezi utoaji wa tuzo kwa wanasayansi waliofanya tafiti mbalimbali za afya nchini.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Baadhi ya Washiriki kutoka sehemu mbalimbali ndani nje ya nchi wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela akizungumza mapema leo,alipokuwa akimkaribisha Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Katika kongamano hilo kauli mbiu yake ni “Uwekezaji katika tafiti zenye ubunifu ili kufikia malengo endelevu ya dunia.”. 
Dkt Mwele alieleza pia Mada zitakazojadiliwa ndani ya kongamano hilo kuwa zitajikita zaid kwenye maeneo kama vile 1. Mkakati wa kuboresha afya ya uzazi, ya mama, watoto wachanga na vijana. 2. Magonjwa sugu yasiyoambukiza na changamoto zake,3. Kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya UKIMWI, kifua kikuu na malaria,4. Usalama wa Maji, Usafi wa mazingira na usafi binafsi,5. Mkakati wa afya moja katika kudhibiti magonjwa ya milipuko,pamoja na 6. Magonjwa ya kitropiki yasiyopewa kipaumbele.


Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya chi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada zaidi ya 200 zitawasilishwa na kujadiliwa kwa siku tatu.
Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya chi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada zaidi ya 200 zitawasilishwa na kujadiliwa kwa siku tatu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya,Dkt.Hamis Kigwangala,alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo,kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),pichani kushoto ni Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela,alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo kufungua Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),pichani kati ni Naibu Waziri wa Afya,Dkt.Hamis Kigwangala.
Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya chi wakiimba wimbo wa Taifa kabla ufunguzi wa Kongamano hilo,lililoanza leo jijini Dar.
BOFYA HAPA KUSOMA HOTUBA YA MAKAMU WA RAIS KUHUSU KONGOMANO HILO BOFYA HAPA KUSOMA HOTUBA YA MKURUGENZI MKUU WA NIMR DKT MWELE MALECELE BOFYA HAPA

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »