Waziri Mizengo Pinda AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI NYUKI

October 31, 2015

1
Waziri Mizengo Pinda akizungumza wakati alipozindua  Chama cha Kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania kwenye hoteli ya Morena mjini Dodoma Oktoba 30, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuuu)
2
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiliza mfugaji na mtalaamu wa masuala ya ufugaji nyuki na usindikaji asali, Bw. David Kaizilegi Kamala (kushoto) katika maonyesho ya ufugaji nyuki na usindikaji asali yaliyotangulia uzinduzi wa Chama cha Kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania alioufanya kwenye hoteli ya Morena mjini Dodoma Oktoba 30, 2015.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa  Kikosi Kazi cha uanzishwaji wa Chama hicho na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Parseko Konne. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Celestine Gesimba na Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa.
3
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama sabuni, mafuta na vipodozi vinavyotengenezwa kwa kutumia mazo ya nyuki kaba ya kuzindua Chama cha Kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania kwenye hoteli ya Morena mjini Dodoma Oktoba 30, 2015.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »