MFAUME SAMATA KOCHA WA MAKIPA COASTAL UNION.

December 13, 2014
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
Katika kuimarisha Benchi la Ufundi  Klabu ya Coastal Union ya
Tanga,umeingia mkataba wa mwaka mmoja  na aliyekuwa kocha wa makipa wa Yanga,Mfaume Athumani Samata ili kuweza kuwanoa makipa wa kikosi hicho.

Akizungumza leo ,Ofisa Habari wa Coastal Unioon  amesema kuwa
kocha huyo anachukua mikoba ya Razack Siwa aliyewahi kuwanoa makipa wa timu hiyo kabla ya kuondoka.

Assenga amesema kuwa kocha huyo aliwahi kuzifundisha timu za soka Yanga ,Ashanti United na Timu ya Taifa ya Vijana U-20 wana matumaini makubwa sana ataimarisha safu ya walinda milango kwenye kikosi hicho ili kuweza kukipa mafanikio.

Akizungumzia mipango yake mara baada ya kutua kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyokuwa yakiendelea kwenye viwanja wa Disuza jijini Tanga,Kocha Mfaume alisema kuwa malengo yake makubwa ni kuhakikisha kikosi cha timu hiyo kinashika nafasi za juu kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.

Kocha huyo ndio aliyeiongoza timu ya Yanga kufungwa goli saba mpaka ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ilipomalizika akiwanoa makipa kama vile Mustapha Barthezi na Yaw Berko.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »