RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dokta Jakaya Mrisho
Kikwete anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi mkoani Tanga Jumapili wiki hii
ambapo ziara hiyo itakuwa kwa awamu mbili .
Mkuu wa mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu,Chiku Gallawa ameyasema
hayo leo wakati akiongeza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu ujio wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani hapa.
Gallawa amesema mapokezi hayo yatafanyika machi 23 mwaka huu
eneo la Manga mpakani mwa mikoa ya Tanga na Pwani ambapo awamu ya kwanza ya ziara hiyo itaanzia
kwenye wilaya za Handeni,Korogwe,Muheza na Tanga.
Awamu ya pili ya ziara hiyo itafanyika mwezi april 2014
ikihusisha wilaya zitakazokuwa zimebakia ambazo ni Kilindi,Lushoto,Pangani na
Mkinga ambapo tarehe yake itajulikana baada ya kumalizika awamu ya kwanza.
Akiwa mkoani hapa ,Rais Kikwete atazindua miradi mbalimbali
ya maendeleo ,kuweka mawe ya msingi,kusikiliza kero za wananchi na kupokea
taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za maendeleo pamoja na kuzungumza
na wananchi ikiwemo viongozi.
Mkuu huyo wa mkoa ametaja thamani ya miradi ya awamu ya
kwanza itakuwa ni Tsh bilioni 194.3kwenye wilaya nne ambazo atazitembelea
wakati wa ziara yake akiwa mkoani hapa.
Aidha aliwataka wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani hapa ambapo mh.Rais Kikwete atapita wajitokeze kwa wingi ili kuweza kumlaki kiongozi huyo.
EmoticonEmoticon