KAMATI YA UCHUMI NA FEDHA YA HALMASHAURI YA MJI KOROGWE, TANGA YAPITISHA MPANGO WA TIBA KWA KADI (TIKA)
Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji
Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera
akiendesha kikao cha Kamati ya Uchumi na Fedha cha Halmashauri ya Mji
kujadili mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii
(CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi
(TIKA). Kikao hicho cha tatu kimefanyika leo Machi 27, 2014 katika
ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Makamu Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga, Mheshimiwa
Francis Komba (kushoto), anayefuatia ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya
mji Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale (kulia) na Meneja wa Bima ya Afya –
Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).
Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa
Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto) akieleza umuhimu wa matumizi ya
Tiba kwa Kadi (TIKA) kikao cha Kamati ya Uchumi na Fedha cha Halmashauri
ya Mji kujadili mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya
ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa
Kadi (TIKA). Kikao hicho cha tatu kimefanyika leo Machi 27, 2014 katika
ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Mganga Mkuu wa
Halmashauri ya mji Korogwe, Dokata Jerry Mwakanyamale (kulia),
Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya
Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga, Mheshimiwa Francis Komba.
Wajumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha ya Halmashauri ya Mji Korogwe, Tanga wajadiliana jambo wakati wa kikao.
Diwani wa Kata ya Kwamdolwa, Mheshimiwa Hillary Ngonyani akijadili jambo.
Mchumi wa Halmashauri ya Mji
Korogwe, Bw. Kikonge Jeremiah akitoa tathimini zake juu ya matumizi ya
Tiba Kwa Kadi (TIKA) kwa wananchi wa halmashauri yao.
Diwani wa Kata ya Ngombezi
ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi,
Mheshimiwa Omari Chafesi akitoa mwongozo na mtazamo wake katika mchakato
wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda
katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA).
Mwanasheria wa Halmashauri ya
Mji Korogwe, Rabeca Balisidya (wa kwanza kulia) kitoa ufafanuzi wa
vifungo vya sheria katika mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko
wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa
Tiba kwa Kadi (TIKA). Pembeni yake ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji
Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji
Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera.
Afisa Muuguzi Kitengo Cha Afya
ya Akili, Ayubu Mwakalila nae hakuwa nyuma kutoa mtazamo wake juu ya
mada iliyokuwa ikijadiliwa. Picha zoe na Cathbert Kajuna wa Kajunason
Blog.
EmoticonEmoticon