Na Oscar Assenga, Tanga.
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umesema umepania
kuibuka na ushindi kwenye mechi yao na Yanga ambayo inayotarajiwa kuchezwa Mei mosi mwaka huu katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana,Mwenyekiti wa timu hiyo,Hemed Aurora “Mpiganaji”alisema
wanaamini kuwa mechi hiyo wapinzani wao wataingia uwanjani hapo wakiwa
wamebeteka kutokana na kuwa tayari walishatangazwa kuwa mabingwa hivyo watacheza
bila umakini mkubwa.
Aurora alisema licha
ya haya wao watacheza kwa tahadhari kubwa ikiwemo kufa na kupona ili kuweza
kupata matokeo mazuri na sio kufungwa ili kuweza kutimiza malengo yao walijiwekea
ya kumaliza ligi wakiwa katika nafasi tano za juu kwenye msimamo.
Alisema licha ya majeruhi kuonekana kuiletea wakati mgumu
timu hiyo lakini wao watatumia wachezaji waliopo kwenye mechi zilizo salia
pamoja na kuangalia namna nzuri wachezaji ambao watawasajili msimu unaokuja
wasije wakawa kama msimu huu kutokana na wachezaji wengi kuwa na majeruhi.
Aidha alieleza mikakati yao ni kuhakikisha mechi zao mbili
zilizosalia wanapambana vilivyo ili kuweza kupata pointi sita muhimu ambazo
zitaweza kuwasaidia kukaa kwenye nafasi za juu.
“Tunakwenda kucheza
na Yanga kwa hamasa kubwa ya kushinda kwani Yanga tiyari wameshachukua ubingwa
na nadhani hawatacheza kwa hari hivyo watatumia nafasi hiyo kuibamiza timu hiyo
“Alisema Aurora.
Aidha aliwataka mashabiki wa soka mkoani hapa kujitokeza kwa
wingi ili kuweza kuiunga mkono timu hiyo hasa kwenye mechi hiyo kwani
kujitokeza kwao itasaidia kuipa hamasa timu hiyo kushinda au kupata matokeo
mazuri.
Mwisho.
EmoticonEmoticon