TPDC YANG'ARA KATIKA MAONESHO YA 49 YA SABASABA, YASHINDA TUZO YA MAZINGIRA

July 07, 2025 Add Comment
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeibuka mshindi katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, maarufu kama Sabasaba, baada ya kutuzwa kwa mchango wake mkubwa katika kulinda mazingira kupitia matumizi ya nishati safi.

REA YAJIZATITI KUFIKISHA LENGO LA TAIFA KWENYE NISHATI SAFI YA KUPIKIA

July 07, 2025 Add Comment
-Mkurugenzi Mkuu REA abainisha hatua zinazochukuliwa

PROF.NAGU AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA HUDUMA ZA AFYA KWA MIKOA HALMASHAURI ZOTE TANZANIA BARA

July 07, 2025 Add Comment


Na OR- TAMISEMI 


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI ( Afya) Prof. Tumaini Nagu amefunga rasmi mkutano wa mwaka wa tathimini ya utekelezaji wa huduma za Afya na usafi wa mazingira kwa mikoa na halmashauri  zote, uliokuwa ukifanyika jijini Mwanza



Mkutano huo ulioanza Julai 2, yamehitimiswa Leo julai 5, 2025 katika ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza, ambapo mkutano huo ulikuwa na lengo la  kutoa fursa ya kutathimini hali ya utoaji wa huduma afya na Usafi wa Mazingira,  kubainisha maeneo yaliyofanya vizuri, maeneo yenye changamoto na sehemu zinazohitaji ubunifu kwa lengo la la kuboresha huduma na kuikinga jamii.


Aidha, Prof. Nagu amewataka washiriki wote kutumia mkutano huo, na  kuutendea haki kwa kutoa taarifa kamili na Sahihi kwa jamii Ili kuweza kupunguza magonjwa ya mlipuko, huku akiwataka kuweka kipaumbele na kusemea maeneo yenye changamoto ili yaweze kupatiwa ufumbuzi mapema.


“ Mkutano huo wa siku nne naimani tutatumia tuliyojifunza  na, tuendelee kuhimizana na kutoa taarifa kwa wakati Ili kudhibiti magonjwa mlipuko yasiendelee”. Amesema Nagu.


Hata hivyo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba ameongeza mkutano huo kufanyika Mwanza, ametumia jukwaa hilo kuomba waganga wakuu pia kushiriki katika vikao vingine vijavyo kwa lengo la kushirikana na maafisa hao, huku akiwataka kwenda kusambaza kile walichojifunza kwa maana afua tiba ni muhimu Ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili jamii.


“Naaminii tukiendelea kufanya kazi kwa pamoja tutatoka wote katika afua za Afya na usafi wa mazingira”. Ameeleza Dkt. Jesca.



Kwa upande wake, mratibu mkuu wa mkutano wa mwaka wa tathimini ya utekelezaji wa huduma za afya na usafi wa mazingira katika mikoa na halmashauri Tanzania Bara, Seleman Yondu amewataka Washiriki na kuwasihi suala la kuzingatia na kufuata sheria na taratibuu za katika kutimiza wajibu wao. Aidha , amewaasa kuzingatia kufanya kazi kwa bidii, weledi na kuzingatia ubunifu unaoleta utendaji unaoleta matokeo.


Mkutano huo mwenye lengo la kuwapa kupitia utekelezaji, kubadilishana ujuzi na uzoefu miongoni mwa Maafisa Afya ngazi ya Mkoa na Halmashauri. Mkutano huo ulikuwa na kauli mbiu “utekelezaji wa afua za Afya na usafi wa mazingira ni msingi wa kinga endelevu dhidi ya magonjwa na Ustawi wa Jamii”.