OCTOBA KURA ZOTE KWA RAIS DKT SAMIA- UMMY MWALIMU

June 17, 2025 Add Comment


Na Mwandishi Wetu, TANGA


Kazi nzuri na miradi tele ya maendeleo iliyotekelezwa katika Jimbo la Tanga Mjini imetengeneza deni kwa wananchi wa Tanga Mjini dhidi ya Rais Dk. Samia Suluhu ambaye pia ni Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba, 2025.


Hayo yameelezwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini (CCM), Ummy Mwalimu, Juni 16, 2025, alipokuwa akitoa hotuba fupi kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Tanga Mjini katika Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Tanga. Katika hotuba yake, Ummy Mwalimu amesema Jimbo la Tanga Mjini limepata miradi mingi na mikubwa ya maendeleo ambayo imetatua kero za wananchi. 


Kwa msingi huo, Ummy Mwalimu amemuhakikishia Rais Dk. Samia kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu, asiwe na wasiwasi wa kura kwani wananchi wa Tanga Mjini watampa asante yao kwa njia ya kumpigia kura nyingi za kishindo ili aendelee kukaa Ikulu awatumikie Watanzania.


"Kwa kazi nzuri zilizofanyika, sisi watu wa Tanga kwakweli hatuna deni na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, na Oktoba 2025, watu wa Tanga tutamlipa Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kumrejesha Ikulu," amesema Ummy Mwalimu.


Mwenge wa Uhuru wilayani Tanga umezindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikijumuisha miradi ya afya, maji, elimu, viwanda na utawala ambapo wananchi wamepongeza miradi hiyo iliyozinduliwa kwani imegusa ustawi na maendeleo yao.

WIZARA YA NISHATI KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA DODOMA

June 17, 2025 Add Comment

Matukio mbalimbali wakati Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Nishati, Ziana Mlawa alipotembelea Banda la Wizara ya Nishati na Taasisi zake katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma

#NishatiTupoKazini

SERIKALI MKOA WA KILIMANJARO KUENDELEA KUPIGA UKATILI DHIDI YA WATOTO

June 17, 2025 Add Comment

 



Na Ashrack Miraji 

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw.Kiseo Nzowa  ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto.

Bw. Nzowa alitoa kauli hiyo leo Juni 16,2025 wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Manispaa ya Moshi, ambapo aliwataka wazazi na walezi kutoa taarifa za matukio ya ukatili dhidi ya watoto mara yanapotokea ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa wakati.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa, Bi. Pili Bayo, alisema kuwa Serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali imekuwa mstari wa mbele katika kusimamia haki za watoto na kutoa elimu ya kupambana na ukatili katika jamii.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Mkoa wa Kilimanjaro, Ndg. Baraka Mduma, alishukuru Serikali na wadau wa maendeleo kwa kuanzisha mikakati madhubuti ya ulinzi wa mtoto, ikiwemo uundwaji wa mabaraza ya watoto katika ngazi ya mkoa na halmashauri.

Aidha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika hufanyika kila mwaka tarehe 16 Juni, kwa lengo la kuhamasisha jamii kulinda na kutetea haki za watoto barani Afrika.







 

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU AIPONGEZA TANGA UWASA KWA MATUMIZI YA MITA ZA MALIPO KABLA

June 17, 2025 Add Comment

 





Na Oscar Assenga,TANGA

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) imepongezwa kwa kiongozi wa mbio wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ismail Ali Ussi kwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dkt Samia Suluhu la ufungaji wa mita za maji za malipo kabla kwa wananchi lengo likiwa kuboresha utoaji wa huduma

Pongezi hizo zimetolewa leo na Kiongozi wa Mbio mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa Ufungaji wa Dira za Malipo kabla katika eneo la Mwakidila kata ya Tangasisi Jijini Tanga  baada ya kupokea taarifa ya mradi na  kujionea hali ya halisi ya utekelezaji wake.

Alisema kwamba amewapongeza kutokana na kwamba mamlaka hiyo kuwa wasikivu na kutekeleza agizo la MRais kwa  mradi huo wa kimkakati unaoenda kuondosha changamoto ya muda mrefu ambayo walikuwa wakiipata wananchi ya malalamiko ya bili za maji.

Alisema kwamba mfumo huo sasa unaenda kuondosha lawama kwa viongozi  kwani wananchi wanaenda kupata maji kulingana na uwezo wao hivyo kutokana na hilo wamehaidi kwenda kuwa mabalozi waziri kwa kuwasemea juu ya usimamizi wao mzuri wa mfumo huo kwa sababu unaenda kuwasaidia wananchi hivyo tunawashukuru na kuwapongeza sana kwa kazi hii nzuri.

Awali akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Mradi huu kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025,Meneja wa Ankara na Makusanyo wa Tanga Uwasa Francis Barabara alisema kwamba mradi huo ulianza kutekelezwa mwezi Julai mwaka jana  na  una thamani ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 1.87 na unatekelezwa kwa fedha za Serikali Kuu kupitia programu ya IFF-OBA na Mfuko wa Maji wa Taifa. 


Francis alisema kwamba utekelezaji wa mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 55.05 kwa ufungaji wa dira 2,202 kati ya dira 4,000.

Aidha alisema utekelezaji wa mradi huu utaongeza Ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na kupunguza madeni ya wateja, udhibiti wa upotevu wa maji, uimarishaji wa matumizi sahihi ya maji kwa wateja na hivyo kupunguza malalamiko ya bili za maji.

 

Akizungumza wakati mara baada ya Mwenge wa Uhuru kukagua na kutembelea mradi huo,Mwenyekiti  wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo alisema maboresho kupitia mradi wa hati fungani ambao upo kwenye hatua ya utekelezaji una thamani ya Sh.Bilioni 53.

 

Alisema kwamba katika mradi huo wamedhamiria kuboresha miundombiniu kwenye chanzo cha maji bwawa la mabayani ambalo lilijengwa muda mrefu 1978 hivyo kutokufanyiwa ukarabati hivyo wameona walifanyie ukarabati ili liweze kuendana na uhitaji wa maji kwenye mji wa Tanga,Pangani na Mkinga.

 

Aliongeza kwamba hivyo wanarekebisha mtambo kwenye bwawa na katika pampu ambazo zinapeleka maji kwenye mtambo wa kutibu maji  sehemu hiyo ikiwemo kurekebisha kuweka mabomba mapya na kutoka eneo hilo kupelekea mjini kuna bomba kubwa linalazwa .

 

Mwenyekiti huyo alisema kwamba hatua nyengine ni kusambaza maji kwenye mji wa Tanga na mabomba yaliyopo ni ya zamani yamechakaa  na kama watafanikiwa presha itakuwa kubwa na mabomba ya zamani yanashindwa kuhimili na watarekebisha ili kuweza kuhimili na mradi huo mpaka Octaba mwaka huu utakuwa wamemaliza marekebishi na utaanza kufanya kazi.

Akizungumza mita za Luku, Dkt Fungo alisema kwamba matarajio yao ni kuhakikisha wananchi wanaunganishwa na nazo kwa wale ambao hawajafikiwa ambapo alisema kabla ya kufunga mita za luku kulikuwa na malalamiki sana kwa wateja kuona kama wanabambikiziwa bili kitu ambacho hakiwezekana.

Alisema lakini kwa kuondoa shida hiyo kwa wananchi na Rais alitoa maelekezo kuona njia bora ya kuweza kurekebisha dosari zilizojitokeza na hivyo njia bora wakaona  ni mita za luku na walifanya majaribio kwa miaka miwili na sasa wamefikia mita ambazo zinaweza kukudhi mahitaji.

“Tumeanzaa na kuzifungwa kwa wateja wetu na na tulianza na mita 4000 na mpaka sasa tumefikia asilimia 60 wamefunga mita 2200  na tunatarajia kuzimaliza kwa kuwafungia watu wenye uhitaji na wale waliokuwa na madeni na muda mfupi tutakuwa  tumezimaliza kwa wenye madeni”Alisema  

Awali ya pili mradi wa Mradi wa Hat fungani utakuwa na mita 10,000 kwa hiyo wanataraji kuwafikia wananchi kwa wananchi wengi Tanga kutokana na mahitaji ni mengi kutokana wenye uhitaji wa kubadilishiwa mita za luku wana wateja kkaribia 50,000 bado wanaendeleaa kuomba na wanatarajiwa kufikia mpaka 75,000 na ubadilishaji wa mita utakuwa ni urtarbu wa kudumu wataweka za luku.

 Kwa hiyo mita za zamani zitapeleekwa kwenye maeneo ambao hawajayafikia lengo kuhakikisha maeneo yote zinawekwa mita za kisasa,lengo kufiia asilimia 95 na maeneo mengine ni 85 na lengo ni kufikia asilia 100

 

MWISHO.

 

 

REA KUENDELEA KUWEZESHA WAENDELEZAJI WA MIRADI YA NISHATI VIJIJINI

June 17, 2025 Add Comment
-RC Njombe apongeza usimamizi wa miradi ya REA

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) utaendelea kutoa sapoti kwa waendelezaji wa miradi ya kuzalisha na kusambaza umeme kote nchini ili kuwezesha wananchi wengi kufikiwa na huduma bora ya nishati ambayo inachangia kuinua uchumi wa wananchi pamoja na huduma za kijamii.