MD TWANGE AENDELEA KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA UMEME
📌Atumia sehemu ya ziara yake kuelimisha na kugawa zawadi za majiko janja kwa viongozi wa Serikali za Mikoa na Wilaya Kanda ya ziwa
📌Asisitiza wananchi wasiogope kupika kwa umeme kwani ni gharama nafuu.
Katika kuhakikisha elimu ya nishati safi ya kupikia inamfikia kila Mtanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw. Lazaro Twange ametumia sehemu ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya umeme katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupika kwa umeme kwa viongozi wa Serikali za Mikoa na Wilaya ili kuongeza uelewa zaidi kwa wananchi.
Bw. Twange ametumia nafasi hiyo kuelimisha na kutoa zawadi za majiko janja yenye teknolojia inayotumia umeme kidogo kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Saidi Mtanda, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi Pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya TANESCO ya kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutumia umeme.
Amesema licha ya Shirika hilo kujikitika katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme wa uhakika bado wanajukumu la kutekeleza kwa vitendo Ajenda ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi kwa ajili ya kupikia na ametoa majiko hayo kwa viongozi wa Serikali ili kupata picha halisi ya unafuu wa kutumia umeme kupikia ili kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi.
‘’Vifaa hivi vinatumia umeme kidogo kwenye kupika na tumetoa majiko haya kwa ajili ya matumizi ya kupikia ili mtusaidie kuwahamasisha na kuongeza uelewa kwa wananchi kwa kuwa mtakuwa mashahidi na mabalozi wazuri wa kueleza faida za majiko hayo hatua itakayowavutia zaidi wananchi kisha kubadili mitazamo’’ amesisitiza Bw Twange
Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro ameipongeza TANESCO kwa mkakati huo ambao unadhamira ya dhati ya kufanya mageuzi ya elimu ya matumizi ya nishati safi ili kuwafanya wananchi kuachana na matumizi ya nishati isiyo salama zenye athari kiafya kwa watumiaji na chanzo cha uharibifu wa mazingira.
‘’Tumepokea zawadi ya jiko hili tunashukuru, tutaitumia mikutano yetu na wananchi kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi na wananchi wetu ni waaminifu ninaamini wataelewa na kwa sasa tutawaelimisha kwa vitendo,’’ alifafanua Mhe. Mtatiro.
Ziara ya Mkurugenzi wa TANESCO Bw. Lazaro Twange katika Mikoa ya kanda ya ziwa imelenga kukagua miradi mbalimbali ya uzalishaji umeme lakini pia ametumia nafasi hiyo kuongeza msisitizo wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ya umeme ikiwa ni muendelezo wa kampeni inayofanywa na TANESCO ya kuhakikisha ajenda ya Serikali inafanikiwa.
TUME YA UCHAGUZI YAPONGEZWA MAANDALIZI UCHAGUZI MKUU 2025

Na. Mwandishi Wetu, Zanzibar
MRADI WA KUZALISHA UMEME WA JUA KISHAPU WAFIKIA ASILIMIA 63.3-MD TWANGE
📌Asema awamu ya kwanza utazalisha Megawati 50 na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw. Lazaro Twange amesema Mradi wa uzalishaji umeme unaotokana na jua wa Kishapu Mkoani Shinyanga umefikia asilimia 63.3 kukamilika ambapo amesema awamu ya kwanza ya Mradi huo utazalisha Megawati 50 ambazo zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa ifikapo mwishoni mwa mwezi wa kumi mwaka huu.
MD Twange ameyasema hayo leo Juni 8 mwaka 2025 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo ambao unagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 118 kwa awamu ya kwanza huku awamu ya pili ikitarajia kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 204.
‘’Kwanza tunamshukuru Mhe. Rais kwa kutupatia fedha kwa awamu zote, kama mnavyoona kazi inaendelea na Mradi unatarajia kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa mwishoni mwa mwezi wa kumi kwa ajili ya kuwasambazia umeme wananchi, lakini pia tuko katika hatua za mwisho za manunuzi kwa ajili ya kumpata mkandarasi atakayetekeleza Mradi kwa awamu ya pili ambayo itazalisha megati 100’’ alisisitiza Mkurugenzi Mtendaji Twange.
Aidha, amewahakikishia wananchi kuwa TANESCO inafanya jitihada za makusudi za kuhakikisha Mradi unakamilika kwa wakati ili kuendana na ongezeko la mahitaji ya watu na shughuli za uwekezaji ambazo zinategemea nishati ya umeme kujiendesha.
Naye Meneja wa Mradi huo Mhandisi Emmanuel Andarson amesema awali Mradi huo ulipaswa kukamilika mwezi February mwaka huu lakini Mkandarasi aliongezewa muda baada kukabiliwa na baadhi ya changamoto ambapo ameahidi kukamilisha Mradi huo kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba .
Mradi wa uzalishaji wa umeme unaotokana na nguvu ya jua wa Kishapu uliopo katika Kijiji cha Ngunga Mkoani Shinyanga ulianza utekelezaji wake Desemba 8 mwaka 2023 na unatarajia kukamilika rasmi Oktoba 29 2025 ambapo unagharimu jumla ya shilingi bililioni 323 kwa awamu zote mbili ukitarajia kuzalisha megawati 150 za umeme.
MRADI WA KUZALISHA UMEME WA JUA KISHAPU WAFIKIA ASILIMIA 63.3 - MD TWANGE
📌Asema awamu ya kwanza utazalisha Megawati 50 na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw. Lazaro Twange amesema Mradi wa uzalishaji umeme unaotokana na jua wa Kishapu Mkoani Shinyanga umefikia asilimia 63.3 kukamilika ambapo amesema awamu ya kwanza ya Mradi huo utazalisha Megawati 50 ambazo zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa ifikapo mwishoni mwa mwezi wa kumi mwaka huu.
MD Twange ameyasema hayo leo Juni 8 mwaka 2025 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo ambao unagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 118 kwa awamu ya kwanza huku awamu ya pili ikitarajia kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 204.
‘’Kwanza tunamshukuru Mhe. Rais kwa kutupatia fedha kwa awamu zote, kama mnavyoona kazi inaendelea na Mradi unatarajia kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa mwishoni mwa mwezi wa kumi kwa ajili ya kuwasambazia umeme wananchi, lakini pia tuko katika hatua za mwisho za manunuzi kwa ajili ya kumpata mkandarasi atakayetekeleza Mradi kwa awamu ya pili ambayo itazalisha megati 100’’ alisisitiza Mkurugenzi Mtendaji Twange.
Aidha, amewahakikishia wananchi kuwa TANESCO inafanya jitihada za makusudi za kuhakikisha Mradi unakamilika kwa wakati ili kuendana na ongezeko la mahitaji ya watu na shughuli za uwekezaji ambazo zinategemea nishati ya umeme kujiendesha.
Naye Meneja wa Mradi huo Mhandisi Emmanuel Andarson amesema awali Mradi huo ulipaswa kukamilika mwezi February mwaka huu lakini Mkandarasi aliongezewa muda baada kukabiliwa na baadhi ya changamoto ambapo ameahidi kukamilisha Mradi huo kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba .
Mradi wa uzalishaji wa umeme unaotokana na nguvu ya jua wa Kishapu uliopo katika Kijiji cha Ngunga Mkoani Shinyanga ulianza utekelezaji wake Desemba 8 mwaka 2023 na unatarajia kukamilika rasmi Oktoba 29 2025 ambapo unagharimu jumla ya shilingi bililioni 323 kwa awamu zote mbili ukitarajia kuzalisha megawati 150 za umeme.m