SHINYANGA KUNUFAIKA NA MIRADI YA REA,WAUZIWA KWA RUZUKU MITUNGI 13000

June 02, 2025 Add Comment


📌Kila wilaya kunufaika na mitungi ya gesi 3,255 


📌REA yachochea ushiriki wa wanawake katika shughuli za kiuchumi


📌Mradi kupunguza ukataji wa miti unaosababisha mabadiliko ya tabianchi


Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeitambulisha kampuni ya Lake Gas Limited ambayo imepewa jukumu la kusambaza mitungi ya gesi 13,020 itakayouzwa kwa bei ya ruzuku ya asilimia 50 katika Mkoa wa Shinyanga.


Hayo yamebainishwa leo Juni 2, 2025 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Mhandisi wa Miradi kutoka REA, Bi. Annet Ndyanabo wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji mitungi ya gesi yenye ujazo wa kilo sita mkoani humo. 

Mha. Ndyanabo amesema kuwa mitungi ya gesi 13,020 itakayosambazwa mkoani Shinyanga ni utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia ambao una lengo la kuongeza matumizi ya nishati safi kufikia asilimia 80 ifikapo 2034.

"Utekelezaji wa mradi huu unaenda sambamba na malengo ya Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia (2024-2034) ambao unalenga kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia kufikia asilimia 80 ya watanzania wanaotumia nishati hiyo ifikapo mwaka 2034," Amesema Mha. Ndyanabo. 

Ameongeza kuwa, lengo la mradi ni kuongeza upatikanaji wa huduma za nishati safi ya kupikia kwa kuwawezesha wananchi wengi kumudu gharama za bidhaa za nishati safi  ili kutunza mazingira.


"Mradi huu utapunguza umaskini kwa kuwapa muda zaidi wanawake kushiriki katika shughuli za kiuchumi pindi wanapotumia mitungi ya gesi kama njia mbadala ya kupikia badala ya kuni na mkaa," Ameongeza Mha. Ndyanabo.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, CP Salum Hamduni ameipongeza REA kwa kuja na mradi huo na kuiomba iwe endelevu ili iweze kuwasambazia wananchi wengi nishati hiyo muhimu.


Naye, Mratibu wa nishati safi kutoka kampuni ya Lake Gas Limited, Bw. Ramadhan Siasa amesema watatekeleza mradi huo kwa kuzingatia makubaliano ya Mkataba wa kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia pamoja na kutoa elimu kwa wananchi ili kuchochea matumizi ya nishati hiyo.

Gharama ya Mradi huo ni shilingi  272,769,000 na wilaya zitakazonufaika ni pamoja na Wilaya ya  Shinyanga, Kishapu, Ushetu na Msalala na kila wilaya itapata mitungi 3,255.

NSSF YAWATAKA WAAJIRI KULIPA MICHANGO KWA WAKATI WASISUBIRI MPAKA WAPELEKWE MAHAKAMANI

June 01, 2025 Add Comment




Na Oscar Assenga,Tanga

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) umewataka waajiri kuhakikisha wanalipa michango ya watumishi wao kwa wakati na wasisubiri mpaka wapelekwe mahakamani kutokana na kutokuiwasilisha .

Hayo yalisemwa leo na Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga Nuhu Mbaga katika maonyesho ya 11 ya Biashara na Utalii yanayoendelea katika eneo la Mwahako Jijini Tanga.

Ambapo alisema wanashiriki maonyesho hayo kwa lengo la kutoe elimu kwa wananchi juu ya mafao mbalimbali wanayoyatoa wanapojiunga nao.

Alisema kwamba wanatakiwa kulipa michango kwa sababu ipo kwa mujibu wa sheria na wasipofanya hivyo kifungu cha 72 wanaweza kukitumia kwa ajili ya wao kupelekwa mahakamani.

“Hivyo nitumie nafasi hii kuwataka waajiri tusisubiri mpaka mpelekwe mahakamani bali wahakikisheni mnatekeleza wajibu wenu kupeleka michango ya watumishi wenu”Alisema

Aidha alitumia wasaa huo kuwahamasisha wananchi waliojiajiri kufika kwenye banda lao kuweza kupata elimu ya kuweza kujiunga na kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa kwenye mfuko huo ikiwemo ya kupata matibabu kama ilivyo kwa wengine

“Yote haya ni kutokana na sera nzuri ya awamu ya sita chiini ya Rais Dkt Samia Suluhu kwa sababu mtu akiwa na afya njema ataweza kwenda kujishughulisha na kufanya kazi ya kupata kipato cha mtu mmoja mmja na kuweza kujikwamua kiuchumi”Alisema

TANAPA YATUNUKIWA TUZO YA JUU ULAYA KWA MARA YA MFULULIZO

June 01, 2025 Add Comment


Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetunukiwa tuzo ya hadhi ya juu kwa mara ya sita mfululizo iitwayo European Quality Choice Diamond ya mwaka 2025 katika hafla iliyofanyika usiku wa tarehe 29 Mei, 2025, jijini Stockholm, nchini Uswidi, kwa kutambua utendaji wake mahiri katika utalii na uhifadhi.


Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Mshauri Mtendaji Mkuu wa taasisi ya European Society for Quality Research (ESQR), Bw. Michael Harris,  kwa Balozi wa Tanzania nchini Uswidi, Mhe. Mobhare Matinyi, ambaye aliambatana na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Bw. Mussa Nassoro Kuji; Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Rodwell Ole Meing'ataki; Afisa Mkuu wa Uhifadhi, Eunice Msangi; Afisa Uhifadhi Andrew Mbai; na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania, Malik Hassan.

TANAPA ilikuwa kampuni pekee ya utalii na uhifadhi kati ya 49 kutoka nchi 42 duniani zikiwemo zingine sita za Afrika iliyotunukiwa tuzo hiyo. TANAPA ni moja ya taasisi kadhaa nchini zenye usajili wa ISO 9001:2015 ambacho ndicho kigezo cha kupimwa utendaji na ESQR kila mwaka.

GCLA KANDA YA KATI YATOA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA MAJANGA YA KEMIKALI KWA WAKAZI WA RUAHA MBUYUNI

May 31, 2025 Add Comment
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilolo, Eston Kyando (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa makundi mbalimbali ya viongozi wa Kata ya Ruaha Mbuyuni juu ya namna ya kukabiliana na majanga ya kemikali ikiwemo ajali za magari yanayosafirisha kemikali. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa shule ya msingi Mbuyuni A, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, Mei 30, 2025. Kulia ni Meneja wa Usajili wa Kemikali na Maabara za Kemia, Musa Kuzumila.