REA YAHAMASISHA WANANCHI KUTUMIA MKAA MBADALA
habariMAWAZIRI WA NISHATI JUMUIYA YA SADC KUKUTANA NCHINI ZIMBABWE
📌.*Masuala ya Umeme, Gesi, Nishati Safi kujadiliwa*
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga ameongoza jopo la Wataalam kutoka Wizara ya Nishati katika Kikao cha awali cha Kamati Ndogo ya Nishati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kilicholenga kujadili maandalizi ya Mkutano wa Pamoja wa Kamati ya Mawaziri wa SADC wanaoshughulikia masuala ya Nishati utakaofanyika nchini Zimbabwe.
Kikao hicho cha awali kimefanyika tarehe 30 Mei 2025 katika Ukumbi wa Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao.
Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa SADC unatarajia kufanyika nchini Zimbabwe Mei 30 had 04 Juni 2025 ukitanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Nishati wa SADC.
Kikao hicho cha Mawaziri kitajadili ajenda mbalimbali ikiwemo hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme katika Kanda; Maendeleo ya sekta ndogo ya Mafuta na Gesi, Matumizi ya Nishati Safi na kujadili nafasi na utayari wa Kanda katika kutekeleza Azimo la Dar es Salaam lililotokana na Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Misheni 300.
Washiriki wengine katika kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao wametoka katika nchi zote zilizopo katika Jumuiya ya SADC.
WAZIRI KOMBO AWASISITIZA MACHIFU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI
habariPUMA ENERGY TANZANIA KUPITIA UPYA MPANGO MKAKATI WA BIASHARA
habariWawekezaji wa PUMA Energy Tanzania, ambao ni Serikali ya Tanzania na Puma Investments Limited, wamekubaliana kufanya mapitio ya mpango mkakati wa biashara wa kampuni hiyo ndani ya mwaka huu.
Mpango huu mpya wa biashara unalenga kuongeza uwekezaji, kupanua mtandao wa usambazaji, na kuongeza idadi ya bidhaa, kwa lengo la kuimarisha mchango wa wa kampuni hiyo katika uchumi wa Tanzania, na kukuza maendeleo ya sekta ya nishati.
Hayo yalibainishwa Jumatatu, Mei 26, 2025 wakati wa ziara ya viongozi wa ngazi ya juu wa PUMA Energy kwenye Ofisi ya Msajili wa Hazina iliyopo jijini Dar es Salaam, wakiongozwa na Bw. Mark Russel, Afisa Mtendaji Mkuu wa PUMA Energy Duniani.
Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, alisema mapitio ya mpango mkakati wa biashara yanalenga kuona ukuaji wa kampuni unalingana na vipaumbele vya maendeleo ya taifa, pamoja na kufungua milango ya fursa mpya katika sekta ya nishati.
“Uongozi wa kampuni na bodi lazima waangalie upya mpango mkakati wa biashara ndani ya mwaka huu ili kuanzia mwaka ujao tuweze kuzitumia vizuri fursa tulizonazo,” alisema Bw. Mchechu, huku akiweka wazi kuwa utekelezaji wa mpango mkakati mpya utaanza Januari mwakani.
PUMA Energy Tanzania ni kampuni inayomilikiwa kwa asilimia 50 na Serikali ya Tanzania na asilimia 50 na Puma Investments Limited.
Kampuni hii ni tawi la Puma Energy Holdings Pte Ltd, sehemu ya Trafigura PE Holding Ltd.
Bw. Mchechu alisisitiza kuwa uwekezaji wa Serikali katika PUMA ni mkakati muhimu unaolenga kuiwezesha Serikali kuwa na ushawishi mkubwa katika sekta ya nishati na mtandao wa usambazaji wa mafuta nchini.
Kwa upande wake Bw.Russel, alisema Tanzania ina fursa nyingi za kukuza biashara, ikiwemo miradi ya gesi ya asilia (LNG) na gesi ya kupikia (LPG).
“Tuna mpango wa kupanua huduma na kuongeza aina za bidhaa tunazotoa kwa jamii. Kupitia ushirikiano wetu na Serikali, tutashirikiana kufungua fursa zaidi na kukuza biashara hii,” alisema Bw. Russel.
Bw. Ben Quattara, Mkuu wa kampuni za PUMA Energy Afrika, alibainisha kuwa Tanzania ni mshirika muhimu katika biashara za PUMA barani Afrika na kampuni ina nia ya kuendeleza uwekezaji na faida zaidi hapa nchini.
Bi. Fatma Abdallah, Mkurugenzi Mtendaji wa PUMA Energy Tanzania, aliripoti ongezeko la asilimia 51 la faida mwaka 2024 na kufungua vituo vipya vya gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) pamoja na upanuzi wa biashara ya gesi ya kupikia (LPG) katika mikoa kadhaa ikiwemo Dodoma, Mwanza, na Arusha.
“Tegemeeni mambo makubwa kutoka PUMA Tanzania katika miezi na miaka ijayo,” alimalizia Bi. Abdallah.