INEC YATAKA VIONGOZI MIKOA 16 KUSHIRIKI KUONDOA WALIOKOSA SIFA

May 17, 2025 Add Comment

 

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Vunja nazi, Omary Mngwali kutoka Wilayani Mafia mkoani Pwani  akimuonesha Mwenyekiti wa Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele orodha yawatu wasio stahili kuwepo kwenye Daftari. 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akitazama Mwandikishaji Msaidizi katika Kituo cha Kata ya Kilindoni kilichopo Shule ya Msingi Kilimani akichukua taarifa za watu waliopoteza sifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Vunja nazi, Omary Mngwali wakati Mwenyekiti wa Tume alipotembelea vituo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani leo Mei 16, 2025 kuangalia mwenendo wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linaloendelea katika mikoa 16. (Picha na INEC).

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Vunja nazi, Omary Mngwali kutoka Wilayani Mafia mkoani Pwani akitazama daftari la Awali la Wapiga Kura.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akikagua mwenendo wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili wakati akitembelea vituo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani leo Mei 16, 2025(Picha na INEC).


Mkazi wa Mafia Mkoani Pwani akichukuliwa picha baada ya kujitokeza kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akimkabidhi kadi mmoja wa wananchi aliyefika katika kituo cha Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili wakati akitembelea vituo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani leo Mei 16, 2025(Picha na INEC).


Mwenyekiti wa Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akikagua mwenendo wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili wakati akitembelea vituo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani leo Mei 16, 2025(Picha na INEC).


Na Mwandishi wetu, Mafia
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka viongozi wa Mitaa na Vijiji pamoja na wananchi kwa ujumla katika mikoa 16 inayoendelea na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kushirikiana na watendaji wa zoezi hilo vituoni kutoa taarifa za Wapiga Kura waliopoteza sifa za kuwepo katuika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
 
Akiwa Wilayani Mafia, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele, alishuhudia wenye viti wa Mitaa katika vituo mbalimbali alivyopita wakiwaondoa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika zoezi linaloendelea la Uboreshaji wa Daftari awamu ya pili.
 
Akizungumza baada ya kutembelea Vituo vya Uboreshaji Wilayani humo, Jaji Mwambegele aliwa pongeza viongozi wa serikali za mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia mkoani Pwani wanavyoshiriki katikia uhakiki wa Daftari la awali la Wapiga Kura na kubaini watu ambao wamepotesa sifa hivyo kuwatolea taarifa na kuondolewa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
 
“Viongozi wa hapa Mafia wamejitokeza vizuri kuja na orodha ya watu wasiostahili tena kuwepo kwenye Daftari, sasa nawasihi viongozi katika mikoa hii 16 hapa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar pale ambapo wanaona kuna mwenyeji wao amepoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura basi wasisite kuja kujitokeza na kufuta taarifa zao,”alisema Jaji Mwambegele.
 
Aidha, Jaji Mwambegele amesema zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mikoa yote 16 limeanza vizuri na vituo vimefunguliwa kwa wakati na kuwataka wananchi ambao hawakupata fursa ya kujiandikisha hapo awali basi wafanye hivyo sasa ili wapate fursa ya kushiriki katika Uchaguzi Mwezi oktoba mwaka huu.
 
Afisa Mwadikishaji wa Jimbo la Mafia, Mohamed Hussein Othman akizungumzia zoezi hilo amesema limeanza vyema katika vituo vyote 15 ndani ya jimbo hilo na wananchi waliokosa fursa ya kujiandikisha na kuboresha taarifa zao hapo awali wanajitokeza hivi sasa.
 
“Zoezi letu la Uboreshaji wa daftari la Kudumu la Wapiga Kura limeanza vizuri, vituo vyote 15 vimefunguliwa saa 2:00 asubuhi wananchi wanajitokeza kuboresha taarifa zao na wale ambao hawakupata fursa katika uboreshaji wa awamu ya kwanza nao wanajitokeza kuhakikisha kwamba wanakuwepo katika Dafrari la Kudumu la Wapiga Kura,”alisema Othman.
 
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Vunja nazi kilichopo Kata ya Kilindoni Wilayani Mafia, Mwl. Omar Mngwali amesema yeye amekua kiongozi katika kitongoji hicho kwa muda mrefu na kushiriki vyema katika shughuli za kijamii imemuwezsha kutambua watu wake waliopoteza sifa wapatao 11 na kutoa taarifa ili waondolewe kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
 
Mzunguko wa pili wa uboreshaji umeanza leo Mei 16 na utaenda hadi Mei 22, 2025 unahusisha mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia Mei 16 hadi 22, 2025.
 
Zoezi hilo linakwenda sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la awali la Wapiga Kura ambapo  wananchi watapata fursa ya kukagua, kufanya marekebisho ya taarifa za wapiga kura na uwekaji wa pingamizi dhidi ya wapiga kura waliomo kwenye daftari ambao hawana sifa na litabandikwa katika vituo vyote vilivyotumika wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza.
 
Vituo vinafunguliwa Saa 2:00 asubuhi na kufungwa Saa 12:00 jioni kila siku kwa siku zote saba za utekelezaji wa zoezi hilo.

Dkt. Mpango azindua Shule ya Sekondari ya Mfano ya Benki ya CRDB, Benki hiyo ikitimiza Miaka 30

May 17, 2025 Add Comment

 

Arusha 16 Mei 2025 - Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, amezindua rasmi Shule ya Sekondari ya Mfano ya Benki ya CRDB, itayojengwa katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya Benki ya CRDB.

Shule hiyo ya kisasa ni matokeo ya dhamira ya Benki hiyo ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwekeza kwenye elimu bora kwa watoto wa Kitanzania.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shule hiyo uliofanyika katika seimna ya wanahisa wa Benki ya CRDB kuelekea Mkutano Mkuu, Dkt. Mpango aliipongeza Benki ya CRDB kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kijamii, hususan sekta ya elimu.
“Nawapongeza kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa sekta binafsi. Mmekuwa mstari wa mbele sio tu kwenye huduma za kifedha bali pia katika kuleta mabadiliko ya kweli kwenye jamii,” alisema Dkt. Mpango huku akiipongeza benki hiyo pia kwa kutimiza miaka 30 tokea kuanzishwa kwake mwaka 1996.


Akizungumza katika semina hiyo ya wanahisa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996, Benki ya CRDB imeendelea kuwa mshirika muhimu wa maendeleo kwa Taifa kwa kutoa huduma za kifedha zenye kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
Shule ya Sekondari ya Mfano ya Benki ya CRDB ina uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 600 na imejengwa kwa viwango vya kisasa ikiwa na madarasa ya kisasa 16, maabara 4, maktaba 1 chumba cha TEHAMA 1, ofisi za walimu na wafanyakazi 11, vyoo 53, miundombinu rafiki kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, pamoja na maeneo rafiki ya michezo. Mradi huu unatarajiwa kugharimu takribani shilingi bilioni 5.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, alisema shule hiyo ni zawadi ya Benki kwa Watanzania katika kuadhimisha miaka 30 ya mafanikio ya benki hiyo. “Tulipojiuliza ni zawadi gani ya kipekee tungeweza kuwapa Watanzania katika kutimiza miaka 30, tulikubaliana kwamba elimu ni urithi wenye nguvu kuliko wote. Shule hii ni ushahidi wa dhamira yetu ya kuwekeza katika kizazi kijacho,” alisema Nsekela.
Nsekela aliongeza kuwa shule hiyo ni sehemu ya mpango mpana wa Benki ya CRDB wa kurudisha kwa jamii katika nyanja za ya elimu, afya, mazingira na uwezeshaji wanawake kupitia CRDB Bank Foundation. “Tunaamini kuwa maendeleo endelevu hayawezi kufikiwa bila uwekezaji wa makusudi katika elimu. Kupitia shule hii, tunaweka msingi wa taifa lenye maarifa, maadili na ushindani wa kimataifa,” alibainisha.
Akitoa salamu zake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb), aliishukuru Benki ya CRDB kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya sekta ya elimu nchini. “Kwa niaba ya Serikali na Wizara ya Elimu, naishukuru sana Benki ya CRDB kwa maono na uamuzi huu wa kujenga shule ya kisasa kwa ajili ya watoto wa Kitanzania. Huu ni mfano hai wa jinsi sekta binafsi inavyoweza kushirikiana na Serikali katika kujenga musatakabali bora kwa watoto na vijana wetu.”
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB Bank Foundation, Martin Warioba, alisema shule hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa Benki ya CRDB kuboresha mazingira ya elimu nchini na kufungua fursa kwa watoto wa Kitanzania. “Mbali na kujenga shule hii ya mfano, tumejipanga pia kuanzisha mpango wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kwa kushirikiana na Wizara ya elimu.”

Uzinduzi wa shule hiyo unachukuliwa kama alama ya mafanikio ya miaka 30 ya Benki ya CRDB, na uthibitisho wa maono yake ya kujenga taifa lenye misingi imara ya elimu, usawa na maendeleo endelevu. “Tunajivunia kuona uwekezaji wetu ukiendelea kuzaa faida zaidi katika jamii,” alisema mmoja ya Wanahisa waliohudhuria semina hiyo.
Wanahisa wa Benki ya CRDB watafanya Mkutano Mkuu wa 30 kesho ambapo ajenda mbalimbali zinatarajiwa kujadiliwa ikiwamo kuidhinisha pendekezo la bodi ya wakurugenzi la gawio la shilingi 65 kwa hisa ikiwa ni ongezeko la asilimia 30 kulinganisha na gawio la shilingi 50 kwa hisa lililotolewa kwa mwaka 2023.


BENKI YA DUNIA YARIDHISHWA NA UTEKELEZWAJI WA MIRADI YA REA

May 16, 2025 Add Comment
-Yaahidi kuendeleza ushirikiano

-Ni miradi ya usambazaji umeme vitongojini na uhamasishaji wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

RAIS STUBB AZINDUA MRADI WA EURO MILIONI 20 WA UHIFADHI WA MISITU – FORLAND

May 16, 2025 Add Comment




Rais wa Jamhuri ya Finland, Mhe. Alexander Stubb, leo amezindua rasmi Mradi wa Kusimamia Uhifadhi wa Misitu, Matumizi Bora ya Ardhi na Kuongeza Thamani ya Mazao ya Misitu (Forestry, Land Use, and Value Chains Development in Tanzania – FORLAND), wenye thamani ya Euro milioni 20.

Mradi huo unalenga kukuza kanuni endelevu za uhifadhi wa misitu, kuboresha maisha ya wananchi, kuimarisha ukuaji wa uchumi wa Tanzania, pamoja na kuendeleza usimamizi wa misitu katika jamii, upandaji miti, na maendeleo ya mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu.

Katika hafla hiyo iliyofanyika Mei 16, 2025 katika Bustani ya Botanical Garden jijini Dar es Salaam, Rais Stubb ameshiriki katika zoezi la upandaji miti na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Tanzania na Finland katika sekta ya misitu.







“Nina imani mti nilioupanda utakua kama yalivyo mashirikiano kati ya nchi zetu katika sekta ya misitu, hususan kupitia mradi huu wa FORLAND,” amesema Rais Stubb.

Aidha, Rais Stubb ameeleza kuwa Finland ina misitu inayochukua asilimia 70 ya eneo la nchi hiyo, na kwamba bidhaa zake za misitu zinatambulika kwa ubora na uimara wake.

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), amesema kuwa mradi wa FORLAND unatekelezwa katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania, ukiwa na lengo la kuimarisha usimamizi wa rasilimali za misitu na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika jamii zinazozunguka misitu hiyo.


“Nchi yako (Finland) imekuwa mshirika muhimu kwa Tanzania katika sekta ya misitu, ikiwa imesaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali kama vile Mpango wa Usimamizi wa Eneo la Hifadhi ya Usambara Mashariki (1988–2002), vyuo vya misitu nchini Malawi, Tanzania na Zambia (1999–2005), Programu ya Kitaifa ya Misitu (2005–2010), pamoja na Biashara ya Kibinafsi ya Misitu na Kaboni (2010–2011),” amesema Mhe. Chana.

Ameongeza kuwa Finland pia imeisaidia Tanzania kupitia Programu za Kitaifa za Misitu na Nyuki (2013–2016), pamoja na Ufuatiliaji na Tathmini ya Rasilimali za Misitu (NAFORMA) tangu mwaka 2009.

Uzinduzi huo umehudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, pamoja na wanadiplomasia na viongozi waandamizi kutoka Serikali ya Tanzania na Finland.



WAZIRI AWESO ACHAGULIWA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAWAZIRI WA ZAMCOM 2025/2026

May 16, 2025 Add Comment


Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia Mhe  Caesar Chacha Waitara, amemwakilisha Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso (Mb), Waziri wa Maji katika Mkutano wa 12 wa Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (Zambezi Watercourse Commission-ZAMCOM) uliofanyika tarehe 15 Mei 2025 jijini Windhoek, Namibia.

Katika mkutano huo wa ZAMCOM unaojumuisha nchi nane za Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Msumbiji, Namibia, Zambia na Zimbabwe, Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso (Mb) amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa ZAMCOM katika kipindi cha mwaka 2025/2026.