SERIKALI YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA WALIMU 70,657 UTEKELEZAJI MITAALA ILIYOBORESHWA, YAANZA MAPITIO SHERIA YA ELIMU

May 12, 2025 Add Comment
Tarehe 1 Februari 2025 Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizindua rasmi Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023 inayolenga kutoa elimu inayozingatia ujuzi kulingana na mahitaji ya soko la ajira na kuchangia katika maendeleo ya Taifa.

WAZIRI DKT GWAJIMA AISHUKURU KAMATI,WADAU NA WADHAMINI MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE 2025

May 12, 2025 Add Comment


📌 Ahaidi ushirikiano wa Serikali na wadau.


📌 Aishukuru Kamati ya Kitaifa iliyoongozwa na Bi. Sara Masasi kwa kufanikisha maadhimisho hayo.


📌 Asema historia imeandikwa maadhimisho Siku ya Kimataifa ya Wanawake 2025


Na WMJJWM-Dar Es Salaam


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amewashukuru wadau wadhamini na Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa Mwaka 2025 inayoongozwa na Bi. Sara Masasi kwa kufanikisha maadhimisho hayo.


Waziri Dkt. Gwajima ameyasema hayo Mei 12, 2025 wakati wa hafla ya kuwashukuru wadau, wadhamini na Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho hayo iliyofanyika jijini Dar Es Salaam.

Waziri Dkt. Gwajima amesema Maadhimisho ya mwaka huu yamefanikishwa kupitia udhamini wa wadau,  Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi na kuwashukuru wadhamini kwa michango yao ya kifedha na vifaa iliyowezesha maadhimisho hayo kwa kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya Wanawake nchini.

Amesema Maadhimisho hayo hayakuwa tu sherehe bali yalikuwa jukwaa la kutafakari, kuhamasisha na kusherehekea mafanikio ya wanawake katika kipindi cha miaka 30 ya utekelezaji wa maazimio ya ulingo wa Beijing katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

"Kwa niaba ya Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara anayoiongoza huku akiwashukuru kwa kuweka  

historia na historia hiyo haitasahaulika na amewaomba kuendelea kushirikiana katika safari ya kuwawezesha wanawake kwa vitendo kwa sauti na kwa upendo." amesema Waziri Dkt. Gwajima.


Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amewasihi wadau hao kuendelea kushirikiana katika kupeleka mbele ajenda ya kumwezesha mwanamke na kukuza usawa wa Kijinsia hasa kwa kufanya kazi pamoja katika utekelezaji wa ajenda hizo.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake 2025 Bi. Sara Masasi ameishukuru Serikali kupitia Wizara kwa kuwaamini katika maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na amehaidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono juhudi mbalimbali za maendeleo.

Mmoja wa wadau kutoka Benki ya Biashara Tanzania (TCB) Adam Mihayo amesema Benki hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono ajenda mbalimbali hasa katika kuwawezesha Wanawake kiuchumi kupitia programu mbalimbali zinazotekelezwa na ne Benki hiyo.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imekutana na wadau wadhamini na Kamati ya Maandalizi ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa Mwaka 2025 kwa lengo la kufanya thathimini ya Maadhimisho hayo na mipango ya kuboresha zaidi kwa miaka ijayo.


MWISHO.

UCHAGUZI MKUU 2025 :MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA,12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 2025 Add Comment

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma leo Mei 12, 2025 wakati akitangaza  majimbo mapya yaliyogawanjywa na majimbo yaliyobadilishwa majina. (Picha na INEC). 

Na. Mwandishi Wetu, Dodoma

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeanzisha majimbo mapya nane na kubadilisha majina ya majimbo 12 ya uchaguzi yatakayotumika kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele amesema Tume imefikia uamuzi huo baada ya kupitia maombi kutoka kwenye mikoa mbalimbali nchini.

 

Amesema uamuzi huo umefanyika kwa kuzingatia masharti ya ibara ya 75(1), (2) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ikisomwa pamoja na kanuni ya 18(7) ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024.

 


Ameyataja majimbo hayo kuwa ni Jimbo la Kivule amabalo limegawanywa kutoka Jimbo la Ukonga na  Jimbo la Uchaguzi la Chamanzi  ambalo limegawanywa kutoka Jimbo la Mbagala yote ya mkoani Dar es Salaam.

 

“Mkoani Dodoma limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Dodoma Mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Uchaguzi la Mtumba na Mkoani Mbeya limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Mbeya Mjini limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Uyole,” amesema.

 

Ameongeza kuwa Mkoani Simiyu limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Jimbo la Uchaguzi la Bariadi limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la uchaguzi la Bariadi Mjini.

 

Jaji Mwambegele amesema Mkoani Geita yameanzishwa majimbo mawili ambapo Jimbo la Uchaguzi la Busanda limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Katoro na Jimbo la Uchaguzi la Chato limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Chato Kusini.

 

“Mkoani Shinyanga limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Solwa limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Itwangi,” amesema.

 


Akizungumza kuhusu majimbo kumi na mbili (12) ya uchaguzi yaliyobadilishwa majina, Jaji Mwambegele ameyataja majimbo hayo kuwa ni pamoja na Jimbo la Uchaguzi la Chato ambalo limebadilishwa jina kuwa Jimbo la Uchaguzi la Chato Kaskazini.

 

“Jimbo la Uchaguzi la Nkenge limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Missenyi, Jimbo la Uchaguzi la Mpanda Vijijini limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Tanganyika na Jimbo la Uchaguzi la Buyungu limebadilishwa jina sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Kakonko,” amesema.

 

Ameongeza kuwa Jimbo la Uchaguzi la Bariadi limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Bariadi Vijijini, Jimbo la Uchaguzi la Manyoni Mashariki limebadilishwa jina na kuwa Jimbo la Uchaguzi la Manyoni na Jimbo la Uchaguzi la Singida Kaskazini limebadilishwa jina na kuwa Jimbo la Uchaguzi la Ilongero.

 

Majimbo mengine ni Jimbo la Manyoni Magharibi kuwa Jimbo la Itigi, Jimbo la Singida Mashariki kuwa Jimbo la Ikungi Mashariki, Jimbo la Singida Magharibi kuwa Jimbo la Ikungi Magharibi, Jimbo la Tabora Kaskazini kuwa Jimbo la Uyui na Jimbo la Handeni Vijijini kuwa Jimbo la Handeni.

 

“Kutokana na ongezeko hilo la majimbo nane, kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kutakuwa na majimbo ya uchaguzi 272 yatakayofanya uchaguzi wa wabunge, katika Jamhuri ya Muungano.  Kati ya majimbo hayo 222 yapo Tanzania Bara na majimbo 50 yapo Tanzania Zanzibar,” amesema Jaji Mwambegele.

 

Ameongeza kuwa  kutakuwa na kata 3,960 zitakazofanya uchaguzi wa madiwani kwa Tanzania Bara katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

 

Mwisho.

MCHAKATO WA NEMC KUWA MAMLAKA WAENDELEA

May 12, 2025 Add Comment






Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali bungeni wakati wa Kikao cha 21 Mkutano wa 19 wa Bunge jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025.


Ofisi ya Makamu wa Rais imesema mchakato wa kulipa mamlaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji kupitia mchakato unaoendelea.


Kuifanya NEMC kuwa mamlaka kutaipa nguvu ya kisheria ya kusimamia majukumu yake ipasavyo na hivyo kujiwezesha kimapato.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ameliarifu Bunge jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 wakati akijibu swali la nyongeza Mbunge wa Mpendae Mhe. Toufiq Salim Turky lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Viti maalumu Mhe. Amina Ali Mzee aliyetaka kujua ni lini mchakato wa NEMC kuwa mamlaka kamili.


Mhe. Khamis amesema Mchakato wa kulifanya Baraza hilo kuwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (NEMA) tayari umekwishaanza na pindi utakapokamilika utawasilishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa maamuzi.


Alifafanua kuwa changamoto inayosababisha kuchelewa kwa vyeti vya tathmini ya athari kwa mazingira ni mifumo kuwa na changamoto hivyo kutumia muda mrefu wa kuviandaa.


Halikadhalika Naibu Waziri Khamis alisema kuwa baadhi ya miradi inachelewa kwasababu ya kukosa vigezo ambavyo vinataka maeneo ambako miradi inatekelezwa kulinda mazingira na afya.


“Niwapongeze mamemja wa kanda wa NEMC wakimsaidia mkurugenzi wanafanya kazi nzuri mnajitahidi kuhakikisha zoezi la utoaji wa vyeti linafanyika kwa haraka pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo ucheleweshaji wa tarifa kutoka kwa wataalamu za waelekezi,” alisema.


Awali katika swali lake la msingi, Mhe. Turky alitaka kujua kuna mpango gani wa kutatua changamoto za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) hususan za kibajeti ili iweze kushughulikia athari zitokanazo na uchafuzi wa mazingira nchini.


Akijibu swali hilo, Mhe. Khamis alifafanua kuwa NEMC imekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoathiri utekelezaji wa majukumu yake kwa ufanisi.


Alisema ili kukabiliana na changamoto hizi hususani za kibajeti, Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo Kufanya mapitio ya Kanuni za Ada na Tozo za mwaka 2021 na kuongeza vyanzo vipya vya mapato na viwango vya tozo kwa miradi mikubwa ambayo shughuli zake zina athari kubwa kwenye mazingira.


Alisema Serrikali inaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa matumizi ya kanuni mpya ya Ada na Tozo ya mwaka 2024, kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato ambayo inarahisisha ukusanyaji wa ada kwa ajili ya undeshaji wa shughuli za Baraza na kuboresha Kanzidata ya miradi yote inayotakia kulipa ada na tozo za Mazingira.


Naibu Waziri Khamis ameongeza kuwa Serikali inaendelea kufanya kaguzi za kimazingira katika miradi mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu na kuhimiza ulipaji wa ada na tozo za mazingira.


Pia, kuongeza idadi ya watumishi na kuanzisha Ofisi za Kanda ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa Wananchi na kuwafikia wadau wengi kwa muda mupi katika maeneo mbalimbali nchini.

HABARI, JAMII

DKT.DORIYE AVISHA VYEO VYA KIJESHI MAAFISA 145 NA ASKARI 476 WA NCAA NA KUSISITIZA UCHAPAKAZI,NIDHAMU,MAADILI NA UZALENDO KATIKA ULINZI WA RASILIMALI

May 12, 2025 Add Comment


Na Kassim Nyaki, NCAA.


Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) Dkt. Elirehema Doriye leo tarehe 12 Mei, 2025 amevisha vyeo jumla ya watumishi 621 ikijumuisha Maafisa 145 na askari 476 wa jeshi la Uhifadhi. 

Akizungumza na watumishi hao baada ya kuwaapisha na kuwavisha vyeo Dkt. Doriye amewasisitiza maafisa na askari wa jeshi la uhifadhi kuzingatia kiapo walichoapa na kuzingatia maadili ya utendaji kazi, kuzingatia sheria, ushirikiano, upendo na kujiepusha na rushwa katika maeneo ya kazi.


"Leo mmeapa na kuvishwa vyeo vya kijeshi, mnapaswa kuonesha dhamira ya dhati ya kulinda Hifadhi ya Ngorongoro na rasilimali zote za uhifadhi, vyeo mlivyovishwa vinakuja na majukumu makubwa ambayo yanahitaji kujituma na kuwajibika ipasavyo, hakikisheni mnakuwa mfano bora kwa jamii kwa kuzingatia maadili, nidhamu, sheria, uaminifu, uzalendo kwa rasilimali za nchi, kujiepusha na vitendo vya rushwa na kufuata miongozo ya jeshi la Uhifadhi” alisisitiza Dkt. Doriye.

Kamishna Doriye amewakumbusha  watumishi hao kuwa, kupanda cheo ni kuongezewa majukumu ya kiuongozi katika usimamizi wa shughuli za uhifadhi, utalii, ulinzi, maendeleo ya jamii na urithi wa asili na utamaduni uliopo hifadhi ya Ngorongoro na kusisitiza kuwa suala la mafunzo ya kijeshi kwa watumishi wa NCAA litakuwa endelevu ili kuendelea kujenga utimamu wa mwili kwa afisa na askari.

Awali akizungumza katika tukio hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi (SACC) anayesimamia Idara ya Rasilimali watu na Utawala Salma Chisonga ameeleza kuwa tukio la kuvishwa vyeo watumishi hao ni utekelezaji wa vibali vya kupandisha vyeo watumishi ambavyo vilitolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2021/2022 hadi mwaka 2024/2025.

SACC Chisonga amebainisha kuwa maafisa 145 waliovishwa vyeo wamegawanyika katika ngazi mbalimbali ambapo Maafisa uhifadhi Wakuu daraja la kwanza ni 5, Maafisa uhifadhi Wakuu daraja la II ni 21, Maafisa uhifadhi waandamizi ni 31, Maafisa uhifadhi daraja la I ni 56 na Mafiasa uhifadhi daraja la II ni 32.

Ameongeza kuwa askari 476 waliovishwa vyeo wamegawanyika katika ngazi mbalimbali ambapo askari wa uhifadhi mkuu daraja la I ni  39, askari wa uhifadhi wakuu daraja la II ni 54, askari wa uhifadhi Waandamizi ni 70, askari wa uhifadhi daraja la kwanza ni 86 na askari wa uhifadhi daraja la II ni 227.