REA YAPONGEZWA NA JESHI LA MAGEREZA UHAMASISHAJI NISHATI SAFI

May 06, 2025 Add Comment


📌Rais Samia apewa kongole uhamasishaji nishati safi 


📌REA, STAMICO kushirikiana uzalishaji wa Rafiki briquettes


📌Kiwanda cha Rafiki briquettes mbioni kujengwa Geita


📍Geita


Wakala wa Nishati Vijijini (REA), umepongezwa na Jeshi la Magereza kwa kuhamasisha, kuwezesha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa taasisi zinazohudumia watu zaidi ya 100 hapa nchini.

Hayo yemebainishwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza mkoa wa Geita, ACP Jonam Mwakasagule wakati akizungumza na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) mkoani Geita.

'Sisi kama Jeshi la Magereza tulikuwa tunapata shida sana hasa wakati tunatumia kuni kupika na kutupotezea muda mwingi  porini na kuepuka hatari za kupoteza maisha," Amesema ACP Mwakasagule. 


ACP Mwakasagule ameongeza kuwa, matumiz ya nishati safi katika jeshi hilo sasa yamepewa kipaumbe ili kujenga afya bora kwa kupunguza magonjwa ya macho na kifua yanayotokana na matumizi ya kuni wakati wa kupika chakula. 

Naye, Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini Mha. Ahmed Chinemba amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024 - 2034).

"Mhe. Rais amesema taasisi zinazohudumia watu zaidi ya 100 ziachane na matumizi ya kuni na mkaa na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia  ikiwemo gesi asilia, umeme, bayogesi na makaa ya mawe yaliyoboreshwa, ". Amesema Mha. Chinemba

Aidha, Mha. Chinemba ameeleza kuwa REA kwa kushirikiana na STAMICO wapo mbioni kujenga kiwanda cha kuzalisha mkaa mbadala mkoani Geita ili kurahisisha upatikanaji wa mkaa mbadala katika maeneo hayo ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa watanzania.


Mwisho.

MATHIAS CANAL ASHINDA TUZO YA SAMIA KALAMU AWARDS, WAZIRI ULEGA AMPA SHAVU MBELE YA RAIS SAMIA

May 06, 2025 Add Comment
Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa WazoHuru Media Group Limited Ndg Mathias Canal ameshinda Tuzo mbili za SAMIA KALAMU AWARDS sekta ya Ujenzi na chombo bora cha mtandaoni.

Pamoja na zawadi ya Cheti, Ngao, Tsh Milioni 10, lakini pia Mathias Canal amezawadiwa safari ya kwenda nchini Japani pamoja na kufanya kazi ya kusafiri nchi nzima kueleza kwenye vyombo vya habari mafanikio na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025.

Tuzo hizo zimetolewa leo tarehe 5 Mei 2025 katika ukumbi wa Super Dome Masaki Jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan

Tuzo hizo zimetolewa kwa wanahabari watanzania kwa lengo la kuhamasisha, kuhimiza na kukuza wigo wa uchakataji, utangazaji na uchapishaji wa maudhui ya ndani kupitia vyombo vya habari.

Tuzo hizi zitahusisha maudhui yaliyochapishwa kupitia magazeti, redio, televisheni, majukwaa ya mtandaoni pamoja na tuzo kwenda kwa vyombo vya habari. Tuzo hizi zinahusisha habari zilizochapishwa kati ya Januari 01 hadi Oktoba 26, 2024.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi Mhe Abdalah Ulega, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Innocent Bashungwa (Mb) amesema kuwa pamoja na zawadi ya Tuzo pia Waziri Ulega amempa zawadi ya kufanya kazi katika wizara hiyo hivyo akaripoti Wizarani kwa ajili ya kuanza kazi.

Aidha, utoaji wa tuzo hizi umelenga kuchochea uandishi wa makala zilizofanyiwa utafiti na uchambuzi kuhusu maendeleo ya nchi, uwajibikaji, uzalendo na kujenga chapa na taswira ya nchi.





RAIS SAMIA ASHIRIKI HAFLA YA SAMIA KALAMU AWARDS 2025 JIJINI DAR ES SALAAM

May 06, 2025 Add Comment

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Viongozi, Wadau wa habari pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa Tuzo za Samia Kalamu Awards2025 kwa Waandishi wa Habari katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Mei, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za Samia Kalamu Awards 2025 kwa Waandishi wa Habari iliyofanyika katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Mei, 2025.   

     Viongozi, wadau wa Habari pamoja na wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za Samia Kalamu Awards2025 kwa Waandishi wa Habari iliyofanyika katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Mei, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye picha ya pamoja na Mama Getrud Mongela wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo kwa Waandishi wa Habari ijulikanayo Kama Samia Kalamu Award 2025 Ukumbi wa The Super Dome Masaki Dar es Salaam Leo Mei 05,2025.

NYAMGUMA MAHAMUD AIBUKA MSHINDI HABARI ZA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

May 06, 2025 Add Comment



*📌Ni kupitia Tuzo za Uandishi wa Habari za  Samia Kalamu Awards*


*📌Wizara ya Nishati yatambua mchango wake*


📌 *Yamzawadia fedha taslimu, jiko linalotumia umeme kidogo, kompyuta mpakato na uniti za umeme za mwaka mmoja*


📌 *Mhandisi Mramba asema Tuzo ni kielelezo cha kuunga mkono juhudi za Rais Samia uhamasishaji Nishati Safi ya Kupikia*

Nyamguma Mahamud, Mwandishi wa Habari  kutoka Mlimani FM ameibuka kidedea katika Tuzo za Uandishi wa Habari za Samia Kalamu Awards 2025 kupitia kipengele cha habari za Nishati Safi ya Kupikia ambapo Wizara ya Nishati imetambua mchango wake kwa kumpa zawadi mbalimbali ili kuendelea kuhamasisha utoaji wa elimu ya Nishati Safi ya Kupikia.

Hafla ya utoaji wa Tuzo hizo imefanyika jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Dkt. Samia Suluhu Hassan.



Mohamud amekabidhiwa zawadi zake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.

Mshindi huyo amekabidhiwa fedha taslimu shilingi milioni tano, kompyuta mpakato, jiko linalotumia umeme kidogo na uniti za umeme za mwaka mzima.

"Tunatambua  masuala aliyoyaandika katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia, kwahiyo tumemzawadia pia jiko la umeme la kisasa linalotumia umeme mdogo pamoja na umeme wa kutumia nyumbani kwake kwa mwaka mmoja," amesema Mha. Mramba

Amesema Tuzo ya Nishati Safi ya Kupikia ni kielelezo cha  kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika  kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Samia Kalamu Awards  imeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwa na kaulimbiu ya "Uzalendo Ndio Ujanja'