Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

TSB KUTUMIA MCHEZO WA YOGA KUHAMASISHA ZAO LA MKONGE

June 26, 2023 Add Comment


Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) Saady Kambona wakati wa Shughuli ya Kimataifa ya Mchezo wa Yoga iliyofanyika kwenye Hotel ya Mkonge Jijini Tanga.

Mwalimu wa Yoga kwa upande wa Tanga Darshana Minesh akizungumza 

Mwalimu wa Yoga kwa upande wa Tanga Darshana Minesh kulia akiongoza mchezo wa Yoga 
Washiriki wa mchezo wa Yoga wakiendelea nao kwenye Ukumbi wa Hotel ya Mkonge Jijini Tanga 
Mchezo wa Yoga ukiendelea
Mchezo wa Yoga ukiendelea
Wageni mbalimbali wakifuatilia mchezo huo
Picha ya pamoja na kikundi cha Yoga cha Jijini Tanga
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga (TPC) Lulu George ambaye ni miongoni mwa wachezaji wa mchezo huo 


Na Oscar Assenga,Tanga

BODI ya Mkonge Tanzania (TSB) imeweka bayana kwamba itatumia pia mchezo wa Yoga kuhamasisha Kilimo cha zao la Mkonge ili kuweza kupanua wigo mpana ili kuongeza idadi ya wakulima.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) Saady Kambona wakati wa Shughuli ya Kimataifa ya Mchezo wa Yoga iliyofanyika kwenye Hotel ya Mkonge Jijini Tanga.

Kambona ambaye alialikwa kwenye shughuli hiyo kama mgeni Alisema mashuhuri kwenye shughuli ya kimataifaa ya Yoga ambapo Tanga wana wanachama wengi ambapo aliweza kujionea shughuli zinazoendelea.

Alisema kwamba baada ya kuona shughuli hizo amejifunza kwamba mchezo wa Yoga ni mchezo muhimu kwa ajili ya afya ya akili na kuweza kuona namna mazoezi yanavyofanyika tumeshuhudia walimu kutoka nchini India wakifundisha kupitia videeo Conference akionyeha mazoezi yanavyokwenda.

Aidha alisema kwamba hivyo wameona ni hatua muhimu kwao kufika na kuna uwekezako wa kutumia mchezo wa Yoga kuhamasisha kilimo cha zao la mkonge kutokana na kwamba wao kila kila fursa wanaiutumia kuona namna ya kuiunganisha na zao la Mkonge.

Alisema kwamba na jambo hilo linafanyika hoteli ya Mkonge ambayo ni Brand kubwa ya zaio la Mkonge Tanga na amefurahi sana na Taasisi ya Yoga ni jambo nzuri sana.

Kwa upande wake Mwalimu wa Yoga kwa upande wa Tanga Darshana Minesh aliitaka jamii kutambua umuhimu wa Yoga kwa afya ya mwili,akili na roho na kwamba yatawasaidia katika kuleta mitazamo chanya kwenye mambo mbalimbali ya maisha yao.

"Yoga ni muhimu sana kwenye afya ya mwili ,akili na roho na mtu akifanya hatajutia maamuzi ya kujiunga kwani ataona mabadiliko makubwa kwenye maisha yake," alisisitiza Mratibu huyo wa Yoga kwa Mkoa wa Tanga.

RAIS DKT. SAMIA ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA NA TFF

June 13, 2023 Add Comment


Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma (kulia) akipokea Tuzo ya Heshima kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania  (TFF)  Ndg. Wallace Karia (kushoto) ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuendeleza Soka nchini.Tuzo hiyo ameipokea katika Usiku wa Tuzo Juni 12, 2023 Jijini Tanga.

Na Eleuteri Mangi, WUSM, Tanga

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa mchango wake wa kupenda, kuthammini na kuendeleza michezo nchini.

 

Tuzo hiyo imetolewa kwa Rais Dkt. Samia ikiwa ni mwendelezo wake kwenye sekta ya michezo kukutana na kuwapongeza wanamichezo wanapofanya vizuri kwenye michezo tangu aingie madarakani pamoja na kuunga mkono na kutia hamasa vilabu vya Simba na Yanga kwenye mashindano ya kimataifa kwa kutunuku kila goli lililofungwa katika mashindano ya Klabu Bingwa na Shirikisho la Mpira Afrika kwa kila goli lililofungwa maarufu kama "Goli la Mama".

 

Akipokea tuzo hiyo Juni 12, 2023 jijini Tanga kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgeni Rasmi katika usiku wa Tuzo za Shirikisho la Mpira nchini (TFF) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ameahidi kuifikisha tuzo hiyo na kusema imetolewa kwa Rais wa nchi akiwa ni shabiki namba moja na mpenda michezo nchini.

 

Naibu Waziri Mwinjuma ameongeza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga vizuri kuendeleza miundombinu ya michezo nchini kwa kukarabati viwanja saba vya Mkwakwani Tanga, CCM Kirumba Mwanza, Sokoine Mbeya, Jamhuri Dodoma, Uwanja wa Benjamin Mkapa na Uhuru vya jijini Dar es salaam na Uwanja wa Amani Zanzibar pamoja na kujenga viwanja vipya viwili nchini katika mikoa ya Arusha na Dodoma kabla ya mwaka 2027 ambapo Tanzania, Kenya na Uganda zimeomba kuwa wenyeji wa Mashindano ya Afrika (AFCON).

 

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Mpira nchini (TFF) Bw. Wales Karia amesema  wanautaratibu wa kuwatambua na kuwatuza watu mbalimbali waliotoa mchango wao katika kukuza na kuendeleza soka nchini kila wanapofunga msimu wa ligi zote za mpira wa miguu chini.

 

Hafla hiyo ya utoaji tuzo imehudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Waziri Kindamba, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu pamoja na Viongozi mbalimbali, wachezaji na wageni waalikwa walioshamirisha hafla hiyo.


MWENYEKITI WA UVCCM UBUNGO ANOGESHA NUSU FAINALI KIMWANGA CUP, HAWA ABDUL REDE CUP KWA KISHIND0

May 21, 2023 Add Comment







Na Mwandishi Wetu -Dar es Salaam


Hekaheka za michuano ya kuwania kuingia fainali ya michuano ya ligi ya mpira wa miguu katika ligi ya Kimwanga CUP na mashindano ya Hawa Abdul Rede CUP yamepamba moto huku Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa UVCCM Wilaya ya Ubungo, Shadrack Makangula, akiwataka vijana kutumia fursa hiyo kama sehemu ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.


Katika mtanange huo kwa upande wa mpira wa miguu umezikutanisha timu za Ting Wayland ambapo ilifanikiwa kuvuka hatua ya fainali kwa kuchambana timu cha kituo cha kulea vipaji Lamasia FC kwa bao 2-0 huku upande wa Rede timu ya Kanuni ikifanikiwa nayo kwenda fainali kwa ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Manzese Princes.


Hayo ameyasema kabla ya kuanza kwa michuano hiyo inayopigwa katika Uwanja wa Bubu Kata ya Makurumla Manispaa ya Ubungo, katika mashindano hayo ya kuwania ng’ombe aliyoandaliwa na Diwani wa Kata hiyo, Bakari Kimwanga pamoja na Diwani wa Viti Maalumu Manispaa ya Ubungo, Hawa Abdulraman ambaye amekutanisha mabinti nao kuwania ng’ombe katika michuano hiyo.


“Kwanza, nitumie nafasi hii kuwashukuru madiwani wetu kwa kuona umuhimu mkubwa wa kuanzisha michuano ya mpira wa miguu na rede ambayo yote kwa ujumla wake yanawasaidia vijana wetu kuonyesha vipaji vyao walivyonavyo, lakini pia inasaidia kupata exposure (fursa) na kubwa zaidi kutengeneza mahusiano mazuri baina ya viongozi na wananchi.


“Hivyo ni vema kwa mashabiki, wakeleketwa na wananchi kwa ujumla ambao timu zao wanazozishabikia zimefuzu kucheza nusu fainali kuhakikisha kuwa wakati wa michezo hiyo inapoendelea wawe na utulivu wawapo uwanjani kwa sababu tutakapoanzisha vurugu uwanjani hapa tutawakatisha tamaa wadau, wahisani na viongozi katika kuanzisha ligi mbalimbali kwa ujumla wake,” amesema Makangula


Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa UVCCM amewataka wananchi kwa ujumla kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.


Kutokana na hali hiyo mwenyekiti huyo wa UVCCM wilaya aliwashukuru viongozi mbalimbali aliombatana nao na kuwaomba madiwani hao michezo hiyo iwe endelevu.


Mwisho

TRA, KCMC ZATOSHANA NGUVU MICHUANO YA SHIMUTA TANGA

November 17, 2022 Add Comment


Mshambuliaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulia akiwani mpira dhidi ya timu ya KCMC wakati wa michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga
Mshambuliaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulia akiwani mpira dhidi ya timu ya KCMC wakati wa michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga
Mshambuliaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulia akiwani mpira dhidi ya timu ya KCMC wakati wa michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga








NA Oscar Assenga, TANGA

TIMU za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mabingwa Watetezi kwa upande wa mpira wa Miguu na Hospitali ya Rufaa KCMC ya Kilimanjaro zimetoshana nguvu baada ya kufungana bao 1-1, katika michuano ya Shimuta inayoendelea Jijini Tanga.

Mchezo huo ambao ulifanyika kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga ulikuwa na upinzani mkubwa kwa kila timu kutaka kupata matokeo mazuri jambo ambalo lilizidisha ugumu wa mchezo huo

Timu ya KCMC ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kupitia Yusuph Madili aliyepiga faulu ya kona iliyotinga moja kwa moja na hivyo kuamsha shangwe na hari kwa mashabiki wao.

Mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko KCMC walikuwa mbele kwa bao 1-0 ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi kutokana na kila timu kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake na kuingiza nguvu mpya.

Walionekana kujipanga na kujiimarisha katika kipindi hicho timu ya TRA ilianzisha mashambulizi mfululizo lango mwa wapinzani wao huku wakicheza pasi fupi fupi na ndefu .

Kutokana na aina hiyo ya mchezo ambao walikuwa wakicheza iliwapelekea kuweza kupata bao la kusawadhisha kupitia kwa Datram Benzema ambaye alitumia uzembe wa mabeki kupachika wavuni bao hilo na hivyo kuamsha shangwe uwanja mzima.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Katibu wa timu ya TRA Kamna Shomari alisema kwamba wanamshukuru mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha kupata Sare na wana mechi nyengine.

Alisema kwamba hivyo wana matumaini watarekebisha mapungufu na kufanya vizuri Michezo ijayo na kwamba wamepania kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mechi yao


TPDC YAZIGARAGAZA BENJAMINI MKAPA HOSPITALI, TPHPA MICHUANO YA SHIMUTA TANGA.

November 17, 2022 Add Comment

 

Kikosi cha timu ya  Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wanaume 

Kikosi cha timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wanawake 

Na Oscar Assenga, TANGA

TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ya kuvuta kamba kwa upande wa wanaume leo wameibuka kidedea kwenye mchezo wa kuvuta kamba baada ya kuwavuta timu ya Benjamini Mkapa Hospitali kwa seti 2-0.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake ulifanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popatlaly Jijini Tanga ambapo wachezaji wa timu ya kuvuta kamba ya TPDC walionekana kuwa makini jambo ambalo liliwawezesha kuibuka na ushindi huo

Baada ya timu hiyo ya wanaume kumaliza kuvuta kamba iliingia upande wa wanawake ambapo timu ya Shirika hilo nayo iliweza kuibuka kidedea baada ya kuwavuta wanawake wenzao wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu (TPHPA) kwa seti 2-0.

Timu ya TPDC ya kuvuta kamba iliwakilishwa vema na wachezaji wake mahiri ambapo kwa upande wa wanaume iliongozwa na Nahodha Joram Ndalahwa,Nnocent Mvamba,Adam Sajilo na Joseph Majebele.

Kwa upande wa timu ya wanawake iliwakilishwa vema na Rehema Saidi,Robi Chambiri,Catherine Madinda na nahodha wao Joyce Kiheka .