Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

MWANAMKE NI MSUKUMO WA MAENDELEO KATIKA JAMII -DKT BITEKO

August 19, 2025 Add Comment


📌 Asema Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa wanapata haki na heshima wnayostahili

 

📌Azindua Mpango kazi wa Kitaifa wa Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama

 

📌 Unalenga kushirikisha wanawake kikamilifu katika masuala ya Amani na Usalama

 

📌 Ataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutokomeza dalili zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani na usalama katika jamii

 

📌 Asema kuzinduliwa kwa mpango kazi wa Amani na Usalama kunaonesha jinsi Tanzania inavyoheshimu na kutekeleza makubaliano ya kimataifa

 

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

 


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Wanawake ni chanzo cha msukumo wa maendeleo katika Jamii hivyo Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa kila mwanamke nchini awe mama au mtoto wa kike anapata haki na heshima anayostahili.

 


Wakati Serikali ikiendelea kuhakikisha kuwa Wanawake nchini wanapata haki zao ikiwemo ya usalama na amani, ametoa wito kwao kuendelea kujitambua na kuchangamkia kila aina ya fursa inayojitokeza nchini.

 


Dkt. Biteko amesema hayo wakati akizindua Mpango kazi wa Kitaifa wa kutekeleza Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama  2025 – 2029 ikiwa ni Azimio namba 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Wanawake, Amani na Usalama.

 


Azimio hilo ambalo limeridhiwa na nchi zote Wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania linasisitiza na kutoa kipaumbele kwenye ushiriki kamili wa wanawake katika hatua zote za ujenzi wa amani, uzuiaji na utatuzi wa migogoro, mazungumzo ya amani, ulinzi wa amani na ujenzi mpya wa jamii baada ya migogoro.

.


Dkt. Biteko amesema kuwa kutekelezwa kwa Azimio hilo la Umoja wa Mataifa kunaonesha kuwa Tanzania si nchi inayoridhia tu mipango ya kimataifa inayowekwa  bali inaheshimu makubaliano na maazimio ya kimataifa na hii inaifanya Tanzania chini ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan nikuzidi kuaminika Kimataifa na kuwa mfano wa kuigwa.

 


Akizungumzia, utekelezaji wa Ajenda hiyo ya Wanawake nchini Tanzania, Dkt. Biteko amesema kuwa "Tanzania tulishapiga hatua kubwa na tunaendelea vizuri katika kutekeleza Ajenda hii ya Wanawake, Amani na Usalama ambapo kwa mujibu wa Gender Inequality Index ya mwaka 2021, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilishika nafasi ya 146 kati ya nchi 191 kutokana na maendeleo yaliyopo tangu miaka ya 1990 katika kuhimiza usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake, kubiresha afya ya Mama na Mtoto pamoja na uwepo wa Uwakilishi wa Wanawake Bungeni."

 


Ameongeza kuwa, mujibu wa Global Peace Index ya mwaka 2021; Tanzania ilishika nafasi ya 58 kati ya nchi 163 zilizo na hali bora ya amani Duniani.

 


Akieleza kuhusu mafanikio.mengine yaliyofilkiwa katika Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama nchini, Dkt. Biteko amesema Tanzania imeendelea kuwapa Wanawake fursa za juu na za Maamuzi ambapo hadi.kufikia Mei, 2023 Uwakilishi wa Wanawake katika mfumo wa Mahakama umefikia asilimia 46.6.

 


Ameongeza kuwa asilimia 22 ya Askari Polisi ni Wanawake na asilimia 30 ya Maafisa Uhamiaji ni Wanawake vile vile, Tanzania Bara ina Mawakili wa Serikali 785 ambapo kati yao wanawake ni 410 sawa na asilimia 52.

 

Ameeleza  kuwa kwa upande wa Zanzibar, kuna jumla ya Mawakili wa Serikali 76 ambapo Wanawake ni 34 sawa na asilimia 44 ya Mawakili wote hivyo kwa hatuo hizo zilizopigwa na Tanzania nchi haina budi kujipongeza.

 


Pamoja na mafanikio hayo, Dkt. Biteko amesema kuwa bado kuna masuala ambayo yanahitaji kupewa msukumo ili kuleta haki na usalama kwa wanawake  kwani takwimu zinaonesha kuwa asilimia 48.3 ya wanawake wote Tanzania wamewahi kufanyiwa ukatili wa aina mbalimbali, ambapo mwaka 2015 asilimia 65 ya wanawake waliogombea nafasi mbalimbali za uongozi walikutana na changamoto  ikiwemo za matusi huku asilimia 17 ya wanawake hao wakishambuliwa na asilimia 13 wakiombwa rushwa ya ngono.

 


Amesisitiza kuwa takwimu hizo zinaonesha kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuinua haki ya mwanamke hivyo mpango huo uliozinduliwa unalenga kuhakikisha kuwa matendo yasiyo ya haki kwa wanawake yanatoweka na hadhi ya mwanamke inapanda kuliko sasa.

 

Aidha, Dkt. Biteko amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuutekeleza mpango huo wa amani na usalama kwa nguvu kubwa ikiwemo kutoa elimu na kutokomeza dalili zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani na usalama ikiwemo mila na desturi zinazoweza kuleta madhara kwenye jamii, wahamiaji haramu, unyanyasaji wa kijinsia na matumizi ya dawa za kulevya.

 

Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima ametaja baadhi ya vipaumbele vya Mpango wa Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama kuwa ni uzuiaji wa migogoro, ushiriki wa wanawake  katika kufanya maamuzi kwenye ngazi zote katika mikataba ya amani na kuwalinda wanawake na wasichana dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia wakati na baada ya migogoro .

 

Amesema.kuwa mpango huo utaleta matokeo chanya kwenye masuala ya amani na usalama kwa wanawake na kuwezesha Serikali kutimiza wajibu wake kitaifa, kikanda na kimataifa katika kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu kwenye masuala hayo ya amani na usalama.

 

 

Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Stergomena Tax amesema uzinduzi wa mpango huo ni tukio la historia na lenye uzito si kwa taifa tu bali kimataifa katika  kujenga dunia yenye haki usawa na amani.

 

Ameongeza kuwa, ni  kielelezo thabiti cha dhamira ya Serikali katika ushirikishaji wanawake katika masuala ya amani na usalama  na uongozi.

 

Amemshukuru Rais Samia kwa kuwa sauti ya kimataifa katika kuhakikisha kuwa Dunia inakuwa na haki na amani na hii imepelekea Tanzania kutambulika duniani kwa kutoa mchango mkubwa katika misheni za kuleta amani ambapo hadi sasa Tanzania imeshatoa takriban askari 1500 katika misheni za kuleta amani na idadi hiyo ikijumuisha wanawake na wanaume.

 

 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto - Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe  ameeleza kuwa Mpango wa Ajjenda ya Wanawake, Amani na Usalama uliozinduliwa ni muhimu kwa maendeleo ya wanawake wote na Tanzania kwani maendeleo yanazidi kuchipua pale kunapokuwa na amani na usalama.

 

Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatekeleza ajenda hiyo kwa vitendo kwani nafasi za uongozi kwa wananwake zimeongezeka, mfano ukiwa ni uteuzi wa majaji wanawake wasiopungua sita ambapo hapo nyuma idadi  ilikuwa chini ya hapo, pia Serikali  inazingatia bajeti za masuala ya kijinsia kwa wizara zote .

 

  Naye, Anna Mutavati, Mkurugenzi wa UN- Women katika Kanda ya  Mashariki na Kusini mwa Afrika, ameipongeza Tanzania kwa kuzindua ajenda hiyo ya Usalama na Amani kwa wanawake  na kueleza kuwa inaendelea kuwa mfano wa kuigwa katika masuala ya amani na usalama ikiongozwa na Amiri Jeshi Mkuu amabye ni Rais, Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan.

 

Mwisho.

UMEME JUA KUCHOCHEA UCHUMI MAENEO YA VIJIJINI

August 19, 2025 Add Comment


*📌Kaya 1,227 kunufaika na mradi wa Umeme Jua Lindi*


*📌REA kusambaza Majiko Banifu 5,576 Lindi*


*📍Kila wilaya kugawiwa  Majiko Banifu 1,115*


📍Lindi


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imepeleka Mkoani Lindi Mradi wa Umeme Jua wenye thamani ya shilingi milioni 801.74 katika visiwa vyote vitano vilivyopo wilayani Kilwa ikilenga kuongeza upatikanaji wa umeme katika maeneo hayo ambayo yapo mbali na Gridi ya Taifa na kuhamasisha matumizi ya teknolojia safi kupitia mifumo ya umeme jua.


Akizungumza wakati akipokea taarifa ya mradi huo Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Jiri amekiri kupokea mradi huo na kutoa wito kwa wananchi mkoani humo hasa wakazi wa Visiwani kuchangamkia fursa hiyo kwani tayari Serikali imetoa ruzuku. 

“Kila kaya itakuwa na mfumo wake wa kujitegemea, wito wangu kwa wananchi hasa wakazi wa visiwani tuchangamkie fursa iliyokuja, kama mmoja angekuwa anafunga mwenyewe mfumo wa umeme jua inawezekana ikawa gharama kubwa sana lakini Serikali imetoa ruzuku mpaka asilimia sabini na tano (75%)”. Amesema Bi. Zuwena. 

Sambamba na hilo Bi.Zuwena amewataka wananchi wa Mkoa wa Lindi kuchangamkia fursa ya Majiko Banifu ambapo serikali imetoa ruzuku ya 85% na kufanya gharama ya Jiko moja kuuzwa kwa Shs 9000 tofauti na bei halisia Shs 60000.

Kwa upande wake, Meneja wa Teknolojia za Nishati kutoka REA, Mha. Michael Kyessi amesema mradi unategemea kusambaza Majiko Banifu 5,576 kwa Mkoa wa Lindi ambapo Majiko 1,115 yatagawanywa kwa kila wilaya.

“Gharama ya mradi kwa mkoa wa Lindi ni shilingi 346,560,000.00  ambapo Serikali itatoa ruzuku ya shilingi 294,576,000.00 . Mtoa huduma ni Tango Energy Ltd ambapo jumla ya majiko banifu 5,776 yatauzwa kwa wananchi kwa bei ya ruzuku. Gharama ya jiko moja ni TZS 60,000 kabla ya ruzuku, hivyo serikali itatoa ruzuku ya asilimia 85 sawa na TZS 51,000 na mwananchi atanunua jiko hilo kwa  shilingi 9,000.  Majiko haya yatasambazwa katika wilaya tano za Mkoa wa Lindi”. Amesema Mha. Kyessi. 

Kuhusu mradi  wa jua ambao utafikia kaya 1,227 ndani ya visiwa vitano mkoani humo, Mha. Kyessi amebainisha  mifumo hiyo imegawanyika katika mafungu matatu ya uwezo wa nishati ambayo ni 50Wp, 80Wp na 100Wp. Jumla ya mifumo ya 50Wp ni 736, 80Wp ni 307 na 100Wp ni 184.

 

“Gharama ya ruzuku imetolewa kwa asilimia na kila atakayefungiwa mfumo wa uwezo wa Wati hamsini (50Wp) atapata ruzuku ya 75%, mfumo wa Wati themanini (80Wp) atapata ruzuku ya 65% na mfumo wa Wati mia moja (100Wp) atapata ruzuku ya 55%”. Amesema Mha.Kyessi


Gharama za mradi kwa mkoa wa Lindi ni shilingi miilioni 801.74 ambapo ruzuku ni shilingi milioni 544.21 sawa na asilimia 68 ya gharama zote ya mradi na shilingi milioni 257.53 ni fedha toka kwa wanufaika. 


Katika Mkoa wa Lindi mradi huo unategemea kuhudumia visiwa vitano na mtoa huduma mmoja  ambaye anategemea kuhudumia visiwa hivyo kupeleka jumla ya mifumo 1,227 ndani ya kipindi cha miaka miwili.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATOA WITO WADAU KUIMARISHA USHIRIKIANO NA SERIKALI

August 19, 2025 Add Comment

































Na Mwandishi Wetu – Dodoma

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali, sekta binafsi na taasisi za dini kuimairisha ushirikiano na Serikali na kujiunga katika mtandao wa kitaifa wa usimamizi wa huduma za kibinadamu.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Willium Lukuvi wakati akimwakilisha Waziri Mkuu katika Maadhimisho ya Siku ya Watoa Huduma za Misaada ya Kibinadamu Duniani tarehe 19 Agosti, 2025 Jijini Dodoma.


“Ninatoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali, sekta binafsi na taasisi za dini kuimairisha ushirikiano na Serikali na kujiunga katika mtandao wa kitaifa wa usimamizi wa huduma za kibinadamu, kwa kufanya hivyo kutaongeza uratibu, uwajibikaji na ufanisi katika kushughulikia majanga” ameeleza

Aidha, amesisitiza watoa huduma za kibinadamu kutia mkazo katika suala la kuelimisha umma ili wananchi waweze kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu ili kuweza kupunguza athari za majanga pindi yanapotokea.


“Kwa kuwa yapo majanga ambayo hayakwepeki, ninawasihi sana watoa huduma za kibinadamu, kutilia mkazo suala la kuelimisha umma. Wananchi waelimishwe kuzingatia maelekezo yanayotolewa na watalaamu ili kupunguza athari za majanga yanapotokea” amefafanua.

Mbali na hayo amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mikakati na kampeni zote za uhifadhi na utunzaji wa mazingira kwani kwa kufanya hivyo kutawezesha katika kukabiliana na majanga hususan yale ya asilia.

“Suala na utunzaji wa mazingira ni muhimu sana katika kukabiliana na majanga hususan yale ya asilia, nitoe wito kwa wananchi wote kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mikakati na kampeni zote za uhifadhi na utunzaji wa mazingira. Hatua mojawapo muhimu ni kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi hivyo niwakumbushe Watanzania wote kushiriki kikamilifu katika kampeni hizo muhimu za Kitaifa” amesisitiza.

 Akizungumza kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge unaotarajiwa kufanyika 29 Oktoba, 2025 amewataka Watanzania kushiriki kikamilifu katika kuwachagua Viongozi wao akiwemo Rais, Wabunge na Madiwani. 

“Tujitokeze kwa wingi kutumia haki yetu ya kikatiba, kila Mtanzania atambue kuwa kupiga kura ni haki na wajibu wake ili kuwapata viongozi bora watakaoharakisha maendeleo ya taifa letu” amesisitiza Waziri Lukuvi.

Maadhimisho ya Siku ya Watoa Misaada ya Kibinadamu Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 19 Agosti, Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo kwa mwaka 2025 inasema 

“Kuimarisha Utoaji wa Huduma za Kibinadamu na Ustahimilivu Dhidi ya Majanga.” 

CHILUBA ACHUKUA FOMU KUTETEA KITI CHAKE

August 19, 2025 Add Comment

 


Diwani wa kata ya Mzizima, Chiluba Fredrick akiwa kwenye ofisi za kata hiyo tayari kuchukua fomu, wa pili kulia kwake ni katibu wa kata hiyo Amiri Mligu.










Na Hamida Kamchalla, TANGA.

ALIYEKUWA Diwani wa Kata ya Mzizima kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Chiluba Fredrick amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo tena huku akiomba ushirikiano kwa wananchi na wanachama wote kwa ujumla kuhakikisha wanakipa chama hicho ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Chiluba ameyadema hayo wakati alipochukua fomu ya iuwania nafasi hiyo baada ya kupitia kwenye kura za maoni ambapo pia amewashukuru wananchi pamoja na wajumbe kwa kukuamini na kumpa nafasi hiyo.

"Nashukuru sana wana chama wa chama cha mapinduzi kwa kuendelea kuniamini na kunipa ridhaa tena ya kupeperusha bendera kwa kiti cha udiwani kata ya mzimaa,

"Naomba ushirikiane katika kampeni na pia kuhakikisha tunakipa chama Cha mapinduzi ushindi kwa kuwachagua Rais Mbunge na Diwani wa chama Cha mapinduzi" amesema.

JWT TANGA YAMSHUKURU RAIS DKT SAMIA KWA KUTATUA KERO ZA WAFANYABIASHARA

August 19, 2025 Add Comment




Na Oscar Assenga,TANGA

JUMUIYA wa Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Mkoa wa Tanga imemshukuru Rais Dkt Samia Sukuhu kwa kutatua kero za wafanyabiashara na hivyo kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi kutokana kuondolewa kwa vikwazo ambavyo walikwa walikabiliana navyo awali.

Hayo yalisemwa leo na Katibu wa JWT mkoa wa Tanga Ismail Masoud wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga kutoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu na Serikali kwa mambo aliyoyafanyia wafanyabiashara Tanzania hatua ambayo imepeleka kupandisha mapato kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Masoud ambaye pia ni Mjumbe Bodi ya Jumuiya ya Wafnyabiashara Tanzania (JWT) alizitaja changamoto ambazo awali zilikuwa zinawakili na sasa zimepatiwa ufumbuzi ni pamoja na umeme ambapo alisema ulipelekea kutokuzalisha kisawasawa kutokana na matatizo ya umeme .

Alisema kufuatia uwepo wa changamoto hiyo,Serikali ya awamu ya sita ilitatua tatizo hilo kupitia Bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo limekwisha na hivyo kupelekea kuondoa mgao wa umeme hivyo wanaishukuru awamu ya sita na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa makusanyo.

Akizungumza changamoto ya utoaji wa mizigo Bandarini alisema kwamba hapo awali ilikuwa ni changamoto lakini kwa sasa sio tatizo limekuwa ni historian a mizigo inatoka kwa haraka na wanalipa kodi kikamilifu na hivyo kupelekea kuchangia maendeleo.

“Lakini Mfumo wa ulipaji kodi TRA umeboresha kwa kiasi kikubwa na wafanyabiashara tunalipa kodi kwa hiari na tunavuka malengo kwenye ulipaji kodi na unajua mwezi Julai tulivuka malengo kutokana na juhudi za awamu ya sita na TRA mikoa yote na TRA imeboresha na kutimiza malengo yake kisawasawa na huo ni ushirikiano na Taasi za wafanyabiashara na tunalijenga Taifa kwa pamoja kufikia malengo ya awamu ya sita kukusanya mapato na kutoa elimu”Alisema

Akizungumza namna ambayo Serikali inawajali na kuwathamini wafanyabiashara Katibu huyo alisema kwamba kwa kipindi cha miaka minne iliunda tume tatu kwa ajili ya wafanyabiashara, kamati ya kariakoo ambayo ilizunguka nchi nzima kukusanya maoni na kuangalia changamoto za wafanyabiashara.

Alisema baada ya kuzungumza baadae ilitoa mapendekezo ambayo serikali iliyafanyia kazi na matokeo yake kwa sasa biaishara zimetulia na wanalipa kodi bila shuruti

Alisema pia Serikali iliunda kamati ya Ombeni Sefue iliundwa na Rais kufuatia mwendezo wa ulipaji kodi na matatizo ya mifumo ya ulipaji kodi Tanzania na mapendekezo yake yanafanyiwa kazi na hivyo wanategemea yatafanyiwa kazi na kuleta tija kwa ulipaji wa kodi Tanzania na kamati hiyo ilifika Tanga kutafuta kero za wafanyabiashara.

Hata hivyo alisema nyengine ni Tume ya kuchunguza biashara kwa wageni ambapo awali kulikuwa na matatizo ya wageni hasa Wachina walikuwa Tanzania wanafanyabiashara zinazofanywa na wazawa hivyo iliundwa na Waziri wa Viwanda na Baishara kwa malekezo ya Rais mwenywe na ilifanya kazi na kupeleka mapendekezo kwa Rais kwamba baadhi ya biashara zitafanywa na watanzania wenyewe huo ni upendo mkubwa sana kwa Rais anawalinda wafanyabiashara wa Tanzania kwa vitendo .

Alisema pia wanaipongeza Serikali kwa kuunda kama zote ambazo zinaonyesha Serikali inafuatilia mwendenzo wa wafanyabiashara na kwamba nini kinatakiwa katika sekta ipi ili wafanyabiashara waweze kuondokana na vikwazo walivyokuwa navyo kwa wastawi na Taifa.

“Ukipiga mahesabu utaona kwa kipindi cha miaka minne unakuta kila mwaka Serikali ilikuwa inaunda Tume ya wafanyabiashara tu pelekee inaonyesha namna inavyowajali lakini imepunguza VAT kutoka asilimia 18 mpaka 16 hapo wamsikilize kwa watanzania wanaonunua bidhaa kwa matumizi yao binafsi yatakayofanyika kwa kutumia mtandao ili kuboresha maisha ya watanzania na wafanyabaishara nchini hivyo ni hatua kubwa kwa kuwajali wananchi wa Tanzania.

Hata hivyo akizungumzia suala la Hotel Levy alisema kwamba katika upande huo Serikali ya awamu ya sita wanaipongeza kupunguza tozo ya Hotel ambapo awali ilikuwa ni asilimia 10 na sasa imeshuka mpaka asilimia 2 ambapo ni punguza kwa asilimia 80 hiyo inawasadia wafanyabaishara wa mahoteli kurekebisha hoteli zao na kuhakikisha zinakuwa bora zaidi na kuwavutia wateja na kukusanya mapato zaidi na kulipa kodi zaidi na kuendeleza taifa letu kwa ustawi wa wafanyabiashata wa hotel.

Hata hivyo alisema kwamba Jumuiya hiyo inaihakikishia Serikali watashirikiana na Taasisi za Serikali kutoa elimu ya mlipa kodi kwa wafanyabaishara wote ili walipe kodi bila shuruti ,kodi stahiki kufuati kauli tya Rais Samia kwamba hataki kodi hya dhuluma hiyo ni kauli dhabiti ina hofu ya Mungu na kamishna wa TRA anaisimamia kikamilifu.

Awali akizungumza Makamu Mwenyekiti JWT Mkoa wa Tanga Fredy Mmasy alisema kwamba wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kutokana na hali ya utulivu wa biashara katika Jiji la Tanga na Tanzania kwa ujumla na hata wanaona makusanyo ya kodi kazi kubwa inayosimamiwa na kufanywa na Serikali .

Alisema kutokana na makusanyo hayo makubwa imepelekea ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ikiwemo barabara kubwa ,ujenzi wa hospitali ,shule na ununuzi wa Ambulence za kubebea wagonjwa yanayonunulwa kwa kodi na hata wigo wa mapato kwa mkoa umeongenezaka kwa hivyo wanamshukuru kwa kusimamia vizuri na hivyo wao kama wafanyabiashara wanaona mafanikio wao wafanyabishara

Naye kwa upande Mfanyabiashara wa Tanga barabara ya kumi Jijini Tanga Pateli alisema kwamba wanampongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kutatua kero za wafanyabiashara na hivyo kupelekea uwepo wa mazingira ya ufanyaji wa biashara kwao jambo lililopelekea kuzifanya kwa ufanisi na kutokusumbuliwa kama ilivyokuwa awali.

Alisema kwamba hata upande wa kodi wakienda mamlaka ya Mapato TRA wanapata ushirikiano mzuri na kwa sasa hawana changamoto kama zilizokuwepo awali na hivyo kuendelea na shughuli zao.

Akizungumza kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mapato TRA Thomas Masese aliwashukuru wafanyabiasha na walipa kodi kwa ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka kwao pamoja na kuipongeza Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Mkoa wa Tanga kwa jinsi wanavyoshirikiana.

Alisema kwamba moja ya mashirikiano hayo ni pamoja na kufanya mikutano na semina za wafanyabiashara kwa kushirikiana nao kupitia wilaya mbalimbali kuelimisha na kusikiliza kero za wananchi na hivyo namna ushirikiano huo uendele kutokana na kuwa chachu kubwa kwao .

Aidha alisema kutokana na ushirikiano huo ulipelekea mwaka jana 2024/2025 ambapo walikuwa na lengo la kukusanya Bilioni 335 na wakakusanya Bilioni 330 ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 98 ukilinganisha na mwaka wa nyuma yake mwaka 2023/2024 ambayo walikusanya Bilioni 204 ukilinganisha na mwaka 2024/2025 ambazo wamekusanya Bilioni 330 imekuwa na ongezeko la Bilioni 126 ambazo ni asilimia 61.

Meneja huyo alisema kwamba mwaka huu wamepewa lengo la kukusanya bilioni 361 lakini kwa ushirikiano uliopo kati yao na Jumuiya ya Wafanyabiashara na walipa kodi wanamatumaini watalifikia lengo hilo huku akitoa wito waendelee kushirikiana ili kuweza kukusanya kiwango hicho.

Alisema lakini pia Bandari ya Tanga imefunguka kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Serikali kwa kuongezewa uwezo wa kupokea meli kubwa mbili zinazoweza kufunga wakati mmoja.

Hata hivyo aliwataka watanzania kuendelea kupitisha shehena zao za mizigo na bidhaa katika Bandari ya Tanga na kwamba upitishaji wake wa mizigo hauchukua muda mrefu kutokana na kutokuwa na msongamano .

Naye Mfanyabiashara wa Vifaa vya Ujenzi na Umeme Jijini Tanga Alphonce Mboya alisema kwamba wana mashukuru Rais Dkt Samia Suluhu kutokana na kuzipatia ufumbuzi changamoto ambazo ilikuwa zikiwakabili ikiwemo lile la kulipishwa madeni ya nyuma ya miaka saba iliyopita ambao alisema wasilipishwe.

“Tunamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kutokana na kuwathamini wafanyabiashara na kuwaondolea vikwazo ambavyo vilikuwa vinatukabili na sasa tunafanya shughuli zetu kwa uhuru “Alisema Mwisho.