TADB na TWCC Waingia Mkataba Kuinua Wanawake na Vijana Kwenye Kilimo
habariJUKWAA LA NNE LA UTEKELEZAJI WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI LILETE MABADILIKO -OLLAL
habariMWANZA
Wadau wa madini nchini wametakiwa kutumia Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta la Madini kama kichocheo cha mabadiliko katika Sekta ya Madini hasa kwenye eneo la ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini katika eneo la ajira na utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini kama vile usambazaji wa vifaa na vyakula.
Hayo yamesemwa jijini Mwanza leo Juni 18, 2025 na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Madini, Augustine Ollal kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo wakati akifunga Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta la Madini.Jukwaa hilo lililoanza mapema Juni 16, 2025 limekutanisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wizara ya Madini na Taasisi zake, Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsi, Taasisi za Fedha, Kampuni za Uchimbaji wa Madini na Watoa Huduma kwenye Migodi ya Madini.
![]() |
![]() |
Amesema kufanyika kwa jukwaa hilo ni mkakati wa Serikali kupitia Wizara ya Madini kuhamasisha ushiriki wa watanzania katika shughuli za uchimbaji, uchenjuaji, biashara ya madini na usambazaji wa bidhaa na huduma kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ili wananchi waendelee kunufaika na rasilimali madini na kukuza uchumi wa nchi.
Katika hatua nyingine, amezitaka kampuni za madini kuendelea kutoa kipaumbele kwa watanzania kwenye ajira na utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini.
Wakati huo huo amempongeza Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde kwa kutafsiri maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vitendo kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini hali iliyopelekea mchango wake katika Pato la Taifa kufikia asilimia 10.1.
Jukwaa hilo lenye kaulimbiu inayosema Ongezeko la Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini ni chachu ya Ukuaji wa Uchumi limeambatana na maonesho yenye lengo la kuelimisha kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini.
WAENDELEZAJI WA MRADI WA KUZALISHA UMEME WA LUPALI MKOANI NJOMBE WAELEKEZWA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA WA MRADI
habari-Utekelezwaji wake wafikia 97.5%
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu ameelekeza waendelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa kilowati 317 kwa kutumia maporomoko ya Mto Lupali kuimarisha ulinzi na usalama wa mradi ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Ameelekeza hayo Juni 18, 2025 katika Kata ya Matola Wilaya ya Njombe Mkoani Njombe alipofanya ziara iliyolenga kujionea maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo unaosimamiwa na Watawa wa Kanisa Katoliki wa Shirika la Wabenediktini, Imiliwaha Njombe kwa ufadhili wa REA.
"Mradi huu hadi kufikia hatua hii umetumia gharama kubwa, na ni mradi utakaokuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa maeneo haya na Taifa kwa ujumla, tuna kila sababu ya kuhakikisha unalindwa," alielekeza Balozi Kingu.
Alielekeza kujengwa kwa uzio utakaozunguka bwawa la kuzalishia umeme sambamba na kusimika mifumo ya taa na kamera maalum za ulinzi maarufu kama CCTV Camera maeneo yote muhimu ya mradi.
Sambamba na hilo, Balozi Kingu aliwapongeza kwa hatua waliyofikia na aliwaelekeza waendelezaji wa mradi huo kushirikiana kwa karibu na waendelezaji wa miradi mingine ili kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa miradi.
"Hapa mmezungukwa na waendelezaji wa miradi ya namna hii wenye uzoefu, ni vyema mkajenga utaratibu wa kuwa mnabadilishana uzoefu ili kuimarisha uendeshaji wa mradi," alisisitiza Balozi Kingu.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mratibu wa Mradi, Sista Imakulata Mlowe alitoa shukrani kwa uwezeshwaji unaofanywa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na aliahidi kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Balozi Kingu.
"Tangu kuanza kwa mradi mwaka 2011, REA imetuwezesha sehemu kubwa katika hatua zote; tunaahidi kutimiza maelekezo yote yaliyotolewa," alisema Sista Mlowe.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka REA, Mhandisi Advera Mwijage alisema hadi sasa REA imewezesha zaidi ya shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.
"REA imetoa ruzuku kwa awamu tofauti kwa kushirikiana na wabia wa maendeleo wakiwemo benki ya Dunia na Serikali ya Sweden ili kuwezesha mradi huu tangu hatua za mwanzo za utafiti wa awali, ujenzi wa njia kuu za kusafirisha na kusambaza umeme kwa watumiaji takriban 600.
Mhandisi Advera alibainisha maeneo mengine yaliyowezeshwa na REA kuwa ni pamoja na ruzuku iliyotolewa kukamilisha mradi ikihusisha ujenzi wa sehemu ya kupokelea maji, nyumba ya mtambo, uwekaji wa mabomba pamoja na shughuli nyingine za Mradi.
Alisema kukamilika kwa mradi kutazalisha kiasi cha kilowati 317 ambazo kiasi zitatumiwa na mwendelezaji na kiasi kitakachobaki zitaingizwa katika Gridi ya Taifa.
Alisema kuwa REA imeendelea kufadhili miradi ambayo itaongeza wigo wa Gridi ya Taifa ili kukuza uchumi wa Taifa kwa kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi.
"REA imefadhili miradi ya uzalishaji na usambazaji nishati vijijini inayotekelezwa na taasisi mbalimbali za Serikali na Sekta Binafsi kwa kutoa ruzuku pamoja na kuwezesha mikopo ya masharti nafuu sambamba na kuwajengea uwezo waendelezaji wa miradi," alisisitiza Mha. Mwijage.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu yupo Mkoani Njombe kwa ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya uzalishaji na usambazaji wa umeme inayowezeshwa na REA.

