VIKUNDI 40 VYA WANAWAKE ,VIJANA NA WENYE ULEMAVU SAME VYAKABIDHIWA MIKOPO YA MILIONI 194

April 20, 2025

 


  Na Ashrack Miraji Tangarahatz Blog  

Vikundi arobaini (40) vya wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu katika wilaya ya Same vimekabidhiwa mikopo isiyo na riba ya asilimia kumi ya mapato ya halmashauri yenye thamani ya Shilingi milioni 194 awamu ya pili ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali katika kuwawezesha wananchi kujikwamua  kiuchumi.

Hayo yamebainishwa Aprili 17,2025 na Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Kasilda Mgeni wakati wa hafla ya kukabidhi mfano wa hundi kwa vikundi hivyo ambapo amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia vizuri na kuirejesha kwa wakati ili kunusuru upotevu wa fedha za serikali.

“Kumbukeni fedha hizi sio za msaada, huu ni mkopo usio na riba hivyo lazima zilipwe, Niwaombe wanufaika wote ambao mmepata mikopo hii mhakikishe mnafuata matakwa ya kisheria za mikataba ya mikopo hiyo na pale mnapokiuka hatua za kisheria zitachukuliwa haraka ili kunusuru upotevu wa fedha za Serikali” Amesema Mhe. Kasilda.

Sambamba na hayo Mhe. Kasilda amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita imetoa milioni 308 kwa Halmashauri ya wilaya ya Same kwa ajili ya mikopo na mpaka sasa imetolewa milioni 194 kwa vikundi vilivyokidhi vigezo ambapo amewasisitiza Maafisa Maendeleo ya Jamii na timu ya Uhakiki wa vikundi wilayani hapa kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuwapa uelewa kuhusu mikopo hiyo.

Naye Afisa maendeleo ya jamii wa wilaya ya Same, Charles Anatoly amesema kuwa walipokea maombi ya mikopo kutoka kwenye vikundi 74 na baada ya kufanya tathmini na uhakiki vikundi 40 vilikidhi vigezo vya kupata mikopo hiyo huku Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Yusto Mapande akieleza kuwa mwamko wa vijana umekuwa ni mdogo na kuwasisitiza kuchangamkia fursa hizo.

Wawakilishi kutoka katika makundi hayo matatu ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wameishukuru serikali ya Awamu ya sita kwa kuendelea kuwajali na kuwathamini huku wakiahidi kuifanyia kazi mikopo hiyo kulingana na maandiko ambayo waliwasilisha wakati wa maombi ili waweze kuirejesha kwa wakati.

Mikopo hiyo imetolewa kwa Vikundi vya wanawake 27 ambavyo vimepokea kiasi cha shilingi milioni 134, vikundi nane vya vijana vimepokea milioni 39 na vikundi vitano vya watu wenye ulemavu vimepokea milioni 20.



 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng