
Na Paskal Mbunga, TANGA
Mkuu wa wilaya ya Tanga Japhari Kubecha ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa kutengeneza ubunifu wa kuan daa tamasha la Diko la Amboni ambapo kupitia kampeni hiyo imeleta hamasa kubwa ya utalii wa ndani katika mkoa huu na hivyo kukuza utalii.
Mkuu huyo wa wilaya aliihaidi mamlaka hiyo kwamba Serikali ya wilaya Tanga itaendelea kushirikiana nao kuendeleza na kutunza mapango hayo ya pekee .

“Lakini niwapongeze uongozi wa NCAA kwa kuweza kuinua hadhi ya Mapango ya Amboni ambayo ni kivutio kikubwa kwa watalii kutoka ndani na nje kutembelea eneo Hilo.
"Hivyo kutokana na hamasa hii tutaweza kuongeza pato la nchini”Alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Tanga.

Awali, akimkaribisha Mgeni huyo rasmi kwenye tamasha Hilo, Mhifadhi Mkuu Msaidizi anayesimamia huduma za utalii na masoko (NCCA), Mariam Kobelo, alisema NCAA inaendelea kuboresha miundo mbinu katika eneo Hilo la Mapango ya Amboni yaliyoko Jijini hapa ili yaendelee kuvutia watalii wengi zaidi.
Alisema harakati hizo ni za kuboresha miundo mbinu mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa mapato, kujenga maeneo ya kupumzikia na kuweka kambi za watalii watakaopenda kulala hapo.

Mhifadhi huyo Mkuu Msaidizi alifahamisha kwamba kuhitimishwa kwa kampeni hii leo, itawezesha kufungua ukurasa Mpya utakaoleta fursa ya kipato Kwa wajasiriamali wadogo walioko wilayani hapa.
"Kama mlivyoona tumeendesha mashindano ya mapishi Kwa akina mama wajasiriamali. Washindi wamepatikana watatu na wamekabidhiwa zawadi za fedha taslimu kuanzia laki moja Hadi laki nne. Lengo ni kumwunga mikono Rais Samia katika kampeni yake ya matumizi ya majiko ya gesi", alisema Kobelo.
Mwisho.
EmoticonEmoticon