TAKUKURU TANGA YAPAISHA MAKUSANYO YA MAPATO YATOKANAYO NA ADA ZA LESENI ZA BIASHARA, IKIWEMO USHURU WA HUDUMA

November 09, 2024





Akitoa taarifa ya utendaji kazi ya miezi mitatu ya TAKURU Mkoa wa Tanga kwa waandishi habari leo, Mkuu wa TAKUKURU Mkoani hapa, Ramadhani A. Ndwatah alisema mafanikio hayo yamepatikana kutokana na juhudi za pamoja na Halmashauri ya Jiji la Tanga ambapo katika kipindi cha miezi mitatu kati ya mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu,

Alisema Halmashauri ya Jiji la Tanga ilikusanya mapato yenye jumla ya shs.1,938,185,915/22 ukilinganisha na shs,1,246,611,579/43 ambayo na sawa na wastani wa asilia mia 22.6 ya lengo la mwaka zilizokusanywa kwa miezi mitatu iliyopita.

Alifafanua kuwa kwa kipindi cha Julai-Septemba, 2024, TAKUKURU Mkoa wa Tanga imetekeleza jukumu lake la Uzuiaji Rushwa, Elimu ka umma na uchunguzi na mashtaka.

Akibainisha kuhusu utekelezaji wa jukumu la Uzuiaji Rushwa na Chambuzi za Mifumo, Ndwatah alisema ili kupata imara isiyokuwa na mianya ya rushwa na kukwamisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi na utendaji kazi za serikali, walifanya chambuzi cha mifumo 17.

Alisema miongoni mwachambuzi za mifumo iliyofanyika ni pamoja na uchambuzi wa mfumo wa ukusanyaji mapato kupitia leseni za biashara katika halmashauri zote za mkoa wa Tanga, uchambuzi wa mfumo wa usimamizi na ukusanyaji wa ushuru wa huduma (Service Levy) kwa wafanya biashara na wakandarasi wanaofanya kazi na Taasisi za Serikali Mkoani hapa.

Kuhusu Ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Mkuu huyo wa TAKUKURU (M) alisema wamefuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ipatayo 41 yenye thamani ya shs. 19,072,592,007/= katika sekta za kipaumbele ambazo ni Elimu, Barabara, Maji na Afya.

Alisema TAKUKURU (M) kupitia ofisi za wilaya zote zimeweza kufanya ufuatiliaji wa karibu wa hatua za awali za miradi ya BOOST ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa kamati zinazosimamia miradi hiyo.

Miongoni mwa mirdi hiyo, miradi 13 yenye thamani ya shs.11,850,561,101/=Imebainika kuwa na mapungufu kadhaa na kati ya miradi hiyo, miwili imefunguliwa majalada ya uchunguzi. Miradi hiyo ni Uboreshaji wa miundo mbinu ya maji (HTM) wilayani Korogwe wenye thamani ya shs.407,169,032/= na ujenzi wa jingo la utawala lenye thamani ya shs.2,800,000,000/=.

Pia alizungumzia uchunguzi na mashtaka ambapo alisema katika kipindi cha Julai hadi Septemba, 2024, TAKUKURU ilipokea jumla ya taarifa 109 ambapo taarifa 73 zinahusu vitendo vya rushwa na taarifa 36 hazihusu vitendo ambapo taarifa 27 zimefungwa taarifa 06 zimehamishiwa idara nyingine na taarifa 76 zinaendelea kuchunguzwa.

Kuhusu mashtaka, Mkuu huyo wa TAKUKURU alibainisha kuwa wamefungua mashauri 02 mahakamani ambapo Jamhuri ilishinda shauri 01 linaendelea mahakamani. Alisema jumla ya mashauri 23 yanaendelea katika mahakama mbalimbali Mkoani hapa.

(mwisho).

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »